Watanzania wanalia, Rais wetu Magufuli upo wapi?

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Habari wana jamvi,

Kila aliyepo DSM naamini anajua kinachoendelea kwa sasa,habari ya mjini ni hii bomoa bomoa ya nyumba za mabondeni.Kwa kweli inaumiza sana,ukipita pale Mkwajuni kwenye kibonde karibia nyumba zote zimesafishwa kabisa.Kinachouzunisha mimi ni kwamba hata nyumba za kwenye kilima zinabomolewa.

Rais wetu Magufuli kumbuka ulisema wewe una huruma na watanzania,fikiria wale binadamu wataishije kwa kipindi hiki,fikiria pia kwamba mtu kaishi DSM pengine zaidi ya miaka 20 ndio akajenga kijumba chake,halafu ninyi mnabomoa kwa siku moja, kweli ni haki hiyo?

Fikiri mtu ambaye hana kazi ya kumpa kipato cha kutosha leo hii anabomolewa kijumba chake,anayepika chapati na kushona viatu leo ataishije?

Mbaya zaidi hili zoezi limekuja mwisho wa mwaka,kipindi cha wapangaji kulipa kodi,xmass watoto wanahitaji kuvaa,ada za shule watoto kulipiwa na kijumba kinabomolewa. Je, hayo ni maisha?

Mbona lile ghorofa pacha za pale mtaa wa Indra Gandhi Posta linalohitajika kubomolewa baada ya pacha lake kuanguka hadi leo halijabomolewa, kama sio uonevu ni nini?

Inauma sana
 
Ndio maana nasema 2020 Magufuli atapata kura za vijijini tu ila huku mijini ataisoma namba.

Cha ajabu hakuna Afisa ardhi wala mtaalamu wa Mipango miji aliewajibika mpaka saa ili hali kuna baadhi ya maeneo wananchi walipewa vibali vya ujenzi.
 
Magufuli anaokoa vifo vya watu waliojenga mabondeni kwa matendo. Nchi nyingi sana raia zake wengi hufa sana katika mafuliko kwa sababu ya kujenga kiholela. Asia na ratin America watu wengi sana wamejenga mabondeni na huwa wateja wa mafurico kila kukicha. Usiwe na huruma katika kusafisha jiji la DSM.
 
wakipata mafuliko huililia serikali...wakibomolewa huililia serikali.

kipi ni afadhali...
 
Umetolea mfano hiyo ghorofa ya city centre hiyo inataka ujuzi kuitelemsha na sidhani kama kuna mtu wa kuogopwa hapo muda utafika.Kuhusu mabondeni kweli jamani mara ngapi madhara yanatokea na mwisho watu wana ilalamikia serikali haiwajali!tufike mahali tuyatizame mambo kiuhalisia.
 
Magufuli anaokoa vifo vya watu waliojenga mabondeni kwa matendo. Nchi nyingi sana raia zake wengi hufa sana katika mafuliko kwa sababu ya kujenga kiholela. Asia na ratin America watu wengi sana wamejenga mabondeni na huwa wateja wa mafurico kila kukicha. Usiwe na huruma katika kusafisha jiji la DSM.

Pia anaokoa pesa za walipakodi baada ya mafiriko waanze kugharamikiwa na serikali
Mihimu amabao hawajapata viwanja wapewe
 
Ukijenga bondeni kwenye maeneo yasiyofaa bila kufuata utaratibu wowote halafu mvua ikija unataka Serikali ikusaidie huku ukijua unaishi bondeni hilo halikubaliki kabisa...nawashauri watanzania sasa tuheshimu sheria za nchi ww mwenyewe badilika acha kujijengea hovyo tu...nadhani Rais akiwasikiliza ni kuwapeni muda muondoke wenyewe mabondeni sio kuwaacha mkae humo
 
Ninachozungumzia ni kwa nini wanabomoa hata ambazo hazipo bondeni? Zingine zipo kwenye muinuko kabisa
 
Huu mwaka ni wa mafuriko..yaani el nino. Kwa hiyo tusubiri wafe ndo tuwaokoe ?
 
Ndio maana nasema 2020 Magufuli atapata kura za vijijini tu ila huku mijini ataisoma namba.

Cha ajabu hakuna Afisa ardhi wala mtaalamu wa Mipango miji aliewajibika mpaka saa ili hali kuna baadhi ya maeneo wananchi walipewa vibali vya ujenzi.

Mkuu kwahiyo mjini atapata kura nyingi Ikiwa watu watasombwa na mafuriko ama??
 
Mimi nasema hivi, pale bondeni waachwe kambale tu. Uhuni wa kujifanya mnakaa mjini mpk mkajenge mtoni wa nini?

Tangu katazo liwekwe, nyumba zimeongezeka kwa asilimia 40. Wavunjiwe na wacharazwe bakora 2 familia nzima
 
Back
Top Bottom