Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 39,759
- 25,651
Ndugu zangu Watanzania,
Nimeendelea kuzisikiliza sauti za Watanzania kutoka mitaani, imeendelea kusikia maoni na uchambuzi wa watanzania kutoka vijiwe mbalimbali juu ya Uongozi Wa Rais Samia na serikali Yake,Nimetega masikio vyema Sana kwa kuwa napenda kupata mitizamo na maoni ya Watanzania juu ya Rais Samia na serikali yake ya CCM kutokana na ukweli kuwa Mimi binafsi Namuunga mkono Rais Samia na serikali Yake ya CCM kwa asilimia Mia moja.
Muda wote nipo tayari kutoa majibu kwa watu juu ya kazi kubwa aliyoifanya Rais Samia na serikali Yake ndani ya muda mfupi wa uongozi wake,Ndio maana nimekuwa mfuafiliaji mkubwa wa Taarifa mbalimbali za serikali yangu ya CCM na utekelezaji wa ilani yake iliyoleta Tabasamu na matumaini katika mioyo ya Watanzania.
Nilichogundua na kupata majibu ni kuwa kwa hakika watanzania Wana Imani kubwa Sana na Rais Samia na serikali Yake, wanamwamini Sana na kumuunga mkono kwa nguvu zao zote, katika mazungumzo yao watanzania wanafanya hivyo kutokana na kuguswa na utendaji kazi na uchapa kazi wa Rais Samia, wengi wameridhishwa na hatua mbalimbali za kiutendaji ambazo amekuwa akichukua Rais Samia katika utatuzi wa kero na changamoto mbalimbali.
Rais Samia Ameiteka mioyo ya watanzania, hata palipo na sintofahamu ya aina yoyote bado Watanzania wameelekeza macho, masikio kwake kwa matumaini makubwa Sana, wote wanaamini katika uimara, ushupavu,ujasiri na umadhubuti wake kiuongozi,hawana shida Wala wasiwasi juu yake.
Watanzania wanafahamu na kutambua ya kuwa Rais Samia siyo mkurupukaji katika maamuzi yake ya kiuongozi, wanatambua ya kuwa Nikiongozi mtulivu na mwenye Subira,Ni kiongozi anayefanya mambo na kuchukua hatua baada ya kuwa na kila kitu mkononi mwake kinyaraka na kitaarifa.
Ni kiongozi Ambaye huwezi ukajuwa Ni wakatia gani atafanya Nini Ila Ni lazima ufahamu wakati wote kuwa Rais Samia Hana Subira Wala mzaha katika maslahi ya Taifa, hana Subira Wala simile katika kumuwajibisha mtu yeyote yule bila kujali sura yake au Dini au kabila au ukanda wake anaotokea au familia yake ikiwa atabainika Kuchezea pesa za umma na kwenda kinyume na maadili ,kanuni, sheria, miongozi na taratibu za umma.
Watanzania wanafahamu namna Rais Samia alivyo na misimamo na asiyeyumba Wala kuyumbishwa,Ni kiongozi mwenye Dira na muelekeo unaoeleweka, ni kiongozi anayelitanguliza mbele Taifa letu na wakati wote amelibeba katika mabega yake kwa ujasiri na ushupavu wa Hali ya juu Sana.
Tuendelee kumwombea Rais wetu Afya njema na nguvu za Kuendelea kututumikia watanzania, Tuendelee kumuunga mkono na kumwamini Sana Rais wetu, Rais wetu Anayo dhamira njema Sana na Taifa letu, tumeona hayo kupitia maneno yake na matendo yake ya kizalendo, tuendelee kumwomba Mungu ili ampatie macho ya rohoni ya kufahamu ni akina nani wanafaa kuwa karibu Yake na wasaidizi wake kiutendaji, Mungu aendelee Kumjalia ujasiri na kumpatia maarifa katika kuliongoza na kulitumikia Taifa letu.
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627