Sasa wewe ambaye hata vyombo vya habari vimedhibitiwa unajuwa idadi ya watanzania wangapi watakuwa wamepigwa risasi na kufa. Unatakiwa kusema hayo maneno ukiwa na vyombo huru vya habari.siyo hivi vya kusifu na mapambio.Japo sikubaliani na hili la kufungia mitandao ya kijamii bila sababu za msingi, lakini huwezi linganisha na Kenya ambako hawafungii mitandao ya kijamii lakini wanawapiga risasi wananchi wanaojaribu kutumia Uhuru wao kupinga matokeo ya uchaguzi.
Ingelikua ni Kenya hadi sasa zaidi ya watu 100 wangekua waneshapigwa risasi na kupoteza maisha. Tanzania zaidi ya kuwatisha na kuwahoji viongozi waliotishia kufanya maandamano, hakuna hata mtu mmoja aliyepoteza maisha. Tanzania hoyeeeeee