Watanzania wameanza kuona nuru

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,443
1,046
Ndani ya Utawala huu wa Rais Samia Suluhu mambo mengi sana yamefanyika katika kuleta maendeleo Tanzania ukiachilia maendeleo katika kuhakikisha kuboresha huduma muhimu za kijamii kama vile Maji, Miundombinu, Afya pia Elimu jambo kubwa zaidi kisiasa ni hili la kufungua mikutano ya kisiasa.

Asilimia kubwa ya Watanzania wamepata matumaini mapya na kujiona kama wametoka gerezani rasmi na kusema utawala wa udikteta umezikwa Rasmi maana Rais;
👉 Ameruhusu mikutano ya hadhara.
👉Mchakato wa katiba kuendele.
👉Afunda siasa za kistaarabu.
👉Ataka yeye, CCM wakosolewe.

Hiki kilikua kilio kikubwa cha vyama vya upinzani na watanzania kwa ujumla lakini ndani ya siku 656 za utawala wake amefanikisha kutuondolea minyororo ya kisiasa Hongera sana Rais Samia Suluhu wewe ni mwanadiplomasia namba moja Africa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom