Watanzania waliotekwa waendelea kusota melini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania waliotekwa waendelea kusota melini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 8, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  HATIMA ya watu 28 wakiwemo Watanzania 14 waliomo kwenye Meli ya MV Aly Zoufecar iliyotekwa na maharamia wakati ikisafiri kutoka Moroni katika visiwa vya Comoro kwenda Dar es Salaam Tanzania, imebaki kizani kutokana na mmiliki wa meli hiyo Amin Dazgarali raia wa Comoro kusema hawezi kulipa gharama alizopangiwa na watekaji.


  Meli hiyo ilitekwa kati ya Oktoba 30 na Novemba 1, mwaka jana na maharamia wa Kisomali katika Bahari ya Hindi. Meli hiyo ilikuwa ifike Tanzania Novemba1, 2010.

  Maharamia hao wanataka walipwe Dola za Kimarekani 150,000 sawa na Sh 222 milioni za Kitanzania ili waweze kuwaachia huru mateka pamoja na meli hiyo. Kiasi hicho cha fedha kimemshitua mmiliki wa meli hiyo ambaye ameweka bayana kuwa hawezi kulipa wala kuichukua na kwamba suala la usalama wa watu waliokuwemo ameziachia Serikali za nchi zao.

  Majina ya Watanzania ambao ni miongoni mwa mateka ni Tomas Hussein ambaye ni mfanyakazi katika meli hiyo. Watanzania wengine ambao ni abiria waliotekwa ni pamoja na Augustin Ilias, Rose Mary Maati, Paul Gue , Didas Kitabazi, Bary Omary, Azizi Juma na Mohamed Bundala. Wengine ni Abdallah Mketo, Shandali Mang, Rahma Mbaba, Stephen Ndane, Othuman Seleman na Tai Hamisi.

  Mbali na raia 14 wa Tanzania pia wamo Wacomoro 11 na raia 4 wa Madagascar, huku kukiwa na taarifa kwamba mhandisi katika meli hiyo, Ali Ben Youssouf (sulla) aliuwa kwa kuchinjwa na maharamia hao muda mfupi baada ya kutekwa kwa meli hiyo.

  Raia wa Comoro ambao wako kwenye meli hiyo ni Soilihi Boinaheri ambaye ni nahodha, Backri Ibrahimm Mohamed Hamadi na Youssouf ambaye kwa sasa ni marehemu hawa ni wafanya kazi katika meli hiyo.

  Wengine ni Maissara Mhadjou, Ascar Alphonse, Kubama Fadhili, Kassimou Ismaila, Abouobi Soeuf Toilab Mlomri na Dhoihikou Athoumane ambao ni abiria. Raia wa Madagasca ni Abdou Ali Meca, Hassan Bao (Bosco), Dodo Leonad na Robi Matelot wote wakiwa ni wafanya kazi ndani ya meli.

  Meli hiyo iliyoondoka mjini Moroni Novemba 3 mwaka jana kuelekea Dar es Salaam, ikiwa na watu 29 ambao wafanyakazi ni tisa na abiria 20.

  Wakala wa Meli toka Kampuni ya Transworld Shipping Co. Ltd, Seif Athumani aliliambia Mwananchi kuwa hadi sasa hakuna mawasiliano baina yao na watu walioko ndani ya meli hiyo ambayo ilitekwa tangu Novemba mwaka jana.

  “Ndugu yangu hadi sasa ninapozungumza na wewe hatuna taarifa zozote toka kwa wenzetu walioko ndani ya meli iliyotekwa, hatujui kama wako hai au la,kwa mara ya mwisho mmiliki wa meli hiyo aliniambia suala hilo hawezi kulishughulikia kwa kuwa kampuni yake haina uwezo wa kulipa gharama zinazotakiwa na maharamia hao,”alisema Athuman.

  Athuman alibainisha kuwa mmiliki huyo ambaye ni raia wa Comoro alisisitiza “Gharama zilizotajwa na maharamia ni kubwa, mimi sina uwezo wa kulipa na meli yangu bora wabaki nayo,suala la usalama wa watu walioko ndani ya meli jukumu hilo na ziachia Serikali husika,”alisema Athuman akimnukuu mmiliki huyo.

  Mwananchi lilipotaka kufahamu hatua ambazo Serikali imezichukua kuwaokoa Watanzania hao, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsa Vuai Nahodha, alisema kwa taarifa alizonazo ni kwamba meli hiyo ilitekwa wakati ikiwa eneo la bahari kuu ambalo Jeshi la Wanchi wa Tanzania (JWTZ), ndio wanaohusika nalo na kwamba siyo polisi.

  “Kwa taarifa nilizonazo ni kuwa ile meli ilitekwa ikiwa kwenye bahari kuu, sasa huko wanaohusika ni JWTZ, sisi tunahusika na territory water (sehemu ya bahari iliyopo ndani ya miliki ya nchi),” alieleza Nahodha alipokuwa akizungumza na Mwananchi kwa simu.

  Kutokana na kauli hiyo Mwananchi ilimtafuta Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, ambaye alisema kuwa yeye hana utaratibu wa kuzungumza na waandishi wa habari kwenye simu. "..mimi huwa siyo utaratibu wangu kuzungumza kwenye simu na mwandishi, watafute maofisa wa jeshi watakusaidia..,"alisema Dk Mwinyi na kukata simu.

  Naye Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Generali Abdulrahaman Shimbo, hakuweza kutoa ufafanuzi wa suala hilo na badala yake aliahidi kulizungumzia wiki ijayo mbele ya vyombo vya habari.
   
 2. P

  Penguine JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Shimbo, Shimbo, Shimbo, Shimbooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo uko wapi Mtu wangu? hapo ndiyo panapotakiwa Kauli zako sasa. Au Hapo hapana Maslahi Mtaalam. Toa kauli, toa kauli, toa kauli Mnaadhimu mkuuuuuuuuuuuuu
   
 3. S

  Somi JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  viongozi wetu kila kukicha wanasafiri nje kuomba msaada wa ela kwa wazungu, kwanini wanasita kuomba msaada wa kijeshi kuokoa hawa watanzania? hawa pia si masilahi ya nchi?
   
Loading...