Watanzania waaswa kula nyama. Ulaji wa wafikia wastani wa Kilo 15 kwa mtu kwa mwaka

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
ULAJI wa nyama hapa nchini uko kwa kiwango cha chini ambapo sasa ulaji umefikia kilo 15 huku Shirika la Afya Duniani (WHO) likitaja mtu wa kawaida anatakiwa kula angalau kilo 50 kwa mwaka.

Akizungumza jana kwenye paredi ya mifugo kwenye maonesho ya mifugo na wakulima maarufu Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo, Profesa Elisante ole Gabriel alisema kwa mujibu wa WHO kwa Tanzania bado ulaji si mzuri ambapo takwimu zinaonesha mwaka 2017/ 18 ulaji wa nyama ulikuwa kilo 10 kwa mwaka.

"Angalau sasa tumefikisha kilo 15 kwa mwaka, bado tuko chini sana. Watanzania wajitahidi kula nyama ambayo ni sahihi," alisema.

Pia alisema sasa unywaji wa maziwa umefikia lita 200 kwa mwaka, lakini mwaka 2018/19 unywaji wa maziwa ulikuwa lita 54 kwa mwaka.

"Wakati Rais John Magufuli akiingia madarakani wizara ilikuwa ikichangia Sh bilioni 14 lakini imeongezeka hadi kufikia Sh bilioni 44.5, sawa na ongezeko la asilimia zaidi ya 200,”alisema.

Pia mifugo imeongezeka sasa kuna ng'ombe milioni 33, mbuzi milioni 23, kondoo zaidi ya milioni sita, kuku milioni 83 na kuku mayai yamefika bilioni nne.

"Mayai peke yake ni bilioni 800 hii ni jambo kubwa sana, lazima juhudi ziongezwe," alisema

Kwa upande wake, mgeni rasmi katika maonesho hayo ambaye ni Kaimu Mkuu wa mkoa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda alisema sekta ya mifugo ikisimamiwa vizuri itachangia fedha za kutosha katika pato la taifa.

Alisema kwa wilaya ya Bahi asilimia 80 ya makusanyo ya ndani yanatokana na mifugo.

Angelina Lutambi Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida alisema maonesho hayo yamekuwa ni elimu kwa wananchi na watendaji wa ngazi mbalimbali za serikali na yamekuwa njia nzuri ya kujifunza.

Mkoa wa Singida uchumi wake unategemea kilimo na sekta ya mifuko ikiwa na idadi ya mifugo zaidi ya milioni 1.3.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga alisema wataendelea kuhamasisha ufugaji wenye tija.
 
Ili uwe na afya iliyo bora kula nyama kidogo

Mtangazaji: kwann wewe Van damme umezeeka na una mwili mzuri

Van damme: Sababu kubwa sipendelei kula nyama ninafuata miiko ya afya naweza kula nyama mara moja kwa mwezi
 
Hii sasa ni promotion ya biashara, kwenye nyama kuna nini exactly ambacho hakipatikani kwenye vyanzo vingine hadi hao WHO watuwekee 50kg kwa mwaka?
 
Sheria ya takwimu inatutaka tuziamini takwimu za serikali. Lakini, mayai bilioni 800 kwa watanzania milioni 56 ni sawa na mayai 14286 kwa kila mtu kwa mwaka, sawa na mayai 40 kwa siku! Wastani wa ulaji huu utapungua kama wizara itakuja na takwimu za mayai yanayo uzwa nje ya nchi. Kinyume na hapo, ni takwimu za mikakati.
 
Mchagueni Mzee Rungwe, Mgombea pekee aliyeona swala la lishe duni kwa Watanzania kama changamoto muhimu... Lishe duni huleta akili duni, Afya dumavu, shahawa zisizo na afya, miili iliyo dhohofu nk..

Sasa kwa mwaka mtanzania anakula 15Kg za nyama? hii ni hatari kabisa yaani..
At least kwa mwaka mtu mmoja ng'ombe wawili... samaki kontena nk..
 
Nadhani kuna haja ya kukaa na kuwa na mifumo yetu ya ulaji kama nchi,hasa wizara inayohusika na lishe

Nyama kitaalamu wanasema hutakiwi kizidisha robo kilo kwa wiki kwa mtu mmoja,kwa maana hiyo kwa mwezi unatakiwa kula kilo 1 tu,ambayo ukizidisha kwa miezi 12 ni kwamba hutakiwi kuzidisha kg 12 kwa mwaka kwa mtu mmoja,sasa hawa wanatumbia kg 50.

Maziwa yana cholesterol pia na hutakiwi kunywa mengi lakini ndio tupo Lita 200 ambazo bado ni tunaambiwa chache

Wizara ingeweka vyakula vya taifa na utaratibu wake kutokana na mazingira yetu,hata mambo ya wazungu tuwaachie wao.
 
Sasa nachanganywa juzi daktari kaniambia nipunguze nyama nyekundu…..huku naambiwa nile nyama za kutosha.
 
Back
Top Bottom