Watanzania, ujumbe wenu kwa atawala umefika, lakini 'ili kenge asikie mpaka damu zimtoke masikioni'

RockCarnegie

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
963
1,927
Habari ndiyo hiyo!

Baada ya miaka minne ya utawala wa kujigamba wa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), hatimaye wananchi wametuma ujumbe kwa serikali na CCM kuwa Watanzania siyo 'wajinga sana'.

Mijini na vijijini wananchi wamegoma kujiandisha ili washiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Wananchi wameona kama watawala wanajiapiza kufutilia mbali vyama vya upinzani ili kibaki CCM peke yake, kwa nini wakapoteze muda kujiandisha wakati viongozi watakaowachagua hatatangazwa?

Wananchi wametambua dharau ya viongozi wa CCM na serikali ya kutoheshimu na kuthamini kura za wananchi.

Ni matusi makubwa kwa wananchi kuwatangazia kuwa baada kupiga kura wataotangazwa ni CCM na si vinginevyo.

'Watanzania siyo wajinga sana', tunasubiri wakati wa kupiga kura kama watawala watawalazimisha wananchi kwenda kupiga kura kama wanavyofanya kwenye uandikishaji.

Pamoja na wananchi kufikisha ujumbe kwa watawala na CCM, wakumbuke kuna msemo wa Kisukuma usemao 'kenge hasikii mpaka damu zimtoke masikioni'

Huu ni mwazo tu, nina mashaka, kuna uwezekano mkubwa kama watawala wameelewa wananchi wanataka nini maana kumiliki madaraka ya kulevya afadhali ya kenge kutokusikia.
 
Mleta mada sema ukweli, mbona kama unatarajia taarifa fulani mbaya hivi!.
 
Nchi yetu ilikabidhiwa ikajengwa kwenye misingi ya utu na undugu wa umoja.Amwagaae damu na kuondoa amani yetu atasambaratika yeye na kizazi chake,lkn tza itasimama
 
Habari ndiyo hiyo!

Baada ya miaka minne ya utawala wa kujigamba wa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), hatimaye wananchi wametuma ujumbe kwa serikali na CCM kuwa Watanzania siyo 'wajinga sana'.

Mijini na vijijini wananchi wamegoma kujiandisha ili washiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Wananchi wameona kama watawala wanajiapiza kufutilia mbali vyama vya upinzani ili kibaki CCM peke yake, kwa nini wakapoteze muda kujiandisha wakati viongozi watakaowachagua hatatangazwa?

Wananchi wametambua dharau ya viongozi wa CCM na serikali ya kutoheshimu na kuthamini kura za wananchi.

Ni matusi makubwa kwa wananchi kuwatangazia kuwa baada kupiga kura wataotangazwa ni CCM na si vinginevyo.

'Watanzania siyo wajinga sana', tunasubiri wakati wa kupiga kura kama watawala watawalazimisha wananchi kwenda kupiga kura kama wanavyofanya kwenye uandikishaji.

Pamoja na wananchi kufikisha ujumbe kwa watawala na CCM, wakumbuke kuna msemo wa Kisukuma usemao 'kenge hasikii mpaka damu zimtoke masikioni'

Huu ni mwazo tu, nina mashaka, kuna uwezekano mkubwa kama watawala wameelewa wananchi wanataka nini maana kumiliki madaraka ya kulevya afadhali ya kenge kutokusikia.
Kama umejiandikisha hata usipopiga kura utapigiwa na itatajwa kama kura halali za waliojiandikisha hivyo ushaliwa mzee!
 
Back
Top Bottom