Wito kwa watanzania wote: Ili CCM na serikali zake wajue hatuwataki, 2025 wote tususie uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,877
20,730
Ni miaka 63 sasa CCM ipo madarakani. Kimsingi hakuna maendeleo ya maana waliyotuletea, isipokuwa kuturudisha nyuma kimaendeleo miongo kadhaa.

Kila serikali iliyoingia madarakani ilileta usanii wa kisiasa na kiuchumi na hatimaye kuturudisha nyuma decades.Wanayojisifia kwamba ni maendeleo si lolote kabisa ukilinganisha na rasilimali nyingi tulizo nazo. Tuamke Watanzania.

Comrade Magufuli katika awamu yake moja alijitahitahidi kubadilisha taswira ya Tanzania kwa kutuletea maendeleo kiasi fulani, lakini juhudi zake na kiuhalisia na za kwetu pia,zilifishwa prematurely, inasikitisha sana.

Kwa jinsi hali ya kisiasa ilivyo nchini mwetu, hatuna jinsi yeyote ambayo kama Watanzania tunaweza kujinasua kwenye mkwamo wa kimaendeleo na kisiasa tulio nao sasa.Katiba haiheshimiwi kabisa na sioni uwezekano wa Bunge au hata wana siasa kutusaidia.

Mwito wangu kama Mtanzania kwa Watanzania wenzangu ni huu, kama mpaka 2025 tusipokuwa na Katiba mpya, wala Tume Huru ya Uchaguzi, siku ya uchaguzi wote tubaki nyumbani tusiende kupiga kura.Naamini hii ndiyo lugha tu CCM watakayoelewa.Sisi wananchi ndio tunaowapa wanasiasa legitimacy ya kutawala.Sasa kama wasipotupa Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi tubaki nyumbani,simply tuwanyime legitimacy ya kututawala.It is now or never, naomba tushirikiane wote.

NB: Please share this message widely.
 
Ni miaka 63 sasa CCM ipo madarakani.Kimsingi hakuna maendeleo ya msingi waliyotuletea,isipokuwa kuturudisha nyuma kimaendeleo.
Kila serikali iliyoingia madarakani ilileta usanii wa kisiasa na kiuchumi na hatimaye kuturudisha nyuma decades.Wanayojisifia kwamba ni maendeleo si lolote kabisa ukilinganisha na rasilimali nyingi tulizo nazo.Tuamke Watanzania.

Comrade Magufuli katika awamu yake moja alijitahitahidi kubadilisha taswira ya Tanzania kwa kutuletea maendeleo,lakini juhudi zake zilifishwa prematurely,inasikitisha sana.

Kwa jinsi hali ilivyo ya kisiasa nchini mwetu
,hatuna jinsi yeyote ambayo kama Watanzania tunaweza kujinasua kwenye mkwamo tulio nao sasa.Katiba haiheshimiwi kabisa na sioni uwezekano wa Bunge au hata wana siasa kutusaidia.

Mwito wangu kama Mtanzania ni huu,kama mpaka 2025 tusipokuwa na Katiba mpya, wala Tume Huru ya Uchaguzi,siku ya uchaguzi wote tubaki nyumbani.Sisi wananchi ndio tunaowapa wanasiasa legitimacy ya kutawala,kama wasipotupa Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi tubaki nyumbani,simply tuwanyime legitimacy ya kututawala.It is now or never,tushirikiane wote.
Naam
Hoja imeungwa mkono.

Wanaokubali waseme ndiyoooo
Wasioafiki waseme hapanaa
 
Me huwa siwaelewagi mnaolilia tume huru ya uchaguz et sijui katiba mpya, hivi unahisi hayo yatabadilisha nini ikiwa watu ni wale wale?

Hiyo tume huru ya uchaguzi watashindwa nini kuihonga hela ili watoe matokeo wanayoyataka?

Jirani zetu Kenya hapo uchaguzi wao uliopita ulisimamiwa na tume huru, je wamepata walichotegemea?

Sijui katiba mpya, je yaliyopo kwenye katiba ya sasa yanasimamiwa?

Ishu ni viongozi hawana uchungu na watanzania na ni wabinafsi na issue sio katiba mpya wala tume huru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hasusii mtu uchaguzi ujao,

Tutahakikisha haufanyiki uchaguzi wowote bila kupata Tume HURU ya UCHAGUZI Kwa kubadili vipengele muhimu vya Katiba iliyopo, na baadae tukamulishe KATIBA mpya.
Uchaguzi utafanyika vizuri tu wala usijitie presha huna unaloweza kufanya kuzuia uchaguzi.
 
Hasusii mtu uchaguzi ujao,

Tutahakikisha haufanyiki uchaguzi wowote bila kupata Tume HURU ya UCHAGUZI Kwa kubadili vipengele muhimu vya Katiba iliyopo, na baadae tukamulishe KATIBA mpya.
Mimi nimesema lazima iwepo Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi,bila vitu hivyo viwili tusiende kwenye Uchaguzi,ni kupoteza muda.Infact it is stupid,unafanyaje kitu huku ukijua fika hakina faida.
 
Tunaitaka CCM ila hatuwataki nanihii anayetokea upande ile na nanihii wa kule ambaye nywele zake zimepingua hapa na yule mwenye tai na yule wa goli la nanihii.
 
Mimi naamini ote wanaosoma mada za humu, hakuna hata mmoja mwenye muda wa kwenda kukaa foleni na kusubili kupiga kura. Hata lucas mwashamba hana muda huo..anaongeaga tu humu.
Wanaopiga kura wapo huko vijijini na wengine tangu wazaliwe hata kupata chakula kwa wasiwasi, lakini ndio wapigakura namba moja.
sijui utatumia njiagani kuwashawishi hadi wakuelewe kwa hicho unachosema.
 
Mimi nimesema lazima iwepo Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi,bila vitu hivyo viwili tusiende kwenye Uchaguzi,ni kupoteza muda.Infact it is stupid,unafanyaje kitu huku ukijua fika hakina faida.
Ondoa mawazo ya kike ya KUSUSA kwenye mada Yako!!

HOJA iwe, Bila tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya hautafanyika uchaguzi wowote.

Issue hapo ni kuwa Serikali ihakikishe inatoa ushirikiano Ili uchaguzi ufanyike.

La wajipange.
 
Hapa umeonesha mahaba ya mtu ni vyema ungeenda kwenye Agenda yako kuu.
Sina agenda na mtu yeyote,labda umuweke wewe.Mimi huwa najali issues sio mtu.Samia ameshindwa kazi aliyopewa,wananchi lazima tuonyeshe kwamba we want change,we want a more competent President.Na kwa kuwa hakuna abayeweza kutusaidia,tuonyeshe kutokuridhishwa nae kwa kukaa nyumbani siku ya uchaguzi bila Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.
 
Mtaishia kugongwa virungu na police muishie kuwa walemavu halafu mje na kauli ya Mungu atatulipia.

Ukishajitambua kwenye maisha pigania maendeleo ya familia yako hayo mengine unayoona hayawezekani yaache yakupite tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom