Watanzania tuwaheshimu viongozi wetu tafadhali

Watanzania tuwaheshimu viongozi wetu tafadhali

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
8,873
Reaction score
1,926
Wadau wote habari za Jumapili.
Nimeona nilete hili ombi hapa jamvini kwa kuwa sisi kama Watanzania na wasomi hata kama tuna makanjanja hapa wanautumia vibaya mtandao bado wanayo haki ya kuwepo.Kwa muda sasa nimeona michango iliyo jaa kashfa an kejeli kwa viongozi wetu .Kuanzia wa Chama tawala hadi wa Upinzani.They are all holding Public Office nadhani katika kuwakosoa tujenge hoja zaidi badala kutupa maneno machafu .Kuwa wehu katika hao viongozi hufanya mambo ya kijinga wakitaka ama kusifiwa ama chuki na kuliharibu taifa letu na hao ndiyo tukabaliane nao kwa kila hali .

Nimeona Kigwangala kwa mfano alijivua hata Utanzania kwamba tuna heshimiana wakubwa kwa wadogo akamtukana Ndugu Freeman Mbowe Bungeni .Leo anakuja jukwaani mmeonyesha hasira zenu na kuwa hamkuridhika na ujinga wake tena akiwa kiongozi .Watu wa namna lazima tuwakate kwa nguvu zetu zote na kuwakana .

Wakati wa State of Union kule USA kuna kiongozi toka Repulc alimtukana Rais akiwa anatoa hotuba tuliona Republican they reacted haraka na kumtaka amuombe Rais radhi maana ni Rais wa Taifa la America.

JK ni rais ana mapugufu yake lakini tukimpinga kwa kumpa heshima atajielewa zaidi kuliko kumjadili kwa kejeli .JF tunaweza kujenga hoja na yeye anajua let alone wajinga wachache ambao wamekuwa wana tabia ya kua attack personalities .

Leo mnaona Ndugu Slaa anapewa heshima kubwa Nchini Marekani si kwao lakini anakubalika kama mnavyo ona , sioni kwa nini hata sisi tusimpe heshima yake maana anajiheshimu .NI kiongozi wa Kitaifa .Kwa nini tusiwe na siasa za hoja kutofautiana kwa hoja na kubakia kuheshimiana kama Watanzania ? Najua ni viongozi wa CCM nasema hivyo kwa kuwa mara nyingi wamekuwa na kashfa kwa wapinzania kama si watanzania .Wajifunze sana kufanya siasa za ustaarabu hujui Nchi kesho itakuwa mkononi kwa nani .

Namaliza kwa kumpongeza JK .Mimi si mwana CCM kabisa , lakini katika hotuba yake ilikuwa nakasoro lakini kubwa moja maoni yake na maamuzi yake juu ya Katiba naamini yamempa heshima kama kiongozi wa Nchi kaonyesha mfano na wengine wafuate kwa manufaa ya watanzania .Tuwaheshimu viongozi wetu tafadhali .

Ni maoni yangu tu nimeona niseme mbele yenu .
Asanteni
 
Namaliza kwa kumpongeza JK .Mimi si mwana CCM kabisa , lakini katika hotuba yake ilikuwa nakasoro lakini kubwa moja maoni yake na maamuzi yake juu ya Katiba naamini yamempa heshima kama kiongozi wa Nchi kaonyesha mfano na wengine wafuate kwa manufaa ya watanzania .Tuwaheshimu viongozi wetu tafadhali .

Ni maoni yangu tu nimeona niseme mbele yenu .
Asanteni
Ni kweli, viongozi wanastahili heshima. Lakini nao wajiheshimu. Rais alipotoka aliposema Lissu ni mnafiki na mzandiki. Hakuwa na haja ya kuyasema hayo.
 
mtu kama pinda anafaa kueshimiwa kweli na kauli yake ya kumrisha polisi wawapige wananchi kiongozi kama yeye anasema kauli hii kweli
 
Kiongozi yeyote yule atakayejiheshimu,atakayeheshimu katiba ya nchi na kuheshimu wale waliomfikisha hapo alipo,kwa nini asiheshimiwe?

Lakini tabu inakuja hawa viongozi wanaovunja katiba ya nchi kwa makusudi na kusema 'WAPIGWE TU',wanaonyang'anya ardhi yetu kwa nguvu na kuwapa wageni,wanaolinda wahalifu kwa kigezo cha uswahiba kwa nini wapewe heshima?Hiyo itakuwa sio heshima ni woga!!!
Haiwezekani mtu aamuru upigwe kama utaandamana ambayo ni haki ya kikatiba halafu mtu huyo eti umuheshimu!!!

Kwangu mimi ukifanya YA HOVYO,nakupa YA HOVYO pia!Ukimwaga Mboga namwaga Ugali!!
 
Ni kweli, viongozi
wanastahili heshima. Lakini nao wajiheshimu. Rais alipotoka aliposema
Lissu ni mnafiki na mzandiki. Hakuwa na haja ya kuyasema hayo.

hivi kuna maneno ya ziada ya kumuita Lisu zaidi ya muongo, mnafiki na mzandiki?
 
eti kiongozi anadhurura na kimada kwenye nchi za watu na anaendelea kuwa mzinifu halafu tumheshimu! sidhani kama huku Marekani wanajua kuwa huyu jamaa alipora mke wa mtu. wangejua hilo wasingempokea na kushirikiana naye
 
Nakufananisha na msaidizi wetu wa kazi za ndani,ananionea wivu mimi bosi wake,haishi mitego na visa
 
Mkuu nakubaliana na wewe lakini ukweli ni kwamba viongozi wetu wanatakiwa kwanza wawe na heshima na ndio waheshimiwe.
Mimi mwenyewe siwezi kumheshim mtu yeyote ambaye yeye mwenyewe hajieshimu.sasa nitamheshimu kwa lipi wakati yeye mwenyewe kauli zake na mazungumzo yake yanapotosha?
 
eti kiongozi anadhurura na kimada kwenye nchi za watu na anaendelea kuwa mzinifu halafu tumheshimu! sidhani kama huku Marekani wanajua kuwa huyu jamaa alipora mke wa mtu. wangejua hilo wasingempokea na kushirikiana naye

Lizaboni huu ujinga wako na uongo hauna nafasi na unaweza kuacha kuandika kama akili zako hazina akili kiasi hiki .You busted bastard,
 
Lizaboni huu ujinga wako na uongo hauna nafasi na unaweza kuacha kuandika kama akili zako hazina akili kiasi hiki .You busted bastard,

ndio watu wenyewe unaodai waheshimiwe kaka na huyu Lizaboni ni mmoja wa hao viongozi wenyewe hapa amekuja amevaa gunia usoni ili haweze kutukana vizuri. tuna safari ndefu ndefu Thanks for Trying anyway.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom