Uchaguzi 2020 Watanzania tusiwe wepesi wa kusahau. Hakuna Mbunge wa CCM anaenda Bungeni kuwakilisha Wananchi

HOJA YAKO NAWEZA SEMA NI BORA KABISA KWA SIKU YA LEO HONGERA KWA KUONA MBALI, HAWA JAMAA WA CCM SIO KABISA MUDA WOTE WANAANGALIA MASLAHI YAO TU NA SIO YA WANANCHI WALIOWACHAGUA.
Neno lako la mwisho limeharibu sentence yako
 
Tukiwa tunajiandaa kuchagua viongozi wetu wa kutuwakilisha bungeni awamu ijayo, tunatakiwa kutafakari baadhi ya matukio yaliyotokea Bunge la awamu inayomaliza muda wake.

Huu ndyo muda wetu sisi kama wawakilishwaji kuamua ni nani anafaa kutuwakilisha bungeni. Na huu ndiyo muda sahihi kuwawajibisha wale wote walioshindwa kutuwakilisha ipasavyo.

Watanzania wenzangu, tusiwe wepesi kusahau kama kuku wa kienyeji. Bunge lililopita tuseme tu na ukweli, wabunge wa CCM wote waliishia kuiwakilisha serikali na sio sisi tuliiwatuma uko wakaisimamie serikali na kuwakilisha matatizo yetu.

Ni wabunge wachache sana waliojaribu kuwakilisha matatizo yetu kama wakina Bashe ila baada ya wao kupewa vyeo nao wakafyata mkia.

Tusiwe wepesi kusahau kuwa wabunge hawa hawa wa CCM walikubali hoja ya bunge lisiwe live huku wananchi tuliowachagua tukakosa haki yetu ya kujua tunawakilishwaje na wabunge tuliowachagua. Tena hapa anayetakiwa kuwajibishwa akiwa wa kwanza kabisa ni Nape mbunge wa jimbo la Mtama maana ndye aliyeweka bunge gizani.

Hawa hawa wabunge wameshindwa hata kutetea maslai ya Watumishi/Wafanyakazi huku wakijali posho na viinua mgongo vyao tu.

Report za CAG Assad, miaka miwili mfululizo zimekuja na madudu chungu nzima hasa ya upotevu wa matrilion ila hakuna hata mbunge mmoja wa CCM aliyefungua kinywa chake kuhoji serikali juu ya izo pesa.

Budget iliyokuwa ikipitishwa kwa mbwembwe na Wabunge wa CCM huku wakitukana Wapinzani nazo zilikuwa budget hewa. Utekelezaki hata 50% ilikuwa haifiki.

Mbali na hapo, Rais alikuwa anachukua pesa hazina bila kuidhinishwa na bunge kwa matumizi ambayo hayajaidhinishwa na bunge lakini wabunge wa CCM hawakuweza kufunua midomo yao na kuhoji zaidi ya kukenua na kusifia juhudi. Hapa ndyo wananchi tunajiuliza hivi Wabunge kazi yao ni nini uko mjengoni?

( ref: pesa zilizotumika kununua korosho. Je hasara au faida iliyopatikana bunge lilihoji, Vp na zile zilizonunua ndege kwa cash?).

Tusisahau kuwa ndyo hili bunge limekuja na visheria vipya vipya vya ajabu ambavyo hata vingine Rais John Pombe Magufuli alikataa kuzipitisha kama ile ya Kikokoto kipya cha mafao ya watumishi. Mbali ya hapo ndyo bunge hili hili liipitisha sheria ya kuwapa kinga viongozi wakuu wa mihimili ya serikali. ( hapa ndyo unajua wabunge wameenda kuwakilisha serikali na si wananchi)


Haya ni machache tu nikiendelea kuandika madudu na udhaifu wa wabunge wa ccm naweza andika hata kitabu kizima.
Kwa kifupi, Watanzania wenzangu tuwe makini sana na wabunge tunaochagua. Ninawakakikishieni mkirudia makosa yale yale, kabla ya 2024 katiba yetu itabadilishwa na Rais Magufuli kuongezewa muda kama sio kufanywa Rais wa Maisha.

Asilimia kubwa ya wabunge wa CCM wanachojali ni kujitengenezea mazingira ya kuendelea kukaa bungeni huku wakisahau nini wanatakiwa kufanya wanapochaguliwa na wananchi kuwa mjengoni.
ni mwananchi asiyejitambua na mwenye matatizo ya akili ndiye atakawachagua wabunge wa ccm
 
Kuna mikoa natamani tusingekuwa nchi moja. Mikoa kama Dodoma, Ruvuma, Rukwa, Geita na Njombe hii mikoa inakera sana haijawahi chagua mbunge mzalendo hata awamu moja wenyewe ni ccm tu
Tatizo kubwa la huko wapo nyuma kielimu.. ujinga ndo mtaji Mkuu wa ccm
 
Ndugai kadhibitisha ukweli wa hii post
Screenshot_20200830-103532_Twitter.jpg
 
Umesahau kusema kuwa wabunge wa upinzani hawaaminiki maana hawachelewi kuunga juhudi.

Ila wabunge wa vyama vyote, chama ndio kitu cha kwanza kabisa halafu nyie wananchi ndio mnafuatia.
 
Back
Top Bottom