Uchaguzi 2020 Watanzania tusiwe wepesi wa kusahau. Hakuna Mbunge wa CCM anaenda Bungeni kuwakilisha Wananchi

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,944
18,655
Tukiwa tunajiandaa kuchagua viongozi wetu wa kutuwakilisha bungeni awamu ijayo, tunatakiwa kutafakari baadhi ya matukio yaliyotokea Bunge la awamu inayomaliza muda wake.

Huu ndyo muda wetu sisi kama wawakilishwaji kuamua ni nani anafaa kutuwakilisha bungeni. Na huu ndiyo muda sahihi kuwawajibisha wale wote walioshindwa kutuwakilisha ipasavyo.

Watanzania wenzangu, tusiwe wepesi kusahau kama kuku wa kienyeji. Bunge lililopita tuseme tu na ukweli, wabunge wa CCM wote waliishia kuiwakilisha serikali na sio sisi tuliiwatuma uko wakaisimamie serikali na kuwakilisha matatizo yetu.

Ni wabunge wachache sana waliojaribu kuwakilisha matatizo yetu kama wakina Bashe ila baada ya wao kupewa vyeo nao wakafyata mkia.

Tusiwe wepesi kusahau kuwa wabunge hawa hawa wa CCM walikubali hoja ya bunge lisiwe live huku wananchi tuliowachagua tukakosa haki yetu ya kujua tunawakilishwaje na wabunge tuliowachagua. Tena hapa anayetakiwa kuwajibishwa akiwa wa kwanza kabisa ni Nape mbunge wa jimbo la Mtama maana ndye aliyeweka bunge gizani.

Hawa hawa wabunge wameshindwa hata kutetea maslai ya Watumishi/Wafanyakazi huku wakijali posho na viinua mgongo vyao tu.

Report za CAG Assad, miaka miwili mfululizo zimekuja na madudu chungu nzima hasa ya upotevu wa matrilion ila hakuna hata mbunge mmoja wa CCM aliyefungua kinywa chake kuhoji serikali juu ya izo pesa.

Budget iliyokuwa ikipitishwa kwa mbwembwe na Wabunge wa CCM huku wakitukana Wapinzani nazo zilikuwa budget hewa. Utekelezaki hata 50% ilikuwa haifiki.

Mbali na hapo, Rais alikuwa anachukua pesa hazina bila kuidhinishwa na bunge kwa matumizi ambayo hayajaidhinishwa na bunge lakini wabunge wa CCM hawakuweza kufunua midomo yao na kuhoji zaidi ya kukenua na kusifia juhudi. Hapa ndyo wananchi tunajiuliza hivi Wabunge kazi yao ni nini uko mjengoni?

( ref: pesa zilizotumika kununua korosho. Je hasara au faida iliyopatikana bunge lilihoji, Vp na zile zilizonunua ndege kwa cash?).

Tusisahau kuwa ndyo hili bunge limekuja na visheria vipya vipya vya ajabu ambavyo hata vingine Rais John Pombe Magufuli alikataa kuzipitisha kama ile ya Kikokoto kipya cha mafao ya watumishi. Mbali ya hapo ndyo bunge hili hili liipitisha sheria ya kuwapa kinga viongozi wakuu wa mihimili ya serikali. ( hapa ndyo unajua wabunge wameenda kuwakilisha serikali na si wananchi)

Haya ni machache tu nikiendelea kuandika madudu na udhaifu wa wabunge wa ccm naweza andika hata kitabu kizima.
Kwa kifupi, Watanzania wenzangu tuwe makini sana na wabunge tunaochagua. Ninawakakikishieni mkirudia makosa yale yale, kabla ya 2024 katiba yetu itabadilishwa na Rais Magufuli kuongezewa muda kama sio kufanywa Rais wa Maisha.

Asilimia kubwa ya wabunge wa CCM wanachojali ni kujitengenezea mazingira ya kuendelea kukaa bungeni huku wakisahau nini wanatakiwa kufanya wanapochaguliwa na wananchi kuwa mjengoni.
 
Ni wajibu wa wagombea wa Ubunge kutoka vyama vya upinzani 'halisi' wasisitize somo hili wakati wa kampeni zao.

Ni hasara kubwa sana kwa Taifa letu kuwa na wabunge wengi wa CCM ndani ya Bunge.
Miaka ya nyuma hata kama wabunge wangekuwa wa CCm tu ila wengi walijitahidi kutimiza wajibu wao wa kuisimamia serikali. Ila hawa wa leo ni kuhunga juhudi za mwenyekiti wao tu.
 
1598118296510.png
 
Na mwaka huu ccm ni wengi zaidi maana hawa wachadema ndio sijawaelewa kabisa

Maana wao kazi yao ilikuwa ni kutoka nje
 
Tukiwa tunajiandaa kuchagua viongozi wetu wa kutuwakilisha bungeni awamu ijayo, tunatakiwa kutafakari baadhi ya matukio yaliyotokea Bunge la awamu inayomaliza muda wake.

Huu ndyo muda wetu sisi kama wawakilishwaji kuamua ni nani anafaa kutuwakilisha bungeni. Na huu ndiyo muda sahihi kuwawajibisha wale wote walioshindwa kutuwakilisha ipasavyo.

Watanzania wenzangu, tusiwe wepesi kusahau kama kuku wa kienyeji. Bunge lililopita tuseme tu na ukweli, wabunge wa CCM wote waliishia kuiwakilisha serikali na sio sisi tuliiwatuma uko wakaisimamie serikali na kuwakilisha matatizo yetu.

Ni wabunge wachache sana waliojaribu kuwakilisha matatizo yetu kama wakina Bashe ila baada ya wao kupewa vyeo nao wakafyata mkia.

Tusiwe wepesi kusahau kuwa wabunge hawa hawa wa CCM walikubali hoja ya bunge lisiwe live huku wananchi tuliowachagua tukakosa haki yetu ya kujua tunawakilishwaje na wabunge tuliowachagua. Tena hapa anayetakiwa kuwajibishwa akiwa wa kwanza kabisa ni Nape mbunge wa jimbo la Mtama maana ndye aliyeweka bunge gizani.

Hawa hawa wabunge wameshindwa hata kutetea maslai ya Watumishi/Wafanyakazi huku wakijali posho na viinua mgongo vyao tu.

Report za CAG Assad, miaka miwili mfululizo zimekuja na madudu chungu nzima hasa ya upotevu wa matrilion ila hakuna hata mbunge mmoja wa CCM aliyefungua kinywa chake kuhoji serikali juu ya izo pesa.

Budget iliyokuwa ikipitishwa kwa mbwembwe na Wabunge wa CCM huku wakitukana Wapinzani nazo zilikuwa budget hewa. Utekelezaki hata 50% ilikuwa haifiki.

Mbali na hapo, Rais alikuwa anachukua pesa hazina bila kuidhinishwa na bunge kwa matumizi ambayo hayajaidhinishwa na bunge lakini wabunge wa CCM hawakuweza kufunua midomo yao na kuhoji zaidi ya kukenua na kusifia juhudi. Hapa ndyo wananchi tunajiuliza hivi Wabunge kazi yao ni nini uko mjengoni?

( ref: pesa zilizotumika kununua korosho. Je hasara au faida iliyopatikana bunge lilihoji, Vp na zile zilizonunua ndege kwa cash?).

Tusisahau kuwa ndyo hili bunge limekuja na visheria vipya vipya vya ajabu ambavyo hata vingine Rais John Pombe Magufuli alikataa kuzipitisha kama ile ya Kikokoto kipya cha mafao ya watumishi. Mbali ya hapo ndyo bunge hili hili liipitisha sheria ya kuwapa kinga viongozi wakuu wa mihimili ya serikali. ( hapa ndyo unajua wabunge wameenda kuwakilisha serikali na si wananchi)

Kwa kifupi, Watanzania wenzangu tuwe makini sana na wabunge tunaochagua. Ninawakakikishieni mkirudia makosa yale yale, kabla ya 2024 katiba yetu itabadilishwa na Rais Magufuli kuongezewa muda kama sio kufanywa Rais wa Maisha.

Asilimia kubwa ya wabunge wa CCM wanachojali ni kujitengenezea mazingira ya kuendelea kukaa bungeni huku wakisahau nini wanatakiwa kufanya wanapochaguliwa na wananchi kuwa mjengoni.
Umeandika kwa ureefu sana lakini haya uliyoyaandika ni maoni yako ambayo si kweli.

CCM inasimamia wabunge na viongozi wake ngazi mbalimbali kwa ukaribu sana. Hivi karibuni CCM imeboresha Katiba yake kwamba kada wa chama ambaye ana cheo ndani ya chama hawezi wakati huo huo kiwa kiongozi wa serikali ukiacha wale ambao wanaingia kwa nafasi zao kwenye kamati bila ya kuwa na nguvu za kimaamuzi.

Kama umefanya research ambayo imelenga kuinanga CCM ungejitahidi hata kinafiki kumulika upande wa pili ambao vitendo vyao vya wazi kabisa kuwa hawawakilishi majimbo yao bali matakwa ya viongozi wa vyama vyao.

Angalia issue ya COVID, Bajeti na hoja za msingi wamekuwa wakitoka bungeni kwa matakwa ya viongozi wao....

Mzee umetopola
 
Jielimishe kwanza kazi ya bunge na wajibu wa mbunge. Ukielewa soma tena ulichoandika.
 
Tukiwa tunajiandaa kuchagua viongozi wetu wa kutuwakilisha bungeni awamu ijayo, tunatakiwa kutafakari baadhi ya matukio yaliyotokea Bunge la awamu inayomaliza muda wake.

Huu ndyo muda wetu sisi kama wawakilishwaji kuamua ni nani anafaa kutuwakilisha bungeni. Na huu ndiyo muda sahihi kuwawajibisha wale wote walioshindwa kutuwakilisha ipasavyo.

Watanzania wenzangu, tusiwe wepesi kusahau kama kuku wa kienyeji. Bunge lililopita tuseme tu na ukweli, wabunge wa CCM wote waliishia kuiwakilisha serikali na sio sisi tuliiwatuma uko wakaisimamie serikali na kuwakilisha matatizo yetu.

Ni wabunge wachache sana waliojaribu kuwakilisha matatizo yetu kama wakina Bashe ila baada ya wao kupewa vyeo nao wakafyata mkia.

Tusiwe wepesi kusahau kuwa wabunge hawa hawa wa CCM walikubali hoja ya bunge lisiwe live huku wananchi tuliowachagua tukakosa haki yetu ya kujua tunawakilishwaje na wabunge tuliowachagua. Tena hapa anayetakiwa kuwajibishwa akiwa wa kwanza kabisa ni Nape mbunge wa jimbo la Mtama maana ndye aliyeweka bunge gizani.

Hawa hawa wabunge wameshindwa hata kutetea maslai ya Watumishi/Wafanyakazi huku wakijali posho na viinua mgongo vyao tu.

Report za CAG Assad, miaka miwili mfululizo zimekuja na madudu chungu nzima hasa ya upotevu wa matrilion ila hakuna hata mbunge mmoja wa CCM aliyefungua kinywa chake kuhoji serikali juu ya izo pesa.

Budget iliyokuwa ikipitishwa kwa mbwembwe na Wabunge wa CCM huku wakitukana Wapinzani nazo zilikuwa budget hewa. Utekelezaki hata 50% ilikuwa haifiki.

Mbali na hapo, Rais alikuwa anachukua pesa hazina bila kuidhinishwa na bunge kwa matumizi ambayo hayajaidhinishwa na bunge lakini wabunge wa CCM hawakuweza kufunua midomo yao na kuhoji zaidi ya kukenua na kusifia juhudi. Hapa ndyo wananchi tunajiuliza hivi Wabunge kazi yao ni nini uko mjengoni?

( ref: pesa zilizotumika kununua korosho. Je hasara au faida iliyopatikana bunge lilihoji, Vp na zile zilizonunua ndege kwa cash?).

Tusisahau kuwa ndyo hili bunge limekuja na visheria vipya vipya vya ajabu ambavyo hata vingine Rais John Pombe Magufuli alikataa kuzipitisha kama ile ya Kikokoto kipya cha mafao ya watumishi. Mbali ya hapo ndyo bunge hili hili liipitisha sheria ya kuwapa kinga viongozi wakuu wa mihimili ya serikali. ( hapa ndyo unajua wabunge wameenda kuwakilisha serikali na si wananchi)

Kwa kifupi, Watanzania wenzangu tuwe makini sana na wabunge tunaochagua. Ninawakakikishieni mkirudia makosa yale yale, kabla ya 2024 katiba yetu itabadilishwa na Rais Magufuli kuongezewa muda kama sio kufanywa Rais wa Maisha.

Asilimia kubwa ya wabunge wa CCM wanachojali ni kujitengenezea mazingira ya kuendelea kukaa bungeni huku wakisahau nini wanatakiwa kufanya wanapochaguliwa na wananchi kuwa mjengoni.
Kwa kweli Wabunge wa CCM naweza kusema walichokuwa wanakifanya kule Bungeni ni kuwashambulia Wapinzani wanapotoa hoja zenye mashiko kwa kuomba miongozo mara utasikia Taarifa mh Spika.
 
Kura yangu sipigii hao viumbe kuanzia diwan,mbunge,Rais zote nawapa chadema angalau tubadili ladha maisha magumu mmno tokea 2015
labda utabadili ladha kwenye karatasi.....kwenye kuapishwa ni walewale usiowataka
 
Back
Top Bottom