Watanzania tusiwe kama nyumbu kwa CHADEMA

Watanzania tusiwe kama nyumbu kwa CHADEMA

Mkuu BE nafikiri umekuwa hufuatilii habari nyingi duniani.

Hali imebadilika sasa na hao nyumbu unaowasema kwamba hufuata hatari basi siku hizi wamekuwa wana umoja mkubwa sana.

Ni hivi majuzi tu huko mbugani Cruger nchini Afrika Kusini, nyumbu waliamua kuwatolea uvivu simba kwa kumuua mwenzao na kuanza kumla mbele yao wao nyumbu.

Ni kwa sababu walikuwa wakitaka kunywa maji kutokana na kiu kubwa walokuwa nayo.

Watanzania wana kiu kuu na kiu hio inaweza kuondolewa kwa kupata fursa ya kwenda kunywa maji mtoni.

360_battle_kruger.jpg


Hapo mtoni hao mamba na simba ni lazima wajiandae kwa changamoto kutoka kwa nyumbu na si kungojelea vya bure kwa kutaka kuua nyumbu wakatavyo.
 
Haya tumekusikia bana,tutakua nyumbu kwa ccm waliokutuma
 
Yaani ni nyumbu kweli CDM hata wangefanya nini lakini ukweli upo pale pale hawawezi kuongoza nchi hii asilani kila mwenye akili anajua ghiriba zao!

Si wamezunguka na chopa nchi mzima angalieni matokeo yake mtayaona Kama wanakubalika na matunda yake tuangalie matokeo ya uchaguzi mdogo wa madiwani wa tarehe 9 February!

Chopa inapita siku siku Moja tu tena kwa masaa tu kilichobora ni kuimarisha mifumo yetu ya mashina, matawi na mabalozi hiyo ndio Siri kubwa ya ushindi!
 
Ukienda katika mbunga nyingi za wanyama hapa Tanzania utawakuta wanyama aiana ya Nyumbu, wanyama hawa wakati mwingine huitwa zero brain, yaani wanyama wasio na akili. Sababu inayowafanya waitwe hivyo ni uwezo wao wa kutunza kumbukumbu na waoga wao japo ni wapole sana. Wanyama hawa utawakuta kwa makundi mengi nafikiri ndiyo wanyama wengi katika mbuga zetu. Pamoja na wingi wao hauwasaidii kujilinda na maadui.

Katika mbuga ya Serengeti utawaona wakivuka mto Mara kuelekea upande wa pili wa mto, akipita nyumbu moja kati kati ya mto akakamatwa na kuliwa na mamba nyumbu waliobaki husahau na kuendelea kupita hapo hapo na kuliwa wenye bahati huvuka, lakini pia Nyumbu wakiona simba anawanyemelea huwa hawana uwezo wa kujihami, hata simba akiondoka nyumbu husahau mara moja kama Simba alitafuna mwenzao.

Watanzania tuna sifa kama za mnyama nyumbu. Kwa nini ninasema ni sawa na nyumbu; sifa alizonazo nyumbu ndiyo hizo tulizonazo Watanzania. Watanzania ni waoga sana katika Afrika Mashariki, Tanzania ndiyo nchi ambako nyumbu hupatikana kwa wingi kama walivyo Watanzania katika eneo hili.

Watanzania ni wepesi wa kusahau adui, hupenda kupita njia ile apitayo mnyama nyumbu hata kama kuna hatari. Utawaona Watanzania kwa makundi wakivuka mto mara hata kama baadhi wameliwa na mamba au simba. Simba na mamba huwawinda watanzania na kuwala, hulalamika sana kipindi hicho kuwa simba na mamba wamewashambulia na kuwaua lakini baada ya muda husahau kabisa kama simba na mamba aliwahi kuwadhuru na anaweza kurudia mchezo wa kuwatafuna.

Kwa usahaurifu huu wa Watanzania kwa nini tusiitwe zero brain kama wanyama wetu nyumbu ambao hawaoni hatari iliyo mbele yao? Wakati tukielekea katika uchaguzi wa mwaka huu hatuoni hatari zilizo mbele yetu, tumeshahau tulivyojeruhiwa na baadhi ya wagombea.

Nchi yetu ni masikini japo haistahili kuwa masikini, watu wameweka mapesa nje ya nchi, wamepiga dili kubwa mbalimbali wakituacha hoi bin taabani tukibeba zege la misamaha ya kodi za matajiri.

Kwa kipindi cha miaka 10 kashfa nyingi zilikuwa katika wizara nyeti ya nishati na madini, wizara hii ndiyo imekuwa mto Mara, watanzania tumeliwa ndani ya mto huu ukiacha Simba BoT.

Watanzania sasa utawambia nini kuhusu simba hawa wanaotaka kuwa viongozi wetu, kama waliweza kututafuna wakiwa watoto je sasa wakiwa wakubwa itakuwaje, mfano kuna watoto walibeba pesa kwenye viroba kutoka pale benki ya STANBIC lakini mpaka sasa mifumo ya usalama ya nchi imepata kiharusi kuwakamata au kuwatambua.

Kuna walio nunua mitambo mibovu kwa pesa nyingi , sasa wanatundanganya eti tuvuke mto mamba hawali nyama ya nyumbgu tena, wanakula majani tu. Kwa kuwa watanzania ni zero brain tunaelekea kuamini kuwa mamba wamecha kula nyama sasa wanakula majani.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake!.
 
Mtoa Mada msomi sana ameandika vitu ki usomi halafu nyinyi mnakuja na majibu ya kubabiababia tu.

Cammon guys jibu hoja hacheni majibu ya siyo na kichwa wala miguu.

Weel done mtoa hoja keep it up
 
Pole sana mtanzania pekee mwenye akili ya nyumbu....!!


​
na british economist,
nyumbu ni wanyama wa ajabu, nadhani ni wanyama walio na akili ndogo kuliko wanyama wote wa porini. Wanyama hao wakishaamua kufanya kitu watakifanya tu bila kujali ni madhara gani yatatokana na uamuzi wao.

mfano nyumbu wanaweza kuwa na kiu wakaamua kwenda kunywa maji kwenye mto uliojaa mamba. Kwa wingi wao watafika mtoni na kuanza kunywa maji huku mamba wenye njaa kali wakijikamatia nyumbu mmoja mmoja wakizamisha majini na kujitafunia. Nyumbu waliobaki wataendelea kunywa maji bila kujali yanayowakuta wenzao, wakimaliza kunywa maji wanaondoka zao, lakini wakisikia kiu tena wanarudi palepale bila kukumbuka kuwa kuna wenzao waliotafunwa, na wanaendelea kutafunwa wengine!

Au wakati mwingine nyumbu wanaweza wakaamua kuvuka mto wenye kina kirefu, kwa kuutegemea wingi wao, wataingia kwenye mto ambapo karibu nusu yao watabaki maiti katika mto huo wenye kina kirefu huku wengine wakifanikiwa kuvuka.

Daima hayo ndiyo maisha ya nyumbu, kukilenga ili wakitimize kile wanachokiangalia kwa wakati huo bila kujali madhara ya baadaye.

Tofauti na nyumbu binadamu tumejaliwa akili, pamoja na matatizo na shida tunavyoweza kuwa navyo, katika kuvikabili ni lazima tupime madhara na faida ya kufanya hivyo. Kama madhara yanazidi faida tunaona bora tuache. Ni heri mtu kubaki na shida au matatizo kuliko kutoa uhai kwa tamaa ya kutaka kumaliza matatizo au shida.

Kwa nini nasema hivyo? Kwa sasa kuna mageuzi ya kisiasa, hasa katika nchi nyingi za kiafrika, ambapo vyama vikongwe vya siasa, hasa vilivyopigania uhuru wa nchi vinazozitawala na kuupata toka kwa wakoloni, vinapata shinikizo toka kwa vyama vya upinzani la kuvitaka vyama hivyo vikongwe vikae pembeni na kuviachia vyama vipya vya upinzani kutawala.

Shinikizo hilo limefanikiwa katika baadhi ya nchi, ambapo vyama vya upinzani vimeviondoa madarakani vyama vikongwe. Lakini hatahivyo baada ya kuchukua madaraka, vyama vilivyokuwa vya upinzani, vimeshindwa kuionyesha neema viliyokuwa vikiimba kabla ya kuingia madarakani. Na badala yake vinafanya vibaya zaidi kuliko hata vyama vikongwe vinavyoondolewa madarakani.

Kabla sijaendelea naomba nieleweke. Sio kwamba naikataa demokrasia, mimi ni mpenzi mkubwa wa demokrasia, ila ninachokikataa ni demokrasia hiyo kutugeuza nyumbu ambaye kiu ya maji inamsahaulisha kuwa ndani ya mto kuna mamba, hivyo badala ya nyumbu kumaliza kiu yake akaishia kuumaliza uhai wake.

Ninachokitaka na kukiomba kwa mungu ni demokrasia kwa maana halisi, demokrasia itakayotufanya tuyapate mabadiliko tutakayoyataka na kutuacha salama. Nadhani hiyo ina tofauti na mageuzi yanayoimbwa na walio wengi.

Sababu mabadiliko na mageuzi ni vitu viwili vinavyotofautiana, mabadiliko yanakuja taratibu kwa wanaoyataka kupata muda wa kuyatafakari ili wakayapate yaliyo mema. Lakini mageuzi hayatoi muda wa kutafakari.

Jambo la kusikitisha ni kwamba hapa nchini kwetu kuna kila dalili ya kutokea mageuzi. Watu hawaonekani kutafakari kuhusu kitu wanachokitaka kinachoweza kuwa mbadala wa kile walichokichoka. Wao wanachokitaka ni kukiona cha zamani kinaondoka na kuja kingine bila kujali kinachokuja kimekaaje, ilimradi tu yawepo mageuzi.

Mfano kuna chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), chama hicho kinaonekana kupata ushabiki wa kisiasa kwa kasi sana. Naamini kabisa kwamba wananchi wametokea kukishabikia chama hicho bila kupata muda wa kutafakari kwanza. Wao wanachokiangalia ni mageuzi lakini hawajali mageuzi hayo yana nini ndani yake.

Hebu tukakiangalie hicho chama. Chadema kinaundwa na idadi kubwa ya vijana. Na kawaida ya vijana walio wengi hupendelea mageuzi badala ya mabadiliko, yaani kitu tunachoweza kukiita bandika bandua, hapo tuelewe hakuna muda wa kutafakari. Vijana mara nyingi hawana muda wa kuyapima mema na mabaya yaliyomo katika mageuzi wanayoyatamani na kisha kuyalinganisha.

Mfano wa hivi karibuni ni wa tukio lililotokea kwenye mkutano wa kanda wa chadema kule arusha. Kutokana na sababu ambazo haziko wazi, kundi la vijana waliomchoka mwenyekiti wa chama hicho mkoani arusha, samson mwigamba, likiongozwa na mbunge wa arusha mjini,godbles lema, liliuvamia mkutano huo wa kanda kwa mtindo wa shambulizi la kigaidi na kuanza kumchapa ngumi mwenyekiti huyo wa mkoa bila kuheshimu wala kufuata kanuni yoyote ya mkutano uliokuwa ukiendelea.

Kilichodaiwa ni kwamba eti mwigamba aliandika mambo fulani kwenye mtandao wa kijamii. Kwahiyo vijana hao wakadai kwamba mwigamba afukuzwe kwenye nafasi zake zote alizokuwa akizishikilia kwenye chama hicho. Wala mwigamba hakupewa kwanza nafasi ya kujitetea kufuatia uvamizi huo wa kigaidi. Kwahiyo demokrasia iko wapi? Kilichoangaliwa pale ni mageuzi na sio demokrasia.

Nikirudi upande wa pili, tutaona kwamba mwigamba ni mtu anayeipenda chadema kuliko watu wengi walio wanachama wa chama hicho.

Naweza kusema kwamba bila yeye, mwigamba, si ajabu lema asingejuwa mbunge kwa wakati huu. Lakini inaonekana lema anauangalia ubunge kuliko anavyokijali chama, pengine ndiyo maana akaongoza uvamizi huo ili kumchafulia mwigamba kwa hofu ya kwamba pengine mwigamba anaweza akautamani ubunge katika uchaguzi ujao na hivyo kumnyang’anya lema kitumbua mdomoni.

Katika hatua nyingine ni kwamba yaleyale yaliyodaiwa na lema kwamba mwigamba aliyafanya kiusaliti, kuandika kwenye mtandao wa kijamii kukikosoa chama chake, naye lema kayatumia vilevile kuwashambulia viongozi wa chama chake!

Lema kautumia mtandao wa kijamii kumshambulia naibu katibu mkuu wa chadema, kabwe zubeir zitto maarufu kama zitto kabwe, akidai kwamba ni mtu mnafiki.

Hebu fikiria mtu aliyemshambulia mwenzake kuwa katenda kosa fulani analitumia kosa lilelile kuwashambulia wenzake kwa mtindo uleule, akiliona kosa hilo kuwa ni halali kwake!

Lakini hatahivyo tukiziangalia tuhuma zilizotolewa na lema dhidi ya naibu katibu mkuu wa chama chake pia tutagundua kitu kingine. Ni kwamba zitto kabwe muda wote amekuwa akijipambanua kama mzalendo wa kweli wan chi hii, mtu aliye na uchungu na nchi pamoja na watu wake. Mpaka zitto akafikia hata kuzikataa posho za vikao vya bunge, wananchi wakamuona mzalendo kwa hilo.

Lakini kumbe mtu anayekataa kupokea shilingi 70,000/= kama posho ya kikao cha bunge anapokea kati ya shilingi 700,000/= na 1,000,000/= kama posho ya kikao cha kamati ya bunge anayoisimamia! Hivi kweli kuna uzalendo hapo? Huyu ni mzalendo au anayewageuza wazalendo kuwa matuyuyu?

Hayo niliyoyataja ni baadhi ya mambo machache yanayoonyesha mwenendo wa chama kinachotamaniwa na baadhi ya wananchi kuwa mbadala wa chama tawala. Hiyo ina tofauti gani na nyumbu wenye kiu kwenda kunywa maji kwenye mto uliojaa mamba?

Sababu yanayojitokeza kwenye chama hicho kikuu cha upinzani yanaonekana madogo kwa vile chama hicho hakijapewa ridhaa ya kuvisimamia vyombo vya dola, lakini pindi wananchi wakikipa ridhaa hiyo sitaona ajabu yakitokea hapa nchini kwetu kama yale ya renamo kule msumbiji, unita kule angola, m 23 kule congo nakadhalika. Maana hayo yote ni matokeo ya uasi katika uendeshaji wa nchi, ambao tayari unajionyesha ndani ya chadema.

Waswahili walisema kwamba dalili za mvua ni mawingu. Yanayojionyesha ndani ya chadema kwa sasa yanaashiria hayo niliyoyataja kama chama hicho kinapewa ridhaa ya kutawala nchi.

Je, watanzania tunakubali kugeuzwa nyumbu?

​
:majani7::majani7::majani7::majani7::majani7:
 
Naskia Nyumbu anatabia ya kusahau kiasi kwamba kama anafukuzwa na simba akiona majani pembeni yake yamenawiri anasimama na kuanza kula.

Kifupi ni jingajinga na linawasahau maadui zake kirahisi na kuzani ni marafiki zake.

Tabia gani nyingine ya Nyumbu mnikumbushie.
 
Tabia nyingine inajionesha kwa chadema na wafuasi wake,wamesahau kwamba Walitamka kuwa lowasa ni fisadi leo wamempokea.
 
Ni kweli, nyumbu ni wasahaulifu sana hawapishani na Chadema kabisa.
 
Back
Top Bottom