Watanzania tusiwe kama nyumbu kwa CHADEMA

ama! maelezo yako ulipoanza mpaka katikati mtu angejua kabisa kuwa unawaambia ccm, he kumbe cdm! sifa zinazomstahili mwingine unampa mwingine wewe nyumbu nini?
 
Matunda yenyewe ni Uzinzi na Vurugu.

Labda kwenye moyo wa Wazinzi like Mwenyekiti na Katibu wataalam wa kuvunja ndoa na Kula bata na wapenzi wao nje ya nchi.

Post ya hovyo kabisa hii. Jikite kwenye mada. This is home of GT!
 
ccm ni mafisi kabisa,yanawatafuna hata wale maskini hohehahe wa kitanzania.miaka 52 inatosha wafungashe virago tu!
 
Asante kwa ushauri nyumbu mwenzetu uliye ng'ambo
.
 
Hivi ni kwanini watu Wa ccm ni Kama wako peponi hawana habari na maisha ya dhiki humu duniani?
Na kwakuwa unatukana vijana kuwa hatuna muda Wa kutafakari,basi subiri tafakuri yao mwaka 2015,tumekataa kutumika kwa maslahi ya wachache,watto Wa vigogo wamejaa secta nyeti inamaana wanaakili kuliko wengine? Mmeifanya nchi kuwa ya kifalme kila kitu kurithishana.
 
We unahofia nini CHADEMA ikifa CCM itapata ushindi wa ubwete sasa yanini kuandika makala ndefu, kama MWIGAMBA anautaka ubunge wa Arusha mjini 2015 siyo mbali ajipange tu kama nyota inang'aa atashinda, tusilaumu kitu amabacho kimeshatokea bali tuangalie tusonge vipi mbele,

​
NA BRITISH ECONOMIST,
NYUMBU ni wanyama wa ajabu, nadhani ni wanyama walio na akili ndogo kuliko wanyama wote wa porini. Wanyama hao wakishaamua kufanya kitu watakifanya tu bila kujali ni madhara gani yatatokana na uamuzi wao.

Mfano nyumbu wanaweza kuwa na kiu wakaamua kwenda kunywa maji kwenye mto uliojaa mamba. Kwa wingi wao watafika mtoni na kuanza kunywa maji huku mamba wenye njaa kali wakijikamatia nyumbu mmoja mmoja wakizamisha majini na kujitafunia. Nyumbu waliobaki wataendelea kunywa maji bila kujali yanayowakuta wenzao, wakimaliza kunywa maji wanaondoka zao, lakini wakisikia kiu tena wanarudi palepale bila kukumbuka kuwa kuna wenzao waliotafunwa, na wanaendelea kutafunwa wengine!

Au wakati mwingine nyumbu wanaweza wakaamua kuvuka mto wenye kina kirefu, kwa kuutegemea wingi wao, wataingia kwenye mto ambapo karibu nusu yao watabaki maiti katika mto huo wenye kina kirefu huku wengine wakifanikiwa kuvuka.

Daima hayo ndiyo maisha ya nyumbu, kukilenga ili wakitimize kile wanachokiangalia kwa wakati huo bila kujali madhara ya baadaye.

Tofauti na nyumbu binadamu tumejaliwa akili, pamoja na matatizo na shida tunavyoweza kuwa navyo, katika kuvikabili ni lazima tupime madhara na faida ya kufanya hivyo. Kama madhara yanazidi faida tunaona bora tuache. Ni heri mtu kubaki na shida au matatizo kuliko kutoa uhai kwa tamaa ya kutaka kumaliza matatizo au shida.

Kwa nini nasema hivyo? Kwa sasa kuna mageuzi ya kisiasa, hasa katika nchi nyingi za Kiafrika, ambapo vyama vikongwe vya siasa, hasa vilivyopigania uhuru wa nchi vinazozitawala na kuupata toka kwa wakoloni, vinapata shinikizo toka kwa vyama vya upinzani la kuvitaka vyama hivyo vikongwe vikae pembeni na kuviachia vyama vipya vya upinzani kutawala.

Shinikizo hilo limefanikiwa katika baadhi ya nchi, ambapo vyama vya upinzani vimeviondoa madarakani vyama vikongwe. Lakini hatahivyo baada ya kuchukua madaraka, vyama vilivyokuwa vya upinzani, vimeshindwa kuionyesha neema viliyokuwa vikiimba kabla ya kuingia madarakani. Na badala yake vinafanya vibaya zaidi kuliko hata vyama vikongwe vinavyoondolewa madarakani.

Kabla sijaendelea naomba nieleweke. Sio kwamba naikataa demokrasia, mimi ni mpenzi mkubwa wa demokrasia, ila ninachokikataa ni demokrasia hiyo kutugeuza nyumbu ambaye kiu ya maji inamsahaulisha kuwa ndani ya mto kuna mamba, hivyo badala ya nyumbu kumaliza kiu yake akaishia kuumaliza uhai wake.

Ninachokitaka na kukiomba kwa Mungu ni demokrasia kwa maana halisi, demokrasia itakayotufanya tuyapate mabadiliko tutakayoyataka na kutuacha salama. Nadhani hiyo ina tofauti na mageuzi yanayoimbwa na walio wengi.

Sababu mabadiliko na mageuzi ni vitu viwili vinavyotofautiana, mabadiliko yanakuja taratibu kwa wanaoyataka kupata muda wa kuyatafakari ili wakayapate yaliyo mema. Lakini mageuzi hayatoi muda wa kutafakari.

Jambo la kusikitisha ni kwamba hapa nchini kwetu kuna kila dalili ya kutokea mageuzi. Watu hawaonekani kutafakari kuhusu kitu wanachokitaka kinachoweza kuwa mbadala wa kile walichokichoka. Wao wanachokitaka ni kukiona cha zamani kinaondoka na kuja kingine bila kujali kinachokuja kimekaaje, ilimradi tu yawepo mageuzi.

Mfano kuna Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chama hicho kinaonekana kupata ushabiki wa kisiasa kwa kasi sana. Naamini kabisa kwamba wananchi wametokea kukishabikia chama hicho bila kupata muda wa kutafakari kwanza. Wao wanachokiangalia ni mageuzi lakini hawajali mageuzi hayo yana nini ndani yake.

Hebu tukakiangalie hicho chama. Chadema kinaundwa na idadi kubwa ya vijana. Na kawaida ya vijana walio wengi hupendelea mageuzi badala ya mabadiliko, yaani kitu tunachoweza kukiita bandika bandua, hapo tuelewe hakuna muda wa kutafakari. Vijana mara nyingi hawana muda wa kuyapima mema na mabaya yaliyomo katika mageuzi wanayoyatamani na kisha kuyalinganisha.

Mfano wa hivi karibuni ni wa tukio lililotokea kwenye mkutano wa Kanda wa Chadema kule Arusha. Kutokana na sababu ambazo haziko wazi, kundi la vijana waliomchoka mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha, Samson Mwigamba, likiongozwa na mbunge wa Arusha Mjini,Godbles Lema, liliuvamia mkutano huo wa kanda kwa mtindo wa shambulizi la kigaidi na kuanza kumchapa ngumi mwenyekiti huyo wa mkoa bila kuheshimu wala kufuata kanuni yoyote ya mkutano uliokuwa ukiendelea.

Kilichodaiwa ni kwamba eti Mwigamba aliandika mambo fulani kwenye mtandao wa kijamii. Kwahiyo vijana hao wakadai kwamba Mwigamba afukuzwe kwenye nafasi zake zote alizokuwa akizishikilia kwenye chama hicho. Wala Mwigamba hakupewa kwanza nafasi ya kujitetea kufuatia uvamizi huo wa kigaidi. Kwahiyo demokrasia iko wapi? Kilichoangaliwa pale ni mageuzi na sio demokrasia.

Nikirudi upande wa pili, tutaona kwamba Mwigamba ni mtu anayeipenda Chadema kuliko watu wengi walio wanachama wa chama hicho.

Naweza kusema kwamba bila yeye, Mwigamba, si ajabu Lema asingejuwa mbunge kwa wakati huu. Lakini inaonekana Lema anauangalia ubunge kuliko anavyokijali chama, pengine ndiyo maana akaongoza uvamizi huo ili kumchafulia Mwigamba kwa hofu ya kwamba pengine Mwigamba anaweza akautamani ubunge katika uchaguzi ujao na hivyo kumnyang’anya Lema kitumbua mdomoni.

Katika hatua nyingine ni kwamba yaleyale yaliyodaiwa na Lema kwamba Mwigamba aliyafanya kiusaliti, kuandika kwenye mtandao wa kijamii kukikosoa chama chake, naye Lema kayatumia vilevile kuwashambulia viongozi wa chama chake!

Lema kautumia mtandao wa kijamii kumshambulia Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zubeir Zitto maarufu kama Zitto Kabwe, akidai kwamba ni mtu mnafiki.

Hebu fikiria mtu aliyemshambulia mwenzake kuwa katenda kosa fulani analitumia kosa lilelile kuwashambulia wenzake kwa mtindo uleule, akiliona kosa hilo kuwa ni halali kwake!

Lakini hatahivyo tukiziangalia tuhuma zilizotolewa na Lema dhidi ya Naibu Katibu Mkuu wa chama chake pia tutagundua kitu kingine. Ni kwamba Zitto Kabwe muda wote amekuwa akijipambanua kama mzalendo wa kweli wan chi hii, mtu aliye na uchungu na nchi pamoja na watu wake. Mpaka Zitto akafikia hata kuzikataa posho za vikao vya bunge, wananchi wakamuona mzalendo kwa hilo.

Lakini kumbe mtu anayekataa kupokea shilingi 70,000/= kama posho ya kikao cha bunge anapokea kati ya shilingi 700,000/= na 1,000,000/= kama posho ya kikao cha Kamati ya Bunge anayoisimamia! Hivi kweli kuna uzalendo hapo? Huyu ni mzalendo au anayewageuza wazalendo kuwa matuyuyu?

Hayo niliyoyataja ni baadhi ya mambo machache yanayoonyesha mwenendo wa chama kinachotamaniwa na baadhi ya wananchi kuwa mbadala wa chama tawala. Hiyo ina tofauti gani na nyumbu wenye kiu kwenda kunywa maji kwenye mto uliojaa mamba?

Sababu yanayojitokeza kwenye chama hicho kikuu cha upinzani yanaonekana madogo kwa vile chama hicho hakijapewa ridhaa ya kuvisimamia vyombo vya dola, lakini pindi wananchi wakikipa ridhaa hiyo sitaona ajabu yakitokea hapa nchini kwetu kama yale ya Renamo kule Msumbiji, Unita kule Angola, M 23 kule Congo nakadhalika. Maana hayo yote ni matokeo ya uasi katika uendeshaji wa nchi, ambao tayari unajionyesha ndani ya Chadema.

Waswahili walisema kwamba dalili za mvua ni mawingu. Yanayojionyesha ndani ya Chadema kwa sasa yanaashiria hayo niliyoyataja kama chama hicho kinapewa ridhaa ya kutawala nchi.

Je, Watanzania tunakubali kugeuzwa nyumbu?

​
:majani7::majani7::majani7::majani7::majani7:
 
Nilipofikia tu kwamba eti vijana walimvamia Samson Mwigamba kwenye kikao eti kama shambulio la kigaidi na kuanza kumpiga ngumi,
Nikaona hakuna haja ya kuendelea kupoteza muda wangu kwa kusoma upuuzi kutoka kwa mtu mjinga... na log off.
 
Asante sana kwa Uchambuzi wako mzuri.....lakini mfano wako kuhusu nyumbu unahitaji upatiwe elimu ya wildlife hasa in ecosystem....ndo utajua umuhimu wa maisha hayo kuwa kama hivyo!

Pili maneno ya kusema vijana wanataka mageuzi na si mabadiliko....yalisemwa tangu enzi za kina Nyerere kwa kuwa kipindi wanapigania uhuru walikuwa vijana....walisema kuwa hatuwezi kujiongoza na maendeleo yatafika mwisho....walitoa mfano wa nchi zilizopata uhuru na ambazo zilikuwa na settlers bado! Nadhani kwa post hii,ungekuwepo kipindi hicho ungepinga uhuru kama unavyotoa mifano kwa kusema vyama vya upinzani vimeharibu kabisa bila kufanya tafiti za kweli.
Sababu ya watu wengi kwa sasa kuiunga mkono chadema ni kutaka tuanze upya....kuondoa ukoloni mambo leo....ardhi kuwa mali ya watanzania sio wawekezaji jambo ambalo zimbabwe limewezekana....na kuthaminiwa kwa mtu wa mtanzania....CHADEMA sio Mbowe na Lema ....chadema ni mimi na wewe....ni kama tulivyoambiwa kipindi cha uhuru,TANU ni mimi na wewe!
 
Unajua ukiishi kwa mazoea basi utaishi hata chooni na kinyesi. Yaani kwa miaka hii 52 ya uhuru iliyojaa umasikini kutokana na ufisadi wa ma CCM, bado mtu unang'ang'ania tu? Kweli mazoea yana taabu.
 
Hivi ni kwanini watu Wa ccm ni Kama wako peponi hawana habari na maisha ya dhiki humu duniani?
Na kwakuwa unatukana vijana kuwa hatuna muda Wa kutafakari,basi subiri tafakuri yao mwaka 2015,tumekataa kutumika kwa maslahi ya wachache,watto Wa vigogo wamejaa secta nyeti inamaana wanaakili kuliko wengine? Mmeifanya nchi kuwa ya kifalme kila kitu kurithishana.

Mkuu umegusa kunako,yaani hii nchi wanyonge tunaishi kama tuko utumwani vile. Kila lenye manufaa ni wao na familia zao. Huyu mtoa maada nadhani atakuwa miongoni mwao,kinyume na hapo atakuwa tahira,maana hana huruma na mtanzania anayenyanyaswa na ccm.
 
huyo ni yule aliyekuwa kiongozi wa Arusha chadema akatimuliwa sasa anajiita British Economist
 
Kama mambo yenyewe ndo hayo Mimi natangaza kwamba ni bonge la NYUMBU
 
Nakumbuka Maremu Babu yangu alishawahi kuniambia kua - Ukiona kitu kinaongelewa sana tena Sana basi ujue kinakubalika!
... na kwamba 'shamba lenye ngano bora, ndilo hushambuliwa sana na ndege waharibifu'(CCM).
 
​
NA BRITISH ECONOMIST,
NYUMBU ni wanyama wa ajabu, nadhani ni wanyama walio na akili ndogo kuliko wanyama wote wa porini. Wanyama hao wakishaamua kufanya kitu watakifanya tu bila kujali ni madhara gani yatatokana na uamuzi wao.

Mfano nyumbu wanaweza kuwa na kiu wakaamua kwenda kunywa maji kwenye mto uliojaa mamba. Kwa wingi wao watafika mtoni na kuanza kunywa maji huku mamba wenye njaa kali wakijikamatia nyumbu mmoja mmoja wakizamisha majini na kujitafunia. Nyumbu waliobaki wataendelea kunywa maji bila kujali yanayowakuta wenzao, wakimaliza kunywa maji wanaondoka zao, lakini wakisikia kiu tena wanarudi palepale bila kukumbuka kuwa kuna wenzao waliotafunwa, na wanaendelea kutafunwa wengine!

Au wakati mwingine nyumbu wanaweza wakaamua kuvuka mto wenye kina kirefu, kwa kuutegemea wingi wao, wataingia kwenye mto ambapo karibu nusu yao watabaki maiti katika mto huo wenye kina kirefu huku wengine wakifanikiwa kuvuka.

Daima hayo ndiyo maisha ya nyumbu, kukilenga ili wakitimize kile wanachokiangalia kwa wakati huo bila kujali madhara ya baadaye.

Tofauti na nyumbu binadamu tumejaliwa akili, pamoja na matatizo na shida tunavyoweza kuwa navyo, katika kuvikabili ni lazima tupime madhara na faida ya kufanya hivyo. Kama madhara yanazidi faida tunaona bora tuache. Ni heri mtu kubaki na shida au matatizo kuliko kutoa uhai kwa tamaa ya kutaka kumaliza matatizo au shida.

Kwa nini nasema hivyo? Kwa sasa kuna mageuzi ya kisiasa, hasa katika nchi nyingi za Kiafrika, ambapo vyama vikongwe vya siasa, hasa vilivyopigania uhuru wa nchi vinazozitawala na kuupata toka kwa wakoloni, vinapata shinikizo toka kwa vyama vya upinzani la kuvitaka vyama hivyo vikongwe vikae pembeni na kuviachia vyama vipya vya upinzani kutawala.

Shinikizo hilo limefanikiwa katika baadhi ya nchi, ambapo vyama vya upinzani vimeviondoa madarakani vyama vikongwe. Lakini hatahivyo baada ya kuchukua madaraka, vyama vilivyokuwa vya upinzani, vimeshindwa kuionyesha neema viliyokuwa vikiimba kabla ya kuingia madarakani. Na badala yake vinafanya vibaya zaidi kuliko hata vyama vikongwe vinavyoondolewa madarakani.

Kabla sijaendelea naomba nieleweke. Sio kwamba naikataa demokrasia, mimi ni mpenzi mkubwa wa demokrasia, ila ninachokikataa ni demokrasia hiyo kutugeuza nyumbu ambaye kiu ya maji inamsahaulisha kuwa ndani ya mto kuna mamba, hivyo badala ya nyumbu kumaliza kiu yake akaishia kuumaliza uhai wake.

Ninachokitaka na kukiomba kwa Mungu ni demokrasia kwa maana halisi, demokrasia itakayotufanya tuyapate mabadiliko tutakayoyataka na kutuacha salama. Nadhani hiyo ina tofauti na mageuzi yanayoimbwa na walio wengi.

Sababu mabadiliko na mageuzi ni vitu viwili vinavyotofautiana, mabadiliko yanakuja taratibu kwa wanaoyataka kupata muda wa kuyatafakari ili wakayapate yaliyo mema. Lakini mageuzi hayatoi muda wa kutafakari.

Jambo la kusikitisha ni kwamba hapa nchini kwetu kuna kila dalili ya kutokea mageuzi. Watu hawaonekani kutafakari kuhusu kitu wanachokitaka kinachoweza kuwa mbadala wa kile walichokichoka. Wao wanachokitaka ni kukiona cha zamani kinaondoka na kuja kingine bila kujali kinachokuja kimekaaje, ilimradi tu yawepo mageuzi.

Mfano kuna Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chama hicho kinaonekana kupata ushabiki wa kisiasa kwa kasi sana. Naamini kabisa kwamba wananchi wametokea kukishabikia chama hicho bila kupata muda wa kutafakari kwanza. Wao wanachokiangalia ni mageuzi lakini hawajali mageuzi hayo yana nini ndani yake.

Hebu tukakiangalie hicho chama. Chadema kinaundwa na idadi kubwa ya vijana. Na kawaida ya vijana walio wengi hupendelea mageuzi badala ya mabadiliko, yaani kitu tunachoweza kukiita bandika bandua, hapo tuelewe hakuna muda wa kutafakari. Vijana mara nyingi hawana muda wa kuyapima mema na mabaya yaliyomo katika mageuzi wanayoyatamani na kisha kuyalinganisha.

Mfano wa hivi karibuni ni wa tukio lililotokea kwenye mkutano wa Kanda wa Chadema kule Arusha. Kutokana na sababu ambazo haziko wazi, kundi la vijana waliomchoka mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha, Samson Mwigamba, likiongozwa na mbunge wa Arusha Mjini,Godbles Lema, liliuvamia mkutano huo wa kanda kwa mtindo wa shambulizi la kigaidi na kuanza kumchapa ngumi mwenyekiti huyo wa mkoa bila kuheshimu wala kufuata kanuni yoyote ya mkutano uliokuwa ukiendelea.

Kilichodaiwa ni kwamba eti Mwigamba aliandika mambo fulani kwenye mtandao wa kijamii. Kwahiyo vijana hao wakadai kwamba Mwigamba afukuzwe kwenye nafasi zake zote alizokuwa akizishikilia kwenye chama hicho. Wala Mwigamba hakupewa kwanza nafasi ya kujitetea kufuatia uvamizi huo wa kigaidi. Kwahiyo demokrasia iko wapi? Kilichoangaliwa pale ni mageuzi na sio demokrasia.

Nikirudi upande wa pili, tutaona kwamba Mwigamba ni mtu anayeipenda Chadema kuliko watu wengi walio wanachama wa chama hicho.

Naweza kusema kwamba bila yeye, Mwigamba, si ajabu Lema asingejuwa mbunge kwa wakati huu. Lakini inaonekana Lema anauangalia ubunge kuliko anavyokijali chama, pengine ndiyo maana akaongoza uvamizi huo ili kumchafulia Mwigamba kwa hofu ya kwamba pengine Mwigamba anaweza akautamani ubunge katika uchaguzi ujao na hivyo kumnyang'anya Lema kitumbua mdomoni.

Katika hatua nyingine ni kwamba yaleyale yaliyodaiwa na Lema kwamba Mwigamba aliyafanya kiusaliti, kuandika kwenye mtandao wa kijamii kukikosoa chama chake, naye Lema kayatumia vilevile kuwashambulia viongozi wa chama chake!

Lema kautumia mtandao wa kijamii kumshambulia Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zubeir Zitto maarufu kama Zitto Kabwe, akidai kwamba ni mtu mnafiki.

Hebu fikiria mtu aliyemshambulia mwenzake kuwa katenda kosa fulani analitumia kosa lilelile kuwashambulia wenzake kwa mtindo uleule, akiliona kosa hilo kuwa ni halali kwake!

Lakini hatahivyo tukiziangalia tuhuma zilizotolewa na Lema dhidi ya Naibu Katibu Mkuu wa chama chake pia tutagundua kitu kingine. Ni kwamba Zitto Kabwe muda wote amekuwa akijipambanua kama mzalendo wa kweli wan chi hii, mtu aliye na uchungu na nchi pamoja na watu wake. Mpaka Zitto akafikia hata kuzikataa posho za vikao vya bunge, wananchi wakamuona mzalendo kwa hilo.

Lakini kumbe mtu anayekataa kupokea shilingi 70,000/= kama posho ya kikao cha bunge anapokea kati ya shilingi 700,000/= na 1,000,000/= kama posho ya kikao cha Kamati ya Bunge anayoisimamia! Hivi kweli kuna uzalendo hapo? Huyu ni mzalendo au anayewageuza wazalendo kuwa matuyuyu?

Hayo niliyoyataja ni baadhi ya mambo machache yanayoonyesha mwenendo wa chama kinachotamaniwa na baadhi ya wananchi kuwa mbadala wa chama tawala. Hiyo ina tofauti gani na nyumbu wenye kiu kwenda kunywa maji kwenye mto uliojaa mamba?

Sababu yanayojitokeza kwenye chama hicho kikuu cha upinzani yanaonekana madogo kwa vile chama hicho hakijapewa ridhaa ya kuvisimamia vyombo vya dola, lakini pindi wananchi wakikipa ridhaa hiyo sitaona ajabu yakitokea hapa nchini kwetu kama yale ya Renamo kule Msumbiji, Unita kule Angola, M 23 kule Congo nakadhalika. Maana hayo yote ni matokeo ya uasi katika uendeshaji wa nchi, ambao tayari unajionyesha ndani ya Chadema.

Waswahili walisema kwamba dalili za mvua ni mawingu. Yanayojionyesha ndani ya Chadema kwa sasa yanaashiria hayo niliyoyataja kama chama hicho kinapewa ridhaa ya kutawala nchi.

Je, Watanzania tunakubali kugeuzwa nyumbu?

​
:majani7::majani7::majani7::majani7::majani7:
Maskini! umejitahidi kuiponda CDM, lakini hujapata support hata moja. Mlishaambiwa CDM wapo na Mungu, kwamba walanza nae na watamaliza nae lakini mnajifanya hamuelewi na Shetani wenu.
 
Kaandika utafikiri muungwana, kumbe pimbi tu mwenye njaa na pesa za mafisadi! Hizi buku saba saba za mtaa wa Lumumba zitawafanya mapimbi sana! Nyumbu mwenyewe!
 
Back
Top Bottom