PreGE2025 Watanzania tusiruhusu tena Bunge Kibogoyo dhaifu kama hili, lisilo na Meno, kukosa Kambi ya Upinzani na kushindwa kuisimamia Serikali kikamilifu!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,103
Reaction score
128,718
Wanabodi
Makala yangu gazeti la Mwananchi la leo

Tusiruhusu Tena Bunge Lisilo na Kambi Rasmi ya Upinzani 1.jpg
Bunge la 12, linatarajiwa kuvunjwa hivi karibuni, hii ni makala ya kuwaomba Watanzania tusiruhusu tena Bunge lisilo na kambi rasmi ya upinzani kama Bunge hili la 12!, limekuwa ni Bunge dhaifu kutokana na kukosa meno, hivyo limekuwa kama ni Bunge kibogoyo na na rubber stempu ya serikali, na hata ikitokea Watanzania, kwa mapenzi yao kwa chama chao kipenzi, wakaamua kuichagua tena CCM tuu pekee, katika uchaguzi huru na wa haki, ulioendeshwa na tume huru, halali na shirikishi ya uchaguzi, huo utakuwa ndio uamuzi wa walio wengi, tutauheshimu, ila tutamuomba rais ajaye, atuteulie wapinzani makini kwenye zile nafasi zake 10 za uteuzi, ili kulipa Bunge meno ya kuisimamia serikali kikamilifu!. Tunataka Bunge lijalo, liwe ni Bunge lenye meno na uwezo wa kuisimamia serikali yetu kikamilifu, Bunge ambalo serikali ikikosea, lina uwezo kuiambia serikali hapa mmekosea, na kuirekebisha!.

Mimi mwenzenu, sio tuu nimepiga kura toka uchaguzi wa mwaka 1990 ambao ndio uchaguzi wa mwisho wa chama kimoja!, kwenye urais, tulikuwa tunampigia kura mgombea mmoja anayeshindana na kivuli!, Sasa tunapojiandaa kwa uchaguzi wa 2025, zifanyike juhudi za makusudi, kiingereza inaitwa, affirmative action, kuhakikisha tusiwe tena na Bunge la vyama vingi jina tuu, kama Bunge hili la 12, bila kambi rasmi ya upinzanini Bungeni. Tufungue zaidi milango ya demokrasia ya kweli, wagombea wa ukweli wajitokeze, washindane kwenye uchaguzi wa haki, unaochezwa kwenye uwanja sawa, ili kuzuia wagombea wa chama kimoja kushindana na wagombea vivuli!, hivyo kushinda kwa mteremko!.

Nimeshiriki chaguzi mbalimbali nikiwa mwandishi wa habari na kuna wakati nilikuwa mwangalizi wa chaguzi mbalimbali, ukiwemo uchaguzi wa Marekani wa mwaka jana, kule unaona demokrasia ya kweli inayoanzia kwenye kitu kinaitwa primaries, Tanzania inabidi tufike mahali tufanye uchaguzi wa kweli na sio igizo la uchaguzi!.

Nimebahatika kushiriki chaguzi zote za vyama vingi nchini toka tuliporejesha mfumo wa vyama vingi ile 1992 kwa ule uchaguzi mdogo wa jimbo la Kwahani, 1994, uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, 2020, na sasa 2025, hivyo kuna vitu niliviona naweza kuvitolea ushauri wa busara, kwa kuviandika, vinaweza kusaidia jambo kuelekea uchaguzi wa 2025.

Baada ya uchaguzi wa 2020 na akidi ya uwepo wa kambi rasmi ya upinzani kutotimia, nilishauri, turekebishe kanuni, ili inapokosekana kambi rasmi ya upinzani, wale wabunge wachache wa upinzani, waunde kambi ya wachache (the minority) wayabebe yale majukumu ya kambi rasmi ya upinzani. Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Mabunge yote ya Jumuiya ya Madola, zile oversight committee, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzani ili ziwe na meno ya kuisimamia serikali kikamilifu zaidi. Je, Bunge letu ni Bunge Butu?. Angalia Bunge la Uingereza lenye meno linavyong'ata Serikali. Je, Kuna ubaya tukiiga?

Uchaguzi huu bila mabadiliko ya katiba unaweza kuwa kama ule uliopita, wakashinda chama kimoja!, wapinzani wakikosekana, rais ajaye ateue wapinzani makini wamsaidie.

Udhaifu mkubwa wa Bunge hili, umeshuhudiwa kipindi cha IGA ya DPW "IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

Japo majukumu ya Bunge ni kutunga sheria na kuisimamia serikali, Bunge letu, halitungi sheria wala haliisimamii serikali ndio maana serikali inatunga miswada batili kinyume na katiba, Bunge linaipitisha kama rubber stempu Bunge linatimiza wajibu wake kikamilifu utungaji wa Sheria na kuismamia Serikali?. Nani kati Bunge na serikali anayetutungia hizi Sheria Batili?!

Sheria ya uchaguzi iliyopita ilikuwa na vipengele vinavyokwenda kinyume cha katiba, Mahakama Kuu ikavibatilisha, serikali ya wakati huo, ikapeleka muswada wa marekebisho ya katiba kwa hati ya dharura, huo ubatili wa sheria hiyo, ukachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Mahakama Kuu ikashikilia msimamo, sheria hiyo ni batili, na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa kuuchomekea ubatili huo ndani ya katiba yetu pia ni batili!. Bunge letu, Bunge Kibri, Jeuri? Linawezaje kutunga tena Sheria batili? Limeamriwa kuondoa ubatili huo, linapata wapi jeuri ya kuidharau Mahakama?

Mahakama ya Rufaa , kwa kuliheshimu Bunge, ikaliamuru Bunge ndio liuondoe ubatili huo, Bunge lilivyo kiburi na jeuri, halikuuondoa ubatili huo mpaka leo!, Baada ya Rais Samia kushika madaraka, akaunda kikosi kazi, maoni ya wengi ni kuwepo kwa haja ya kufanya mabadiliko madogo ya katiba, (minimum reforms), Bunge limegoma, limetunga sheria mpya ya uchaguzi, yenye ubatili ule ule ulioshabatilishwa na mahakama!. Tungekuwa na kambi rasmi ya upinzani, hili lisingetokea!.

Bunge halina mamlaka ya kubadili katiba kwa sheria ya kawaida, katiba inabadilishwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba, Bunge hili litunga sheria namba 2 ya 2024 kilicho unda INEC, kifungu cha 4 kinasema kutakuwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya JMT, iliyoanzishwa chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ambayo itajulikana pia kama INEC. Ukifungua Ibara ya 74 ya katiba, hukuti neno INEC, unakutana na neno NEC, hivyo ili kuihalalisha INEC, kulipaswa kufanyike kwanza mabadiliko madogo ya katiba, kuondoa neno NEC na kuchomeka neno INEC ndani ya katiba, ndipo Bunge litunge sheria ya INEC. Bunge halina mamlaka ya kutunga sheria yoyote kinyume cha katiba!.

Mabadiliko hayo madogo ya katiba, pia yangehusisha Ibara ya 98(1) na (2) ya Katiba ya JMT kubadilisha jina la Tume ya uchaguzi kwa kuongeza neno huru/independent na sio neno Tume ya Uchaguzi NEC.

Tungekuwa na kambi rasmi ya upinzani, hili lisingetokea. Nasubiri kwa hamu, kuona chapisho jipya la katiba, ambalo litaongeza neno Huru kwenye Tume ya Uchaguzi, ndipo kisha tuulizane kunakohusika, nani ana mamlaka hata ya kuongeza herufi moja kwenye katiba yetu bila mabadiliko ya katiba!.

Kwa vile Bunge hili limemalizika, likiwa na udhaifu mkubwa wa Bunge la upande mmoja, kama Bunge la upande mmoja limetokana na Watanzania kuwachagua kwa haki wagombea wa chama kimoja, Watanzania wakiamua kuchague vile vile kama uchaguzi wa 2020, huo utakuwa ndio uamuzi wa Watanzania, Tutamuomba rais ajaye aliokoe Bunge letu liwe ni Bunge lenye meno, limsaidie serikali yake.

Naendelea kushauri, Tanzania bado hatuna upinzani imara, hivyo CCM na serikali yake inawajibu wa kusaidia, ule mpaka wa watu kugawana nusu mkate, urejelewe ili uchaguzi huu, tuwatendee haki Watanzania, tusawazishe uwanja, tuingie uwanjani kwenye uwanja ulio sawa, ( a level playing field), tuboreshe kanuni za mchezo kwa fair play, tuweke refa mtenda haki bin haki, ili mwisho wa mchezo, mshindi apatikane kwa haki, tufurahie ushindi wa haki, tena kwa hisia zangu, hizi mambo za figisu, zinaweza kuwa ndio zimechagia kwenye ile karma iliyopelelekea kutokea kwa lile tukio lile!, tusipojirekebisha hii 2025, tutapata Bunge kama la mwaka 2020, hata tukio kama lile linaweza kuja kujirudia!, tena namuomba Dada Mkubwa, kama ikimpendeza, hata kale ka simba ka Kizimkazi, kanaweza kuondolewe tuu kwenye ile cage, ili kalete ushindani wa kweli, vinginevyo kama tunafurahia kushindana na vivuli!.
Hitimisho
Ili hili liwezekane tusirudie makosa ya 2020, tunatakiwa tufanye mambo matatu yafuatayo.
1. Tanzania bado hatuna strong serious opposition to check out CCM, hivyo kwanza nimeshauri Pre GE2025 - Wapinzani wa Tanzania wasaidiwe kuachana na siasa za kufikirika!

2. Kwa vile Chadema ndicho chama pekee cha upinzani kwa huku bara, chenye angalau angalau matumaini ya kuweza kuleta challenge kwa CCM, nimeshauri Wito: Watu Wenye Uwezo, Tujitokeze Tujitolee Kumsaidia TAL na Kuisaidia Chadema to Play Real Politics, No Reforms No Election ni Utopian Politics!.

3. Kumuomba yule mtumishi wetu No.1, Rais wa JMT, asiwasikilize kabisa wahafidhina wa chama chake, na wasaidizi wake sheria wasiomsaidia kitu, alipe Bunge hili some extension of time, lifanye minimum reform za katiba, tufanye uchaguzi huru kweli na wa haki kweli, kale ka simba ka Kizimkazi kalikozuiliwa kwenye ile.cage, kaachiwe, watu warejee mezani kwenye yale mazungumzo ya nusu mkate, Bunge lijalo liwe na kambi rasmi ya upinzani.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 
Tatizo lipo kwa Watanzania basi? tatizo lipo kwa CCM na jopo lao la ujangili wa kudhulumu haki zetu kwa kutotupatia wale tunaowachagua kupitia wizi wao wa kura wa dhahiri.

Leo hii ukifanyika uchaguzi wa haki bila ya ukiritimba wa CCM, pasi na shaka, hao CCM ndio watakuwa minority bungeni na raisi wao atarudi Kizimkazi kucheza na wajukuu.
 
Mkuu nakuunga mkono. Nimesoma tu heading maandishi baadae.
Zamani jamaa walikuwa wanaing'ang'ania Serikali Hadi unaona mabadiliko. Binafsi hili bunge tangu linaanza Hadi linaisha sijawahi kulisikiliza hata siku moja maana wanachokijadili hakina tofauti na tunachokisikia mtaani KWA Viongozi wa Serikali.

Newton third Law of Motion.
Upinzani unaleta opposite thrust ya maendeleo kutoka upande unaopewa changamoto
 
Wanabodi
Makala yangu gazeti la Mwananchi la leo
View attachment 3382170
Bunge la 12, linatarajiwa kuvunjwa hivi karibuni, hii ni makala ya kuwaomba Watanzania tusiruhusu tena Bunge lisilo na kambi rasmi ya upinzani kama Bunge hili la 12!, limekuwa ni Bunge dhaifu kutokana na kukosa meno, hivyo limekuwa kama ni Bunge kibogoyo na na rubber stempu ya serikali, na hata ikitokea Watanzania, kwa mapenzi yao kwa chama chao kipenzi, wakaamua kuichagua tena CCM tuu pekee, katika uchaguzi huru na wa haki, ulioendeshwa na tume huru, halali na shirikishi ya uchaguzi, huo utakuwa ndio uamuzi wa walio wengi, tutauheshimu, ila tutamuomba rais ajaye, atuteulie wapinzani makini kwenye zile nafasi zake 10 za uteuzi, ili kulipa Bunge meno ya kuisimamia serikali kikamilifu!. Tunataka Bunge lijalo, liwe ni Bunge lenye meno na uwezo wa kuisimamia serikali yetu kikamilifu, Bunge ambalo serikali ikikosea, lina uwezo kuiambia serikali hapa mmekosea, na kuirekebisha!.

Mimi mwenzenu, sio tuu nimepiga kura toka uchaguzi wa mwaka 1990 ambao ndio uchaguzi wa mwisho wa chama kimoja!, kwenye urais, tulikuwa tunampigia kura mgombea mmoja anayeshindana na kivuli!, Sasa tunapojiandaa kwa uchaguzi wa 2025, zifanyike juhudi za makusudi, kiingereza inaitwa, affirmative action, kuhakikisha tusiwe tena na Bunge la vyama vingi jina tuu, kama Bunge hili la 12, bila kambi rasmi ya upinzanini Bungeni. Tufungue zaidi milango ya demokrasia ya kweli, wagombea wa ukweli wajitokeze, washindane kwenye uchaguzi wa haki, unaochezwa kwenye uwanja sawa, ili kuzuia wagombea wa chama kimoja kushindana na wagombea vivuli!, hivyo kushinda kwa mteremko!.

Nimeshiriki chaguzi mbalimbali nikiwa mwandishi wa habari na kuna wakati nilikuwa mwangalizi wa chaguzi mbalimbali, ukiwemo uchaguzi wa Marekani wa mwaka jana, kule unaona demokrasia ya kweli inayoanzia kwenye kitu kinaitwa primaries, Tanzania inabidi tufike mahali tufanye uchaguzi wa kweli na sio igizo la uchaguzi!.

Nimebahatika kushiriki chaguzi zote za vyama vingi nchini toka tuliporejesha mfumo wa vyama vingi ile 1992 kwa ule uchaguzi mdogo wa jimbo la Kwahani, 1994, uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, 2020, na sasa 2025, hivyo kuna vitu niliviona naweza kuvitolea ushauri wa busara, kwa kuviandika, vinaweza kusaidia jambo kuelekea uchaguzi wa 2025.

Baada ya uchaguzi wa 2020 na akidi ya uwepo wa kambi rasmi ya upinzani kutotimia, nilishauri, turekebishe kanuni, ili inapokosekana kambi rasmi ya upinzani, wale wabunge wachache wa upinzani, waunde kambi ya wachache (the minority) wayabebe yale majukumu ya kambi rasmi ya upinzani. Mabunge yote ya Jumuiya ya Madola, zile oversight committee, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzani ili kuisimamia serikali kikamilifu zaidi. Wakikosekana, rais ajaye ateue wapinzani makini wamsaidie.

Sheria ya uchaguzi iliyopita ilikuwa na vipengele vinavyokwenda kinyume cha katiba, Mahakama Kuu ikavibatilisha, serikali ya wakati huo, ikapeleka muswada wa marekebisho ya katiba kwa hati ya dharura, huo ubatili wa sheria hiyo, ukachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Mahakama Kuu ikashikilia msimamo, sheria hiyo ni batili, na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa kuuchomekea ubatili huo ndani ya katiba yetu pia ni batili!.

Mahakama ya Rufaa , kwa kuliheshimu Bunge, ikaliamuru Bunge ndio liuondoe ubatili huo, Bunge lilivyo kiburi na jeuri, halikuuondoa ubatili huo mpaka leo!, Baada ya Rais Samia kushika madaraka, akaunda kikosi kazi, maoni ya wengi ni kuwepo kwa haja ya kufanya mabadiliko madogo ya katiba, (minimum reforms), Bunge limegoma, limetunga sheria mpya ya uchaguzi, yenye ubatili ule ule ulioshabatilishwa na mahakama!. Tungekuwa na kambi rasmi ya upinzani, hili lisingetokea!.

Bunge halina mamlaka ya kubadili katiba kwa sheria ya kawaida, katiba inabadilishwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba, Bunge hili litunga sheria namba 2 ya 2024 kilicho unda INEC, kifungu cha 4 kinasema kutakuwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya JMT, iliyoanzishwa chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ambayo itajulikana pia kama INEC. Ukifungua Ibara ya 74 ya katiba, hukuti neno INEC, unakutana na neno NEC, hivyo ili kuihalalisha INEC, kulipaswa kufanyike kwanza mabadiliko madogo ya katiba, kuondoa neno NEC na kuchomeka neno INEC ndani ya katiba, ndipo Bunge litunge sheria ya INEC. Bunge halina mamlaka ya kutunga sheria yoyote kinyume cha katiba!.

Mabadiliko hayo madogo ya katiba, pia yangehusisha Ibara ya 98(1) na (2) ya Katiba ya JMT kubadilisha jina la Tume ya uchaguzi kwa kuongeza neno huru/independent na sio neno Tume ya Uchaguzi NEC.

Tungekuwa na kambi rasmi ya upinzani, hili lisingetokea. Nasubiri kwa hamu, kuona chapisho jipya la katiba, ambalo litaongeza neno Huru kwenye Tume ya Uchaguzi, ndipo kisha tuulizane kunakohusika, nani ana mamlaka hata ya kuongeza herufi moja kwenye katiba yetu bila mabadiliko ya katiba!.

Kwa vile Bunge hili limemalizika, likiwa na udhaifu mkubwa wa Bunge la upande mmoja, kama Bunge la upande mmoja limetokana na Watanzania kuwachagua kwa haki wagombea wa chama kimoja, Watanzania wakiamua kuchague vile vile kama uchaguzi wa 2020, huo utakuwa ndio uamuzi wa Watanzania, Tutamuomba rais ajaye aliokoe Bunge letu liwe ni Bunge lenye meno, limsaidie serikali yake.

Naendelea kushauri, Tanzania bado hatuna upinzani imara, hivyo CCM na serikali yake inawajibu wa kusaidia, ule mpaka wa watu kugawana nusu mkate, urejelewe ili uchaguzi huu, tuwatendee haki Watanzania, tusawazishe uwanja, tuingie uwanjani kwenye uwanja ulio sawa, ( a level playing field), tuboreshe kanuni za mchezo kwa fair play, tuweke refa mtenda haki bin haki, ili mwisho wa mchezo, mshindi apatikane kwa haki, tufurahie ushindi wa haki, tena kwa hisia zangu, hizi mambo za figisu, zinaweza kuwa ndio zimechagia kwenye ile karma iliyopelelekea kutokea kwa lile tukio lile!, tusipojirekebisha hii 2025, tutapata Bunge kama la mwaka 2020, hata tukio kama lile linaweza kuja kujirudia!, tena namuomba Dada Mkubwa, kama ikimpendeza, hata kale ka simba ka Kizimkazi, kanaweza kuondolewe tuu kwenye ile cage, ili kalete ushindani wa kweli, vinginevyo kama tunafurahia kushindana na vivuli!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Dah sikujua kama kukosa teuzi kunauma hivi😢

Ulie juu kupita vyote duniani na mbinguni nisaidie na roho ya ujasiri nisiwe na hasira za kupiga spana baada ya fungu kunikosa na kuendekeza sifa zisizo na kichwa wala miguu ili kutaka upendeleo
 
Mkuu nakuunga mkono. Nimesoma tu heading maandishi baadae.
Zamani jamaa walikuwa wanaing'ang'ania Serikali Hadi unaona mabadiliko. Binafsi hili bunge tangu linaanza Hadi linaisha sijawahi kulisikiliza hata siku moja maana wanachokijadili hakina tofauti na tunachokisikia mtaani KWA Viongozi wa Serikali.

Newton third Law of Motion.
Upinzani unaleta opposite thrust ya maendeleo kutoka upande unaopewa changamoto
Hakuna bunge pale lile ni kundi la majangili tupu
 
Wanabodi
Makala yangu gazeti la Mwananchi la leo
View attachment 3382170
Bunge la 12, linatarajiwa kuvunjwa hivi karibuni, hii ni makala ya kuwaomba Watanzania tusiruhusu tena Bunge lisilo na kambi rasmi ya upinzani kama Bunge hili la 12!, limekuwa ni Bunge dhaifu kutokana na kukosa meno, hivyo limekuwa kama ni Bunge kibogoyo na na rubber stempu ya serikali, na hata ikitokea Watanzania, kwa mapenzi yao kwa chama chao kipenzi, wakaamua kuichagua tena CCM tuu pekee, katika uchaguzi huru na wa haki, ulioendeshwa na tume huru, halali na shirikishi ya uchaguzi, huo utakuwa ndio uamuzi wa walio wengi, tutauheshimu, ila tutamuomba rais ajaye, atuteulie wapinzani makini kwenye zile nafasi zake 10 za uteuzi, ili kulipa Bunge meno ya kuisimamia serikali kikamilifu!. Tunataka Bunge lijalo, liwe ni Bunge lenye meno na uwezo wa kuisimamia serikali yetu kikamilifu, Bunge ambalo serikali ikikosea, lina uwezo kuiambia serikali hapa mmekosea, na kuirekebisha!.

Mimi mwenzenu, sio tuu nimepiga kura toka uchaguzi wa mwaka 1990 ambao ndio uchaguzi wa mwisho wa chama kimoja!, kwenye urais, tulikuwa tunampigia kura mgombea mmoja anayeshindana na kivuli!, Sasa tunapojiandaa kwa uchaguzi wa 2025, zifanyike juhudi za makusudi, kiingereza inaitwa, affirmative action, kuhakikisha tusiwe tena na Bunge la vyama vingi jina tuu, kama Bunge hili la 12, bila kambi rasmi ya upinzanini Bungeni. Tufungue zaidi milango ya demokrasia ya kweli, wagombea wa ukweli wajitokeze, washindane kwenye uchaguzi wa haki, unaochezwa kwenye uwanja sawa, ili kuzuia wagombea wa chama kimoja kushindana na wagombea vivuli!, hivyo kushinda kwa mteremko!.

Nimeshiriki chaguzi mbalimbali nikiwa mwandishi wa habari na kuna wakati nilikuwa mwangalizi wa chaguzi mbalimbali, ukiwemo uchaguzi wa Marekani wa mwaka jana, kule unaona demokrasia ya kweli inayoanzia kwenye kitu kinaitwa primaries, Tanzania inabidi tufike mahali tufanye uchaguzi wa kweli na sio igizo la uchaguzi!.

Nimebahatika kushiriki chaguzi zote za vyama vingi nchini toka tuliporejesha mfumo wa vyama vingi ile 1992 kwa ule uchaguzi mdogo wa jimbo la Kwahani, 1994, uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, 2020, na sasa 2025, hivyo kuna vitu niliviona naweza kuvitolea ushauri wa busara, kwa kuviandika, vinaweza kusaidia jambo kuelekea uchaguzi wa 2025.

Baada ya uchaguzi wa 2020 na akidi ya uwepo wa kambi rasmi ya upinzani kutotimia, nilishauri, turekebishe kanuni, ili inapokosekana kambi rasmi ya upinzani, wale wabunge wachache wa upinzani, waunde kambi ya wachache (the minority) wayabebe yale majukumu ya kambi rasmi ya upinzani. Mabunge yote ya Jumuiya ya Madola, zile oversight committee, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzani ili kuisimamia serikali kikamilifu zaidi. Wakikosekana, rais ajaye ateue wapinzani makini wamsaidie.

Sheria ya uchaguzi iliyopita ilikuwa na vipengele vinavyokwenda kinyume cha katiba, Mahakama Kuu ikavibatilisha, serikali ya wakati huo, ikapeleka muswada wa marekebisho ya katiba kwa hati ya dharura, huo ubatili wa sheria hiyo, ukachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Mahakama Kuu ikashikilia msimamo, sheria hiyo ni batili, na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa kuuchomekea ubatili huo ndani ya katiba yetu pia ni batili!.

Mahakama ya Rufaa , kwa kuliheshimu Bunge, ikaliamuru Bunge ndio liuondoe ubatili huo, Bunge lilivyo kiburi na jeuri, halikuuondoa ubatili huo mpaka leo!, Baada ya Rais Samia kushika madaraka, akaunda kikosi kazi, maoni ya wengi ni kuwepo kwa haja ya kufanya mabadiliko madogo ya katiba, (minimum reforms), Bunge limegoma, limetunga sheria mpya ya uchaguzi, yenye ubatili ule ule ulioshabatilishwa na mahakama!. Tungekuwa na kambi rasmi ya upinzani, hili lisingetokea!.

Bunge halina mamlaka ya kubadili katiba kwa sheria ya kawaida, katiba inabadilishwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba, Bunge hili litunga sheria namba 2 ya 2024 kilicho unda INEC, kifungu cha 4 kinasema kutakuwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya JMT, iliyoanzishwa chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ambayo itajulikana pia kama INEC. Ukifungua Ibara ya 74 ya katiba, hukuti neno INEC, unakutana na neno NEC, hivyo ili kuihalalisha INEC, kulipaswa kufanyike kwanza mabadiliko madogo ya katiba, kuondoa neno NEC na kuchomeka neno INEC ndani ya katiba, ndipo Bunge litunge sheria ya INEC. Bunge halina mamlaka ya kutunga sheria yoyote kinyume cha katiba!.

Mabadiliko hayo madogo ya katiba, pia yangehusisha Ibara ya 98(1) na (2) ya Katiba ya JMT kubadilisha jina la Tume ya uchaguzi kwa kuongeza neno huru/independent na sio neno Tume ya Uchaguzi NEC.

Tungekuwa na kambi rasmi ya upinzani, hili lisingetokea. Nasubiri kwa hamu, kuona chapisho jipya la katiba, ambalo litaongeza neno Huru kwenye Tume ya Uchaguzi, ndipo kisha tuulizane kunakohusika, nani ana mamlaka hata ya kuongeza herufi moja kwenye katiba yetu bila mabadiliko ya katiba!.

Kwa vile Bunge hili limemalizika, likiwa na udhaifu mkubwa wa Bunge la upande mmoja, kama Bunge la upande mmoja limetokana na Watanzania kuwachagua kwa haki wagombea wa chama kimoja, Watanzania wakiamua kuchague vile vile kama uchaguzi wa 2020, huo utakuwa ndio uamuzi wa Watanzania, Tutamuomba rais ajaye aliokoe Bunge letu liwe ni Bunge lenye meno, limsaidie serikali yake.

Naendelea kushauri, Tanzania bado hatuna upinzani imara, hivyo CCM na serikali yake inawajibu wa kusaidia, ule mpaka wa watu kugawana nusu mkate, urejelewe ili uchaguzi huu, tuwatendee haki Watanzania, tusawazishe uwanja, tuingie uwanjani kwenye uwanja ulio sawa, ( a level playing field), tuboreshe kanuni za mchezo kwa fair play, tuweke refa mtenda haki bin haki, ili mwisho wa mchezo, mshindi apatikane kwa haki, tufurahie ushindi wa haki, tena kwa hisia zangu, hizi mambo za figisu, zinaweza kuwa ndio zimechagia kwenye ile karma iliyopelelekea kutokea kwa lile tukio lile!, tusipojirekebisha hii 2025, tutapata Bunge kama la mwaka 2020, hata tukio kama lile linaweza kuja kujirudia!, tena namuomba Dada Mkubwa, kama ikimpendeza, hata kale ka simba ka Kizimkazi, kanaweza kuondolewe tuu kwenye ile cage, ili kalete ushindani wa kweli, vinginevyo kama tunafurahia kushindana na vivuli!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
We mwenyewe chawa tu, ukipewa teuz mnajisahau
 
Bila reforms za uhakika hakuna Bunge la maana, wote wa chama Tawala watakuwa chawa tu
 
Mzee wangu Pascal Mayalla wewe ni hadhina unajua mengi kwa ufasaha na kwa usahihi. Hongera kwa kuendelea kulipigania taifa lako.

Alichokuzidi Lisu ni ujasiri na sadaka aliyoamua kujitoa kwa ajili ya watanzania. Tunakuheshimu na tunakuthamini naomba kwa yale ambayo unaona ni mazito na magumu kuyasimamia kwa sababu ya uhatari wake kwa maisha yako. Basi usimkatishe tamaa shujaa wetu. Muombee kwa Mungu kama nasi tunavyomuombea zaidi sana mabandiko elimishi kama haya uendelee kuyatoa maana kuna bandiko lako uliandika kuhusiana na kelele za chura. Naamini ni ndogo lakini ni muhimu kwa zinaonesha maumivu na masikitiko yetu kuliko kukaa kimya kabisa kana kwamba hakuna baya linaloendelea.

Mungu wa mbinguni akubariki sana mzee wangu Pascal Mayalla
 
Wanabodi
Makala yangu gazeti la Mwananchi la leo
View attachment 3382170
Bunge la 12, linatarajiwa kuvunjwa hivi karibuni, hii ni makala ya kuwaomba Watanzania tusiruhusu tena Bunge lisilo na kambi rasmi ya upinzani kama Bunge hili la 12!, limekuwa ni Bunge dhaifu kutokana na kukosa meno, hivyo limekuwa kama ni Bunge kibogoyo na na rubber stempu ya serikali, na hata ikitokea Watanzania, kwa mapenzi yao kwa chama chao kipenzi, wakaamua kuichagua tena CCM tuu pekee, katika uchaguzi huru na wa haki, ulioendeshwa na tume huru, halali na shirikishi ya uchaguzi, huo utakuwa ndio uamuzi wa walio wengi, tutauheshimu, ila tutamuomba rais ajaye, atuteulie wapinzani makini kwenye zile nafasi zake 10 za uteuzi, ili kulipa Bunge meno ya kuisimamia serikali kikamilifu!. Tunataka Bunge lijalo, liwe ni Bunge lenye meno na uwezo wa kuisimamia serikali yetu kikamilifu, Bunge ambalo serikali ikikosea, lina uwezo kuiambia serikali hapa mmekosea, na kuirekebisha!.

Mimi mwenzenu, sio tuu nimepiga kura toka uchaguzi wa mwaka 1990 ambao ndio uchaguzi wa mwisho wa chama kimoja!, kwenye urais, tulikuwa tunampigia kura mgombea mmoja anayeshindana na kivuli!, Sasa tunapojiandaa kwa uchaguzi wa 2025, zifanyike juhudi za makusudi, kiingereza inaitwa, affirmative action, kuhakikisha tusiwe tena na Bunge la vyama vingi jina tuu, kama Bunge hili la 12, bila kambi rasmi ya upinzanini Bungeni. Tufungue zaidi milango ya demokrasia ya kweli, wagombea wa ukweli wajitokeze, washindane kwenye uchaguzi wa haki, unaochezwa kwenye uwanja sawa, ili kuzuia wagombea wa chama kimoja kushindana na wagombea vivuli!, hivyo kushinda kwa mteremko!.

Nimeshiriki chaguzi mbalimbali nikiwa mwandishi wa habari na kuna wakati nilikuwa mwangalizi wa chaguzi mbalimbali, ukiwemo uchaguzi wa Marekani wa mwaka jana, kule unaona demokrasia ya kweli inayoanzia kwenye kitu kinaitwa primaries, Tanzania inabidi tufike mahali tufanye uchaguzi wa kweli na sio igizo la uchaguzi!.

Nimebahatika kushiriki chaguzi zote za vyama vingi nchini toka tuliporejesha mfumo wa vyama vingi ile 1992 kwa ule uchaguzi mdogo wa jimbo la Kwahani, 1994, uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, 2020, na sasa 2025, hivyo kuna vitu niliviona naweza kuvitolea ushauri wa busara, kwa kuviandika, vinaweza kusaidia jambo kuelekea uchaguzi wa 2025.

Baada ya uchaguzi wa 2020 na akidi ya uwepo wa kambi rasmi ya upinzani kutotimia, nilishauri, turekebishe kanuni, ili inapokosekana kambi rasmi ya upinzani, wale wabunge wachache wa upinzani, waunde kambi ya wachache (the minority) wayabebe yale majukumu ya kambi rasmi ya upinzani. Mabunge yote ya Jumuiya ya Madola, zile oversight committee, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzani ili kuisimamia serikali kikamilifu zaidi. Wakikosekana, rais ajaye ateue wapinzani makini wamsaidie.

Sheria ya uchaguzi iliyopita ilikuwa na vipengele vinavyokwenda kinyume cha katiba, Mahakama Kuu ikavibatilisha, serikali ya wakati huo, ikapeleka muswada wa marekebisho ya katiba kwa hati ya dharura, huo ubatili wa sheria hiyo, ukachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Mahakama Kuu ikashikilia msimamo, sheria hiyo ni batili, na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa kuuchomekea ubatili huo ndani ya katiba yetu pia ni batili!.

Mahakama ya Rufaa , kwa kuliheshimu Bunge, ikaliamuru Bunge ndio liuondoe ubatili huo, Bunge lilivyo kiburi na jeuri, halikuuondoa ubatili huo mpaka leo!, Baada ya Rais Samia kushika madaraka, akaunda kikosi kazi, maoni ya wengi ni kuwepo kwa haja ya kufanya mabadiliko madogo ya katiba, (minimum reforms), Bunge limegoma, limetunga sheria mpya ya uchaguzi, yenye ubatili ule ule ulioshabatilishwa na mahakama!. Tungekuwa na kambi rasmi ya upinzani, hili lisingetokea!.

Bunge halina mamlaka ya kubadili katiba kwa sheria ya kawaida, katiba inabadilishwa kwa sheria ya mabadiliko ya katiba, Bunge hili litunga sheria namba 2 ya 2024 kilicho unda INEC, kifungu cha 4 kinasema kutakuwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya JMT, iliyoanzishwa chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ambayo itajulikana pia kama INEC. Ukifungua Ibara ya 74 ya katiba, hukuti neno INEC, unakutana na neno NEC, hivyo ili kuihalalisha INEC, kulipaswa kufanyike kwanza mabadiliko madogo ya katiba, kuondoa neno NEC na kuchomeka neno INEC ndani ya katiba, ndipo Bunge litunge sheria ya INEC. Bunge halina mamlaka ya kutunga sheria yoyote kinyume cha katiba!.

Mabadiliko hayo madogo ya katiba, pia yangehusisha Ibara ya 98(1) na (2) ya Katiba ya JMT kubadilisha jina la Tume ya uchaguzi kwa kuongeza neno huru/independent na sio neno Tume ya Uchaguzi NEC.

Tungekuwa na kambi rasmi ya upinzani, hili lisingetokea. Nasubiri kwa hamu, kuona chapisho jipya la katiba, ambalo litaongeza neno Huru kwenye Tume ya Uchaguzi, ndipo kisha tuulizane kunakohusika, nani ana mamlaka hata ya kuongeza herufi moja kwenye katiba yetu bila mabadiliko ya katiba!.

Kwa vile Bunge hili limemalizika, likiwa na udhaifu mkubwa wa Bunge la upande mmoja, kama Bunge la upande mmoja limetokana na Watanzania kuwachagua kwa haki wagombea wa chama kimoja, Watanzania wakiamua kuchague vile vile kama uchaguzi wa 2020, huo utakuwa ndio uamuzi wa Watanzania, Tutamuomba rais ajaye aliokoe Bunge letu liwe ni Bunge lenye meno, limsaidie serikali yake.

Naendelea kushauri, Tanzania bado hatuna upinzani imara, hivyo CCM na serikali yake inawajibu wa kusaidia, ule mpaka wa watu kugawana nusu mkate, urejelewe ili uchaguzi huu, tuwatendee haki Watanzania, tusawazishe uwanja, tuingie uwanjani kwenye uwanja ulio sawa, ( a level playing field), tuboreshe kanuni za mchezo kwa fair play, tuweke refa mtenda haki bin haki, ili mwisho wa mchezo, mshindi apatikane kwa haki, tufurahie ushindi wa haki, tena kwa hisia zangu, hizi mambo za figisu, zinaweza kuwa ndio zimechagia kwenye ile karma iliyopelelekea kutokea kwa lile tukio lile!, tusipojirekebisha hii 2025, tutapata Bunge kama la mwaka 2020, hata tukio kama lile linaweza kuja kujirudia!, tena namuomba Dada Mkubwa, kama ikimpendeza, hata kale ka simba ka Kizimkazi, kanaweza kuondolewe tuu kwenye ile cage, ili kalete ushindani wa kweli, vinginevyo kama tunafurahia kushindana na vivuli!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Mmetumia nguvu nyingi kuhakikisha mnaua chadema halafu unasema tusiruhusu bunge dhaifu, chama gani cha upinzani kinaweza kuiwajibisha serikali wakati vyama vilivyobaki vyoote ni mali ya ccm
 
Bunge kuwa la wanaccm watupu ni furaha kwa kila mwanaccm na Pascal Mayalla akiwemo.

Mleta mada unaposema watanzania tusikubali, hiyo nguvu ya watanzania kutokukubali itatoka wapi wakati ccm hamtaki mabadiliko?

Kama kweli unawiwa kuona bunge linakuwa lenye mchanganyiko wa fikra basi andika makala za kuchagiza NO REFORMS NO ELECTION
 
Anayekubali na kushiriki uchaguzi wa Tanzania ni kama hana akili tu(sorry for this). Tanzania hakuna uchaguzi na mwenye akili timamu ambaye ameamua kuitumia analijua hili vizuri sana.

Ndio maana wenye kuzitumia akili zao wameona hakuna sababu ya kufanya hivyo kama hakuna marekebisho ya kanuni za uchaguzi.

Ila sio ajabu maana kwa namna yoyote ile CCM watafanya ili waendelee kuteuana kwenye nafasi za juu(ubovu wa katiba).
 
Back
Top Bottom