mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Mara nyingi watanzania walipokuwa wanaulizwa aina ya rais wanayemtaka, wamekuwa wakisema wanataka rais mkali kwa mafisadi na wabadhirifu, rais atakayeogopwa na waliochini yake. kwa lugha nyingine wanamtaka rais mwenye hulka ya kidikteta kidogo katika kusukuma mambo.
Hili linaonekana ni kutokana na huyu rais anayemaliza muda wake kutokuwa serious katika mambo mengi na pia kuonekana kutoogopwa na waliochini yake. Mfano , aliwahi kusema wezi wa Epa wakirudisha pesa atawasamehe, mapaka leo hatujui nani walirudisha na nani hawajarudisha na hatua gani zimechukuliwa.
Aliwatetea mafisadi wa Escrow badala ya kuonesha ukali kuwaondoa na kuwashitaki. Kinyume chake alidai fedha za escroe hazikuwa za umma. Mpaka leo kina Seith na Rugemalila pamoja na kutoa rushwa kwa viongozi wa serikali hawajachukuliwa hatua yoyote. Zaidi sana pesa zilizowekwa kwenye akaunti ya Stanbic mpaka leo hawajulikani waliozibeba na magunia na sandarusi. Hajaoekana kujali na hili limewafanya wengi wahisi naye ni mnufaika.
Kuna kipindi Sitta akiwa spika alimwambia aongoze ukali kidogo!
Imemlazimu kuvunja baraza la mawaziri mara nyingi kwa utendaji mbovu wa wateule wake. Na mara zote amefanya haya kwa kushinikizwa na sio kwa hiari yake mwenyewe.
Haya yote yamewafanya wananchi waone kwamba Tanzania inahitaji kiongozi dikteta na mkali ili kusukuma mambo yaende. na mara nyingi hata leo ukiwauliza utapata jibu la namna hii.
Je nje ya upinzani kuna uwezekano wa kupata kiongozi wa namna hii ndani ya CCM kati ya wale wenye uwezekano mkubwa wa kupitishwa? Kwa maneno mengine kuna mwelekeo CCM kuzingatia mawazo haya ya wananchi katika vikao vinavyoendelea huko dodoma?