Watanzania tunaibiwa mchana kweupe TANESCO

hydrogen

JF-Expert Member
Nov 12, 2012
993
694
Nimenunua Luku ya 50,000 Leo hii nikakutana na mchanganuo huu

Unit 100.50KWH
Cost TZS 29943.61
Timebased amount 11040.00
Total TZS 50,000

11,040 naelewa ni service charge ya miezi miwili (Juni & Julai). Swali ni kwamba, kama unit 100.50KWH ni shilingi 29,943.61,
Sh. 9,000 imeenda wapi kama sio wizi?

Anaefaham atujuze...
 
hujaweka 18% ya VAT. Lakini mchanganuo wako unatakiwa kuonesha VAT 18%, EWURA 1% na REA (3% kama sikosei).
 
hujaweka 18% ya VAT. Lakini mchanganuo wako unatakiwa kuonesha VAT 18%, EWURA 1% na REA (3% kama sikosei).

Inategemeana kanunua wapi. Kama amenunua kwa Maxmalipo au Selcom risiti zao huwa hazonyeshi huo mchanganuo. Ukinunua Tanesco au kwa maajenti wakubwa ndio risiti zao huonyesha makato yote.
 
hujaweka 18% ya VAT. Lakini mchanganuo wako unatakiwa kuonesha VAT 18%, EWURA 1% na REA (3% kama sikosei).

hata kama hizo kodi zipo hivyo huu ni wizi tu. Yaani nusu wao na nusu yako! Sioni faida yake bora kufunga solar niachane nao.
Sasa, ina maana tanesco hawatengi fedha za miradi mipya? Serikali haitoi hizo pesa za rea? Kama hawatoi, bajeti ya wizara hufanya kazi gani? Ccm iache wizi wake wa mchana vinginevyo wateja wa tanesco wataacha kuitumia huduma yao.
 
Vijana Kwa wazee tuache kulalamika maamzi Ni kujiandikisha kisha kuwasubiri October 25....
 
Yaani mtu unalipa elf 50 inakatwa mpaka unabaki na elf 29!!!!???

Ni wizi uliotukuka. Yaani hata umeme sio necessary goods ndio maana una kodi. Tuseme hizo REA, service charges na mengine hayawezi kukatwa kwenye hiyohiyo hela ya units mpaka watukate separately??
 
Ni wizi uliotukuka. Yaani hata umeme sio necessary goods ndio maana una kodi. Tuseme hizo REA, service charges na mengine hayawezi kukatwa kwenye hiyohiyo hela ya units mpaka watukate separately??

kwa kweli serikar ya ccm inabidi ipumzike. tumechoka.
 
Ref BP80KM6129
Dongo La Kiemba
Meter 37123456789
Receipt EVG123456789
Units 21.60KWH

Token 6332 6974 5027 6435 1234

Cost TZS6441.97
Total TZS55000
Timebased amount 38640.00
eSign

Mie ndio huwasiwaelewi kabisaa
 
hydrogen

Maana yake Utaijua
tukimaliza kufunga goli letu la
la mkono mnano
tar 25 october 2015.
 
Last edited by a moderator:
Vijana Kwa wazee tuache kulalamika maamzi Ni kujiandikisha kisha kuwasubiri October 25....

Were crashwise sasa Tanesco na uchaguzi wapi na wapi na isitoshe wantanzani kwa kulalamika hatujambo. Maana hata huyo aliyenunua alipaswa kuuliza kwanza kwa wausika wa nsoshugulikia maswala ya Luku then spate majibu kisha ndo atoe lawama kama kweli kaibiwa. Tusipende kulaumu bila sababu.
 
Hydrogen Je umeuliza kwa uongozi Wa Tanesco kitengo cha Luku kwanini imekuwa hivyo au ndo kawaida yetu wantanzania kulalamika bila kufatilia kwanini imekuwa vile. Fatilia kwanza uone tatizo nini naikiwezekana wapigie Simu utapata msjibu sahii kuliko kuleta mjadala humu usio weza kukusaidia kitu zaidi ya kulaumu tu. Kama hauna nenda ofisi ya Tanesco iliyokaribu nawe na hiyo risti yako uliyo nunulia watakusaidia
 
VAT 18%? REA? EWURA? Au ulidhani makato ni service charge tu?

Nilidhani ni service charge tu. Ndo,maana nikasema anaefaham atujuze
Basi nadhani Tanzania ndo ina gharama kubwa za umeme ukanda huu
 
Back
Top Bottom