Chaliifrancisco
JF-Expert Member
- Jan 17, 2015
- 26,532
- 81,261
Katika pita pita zangu hapa JF na mitandao mingine naona watu wanashangilia sana Magufuli kuagwa kwa nyomi ya watu.
Kuna wengine wana "spam" nyuzi za wengine kwa picha za kujirudia rudia zikionyesha idadi kubwa ya watu waliojitokeza tokea jana mpaka leo katika uwanja wa Uhuru na barabarani kumuaga Hayati John Magufuli. Mfano mama D
Wengine wamefungua nyuzi kabisa kusifia mafuriko katika kumuaga Rais Magufuli. Mfano Nyani Ngabu
Shida yangu sio Hayati Magufuli kuagwa na watu wengi. Tatizo ni kuwa je bado Watanzania hatutaki kuelewa uhalisia wa hali ilivyo kuhusu janga la dunia nzima la covid-19?
Je sisi Tanzania ni nani mpaka tupuuze kwa kiasi hiki? Je hakuna watu wanaougua Corona Tanzania? Hakuna wanaokufa kwa corona?Tukificha tunamkomoa nani?
Hii mikusanyiko sio jambo la kushangilia kwa mtu yeyote anaejielewa.
Tunahitaji reality check. Tunahitaji kukumbushwa hali halisi ilivyo.