Watanzania tunahitaji nini hasa!!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tunahitaji nini hasa!!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by firstcollina, Oct 2, 2010.

 1. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hakika katika hali ya kawaida, hakuna nchi iliyojitosheleza kwa kila kitu katika ulimwengu huu. Kila nchi ina mapumbufu au mambo ambayo hayajakaa sawa katika kuishibisha ile mihimili ya kimtazamo na kiitikadi katika nchi husika. Jambo hili ndilo ambalo mara nyingi huibua hisia za pande fulani kuona kuwa ni wao ni bora zaidi kuliko upande mwingine hivyo kuanzisha michakato mizito ya kisiasa ili kuhakikisha sera zao zinashika hatamu.

  Mambo haya hutokea baada ya mijadala mizito ya chini kwa chini yenye lengo la kuhoji uhalali wa jambo fulani au taratibu fulani na ndipo jamii nzima hujikuta ikiwa katika mahitaji fulani na hivyo kuwa na kauli moja au mbili tofauti juu ya kile kinachohitajika kwa wakati huo husika.

  Hivi tukisimama katika hali halisi ya nchi yetu Tanzania. Ni nini ambacho watanzania tunakihitaji kwa dhati.

  1. Je, ni mapenzi au ushabiki tu waliokuwa nao watanzania juu chama fulani, ndiyo yatuamulie nani apewe ridhaa ya kuongoza nchi?
  2. Je, ni sera dhabiti zenye kutekelezeka ndizo zitusukume katika kuamua nani apewe hatamu ya uongozi wa taifa letu.
  3. Je, ni ushupavu na ubora wa kiongozi mmoja mmoja ndio utuamulie nani ashike madaraka? au
  4. Tuangalie nini zaidi ili kupata ubora stahiki wa kitaifa?
  Naombeni tuchangie ili tupeane ufahamu juu ya nini hasa watanzania tunahitaji kwa wakati huu wakuamua hatima ya siasa ya nchi yetu.
   
Loading...