Watanzania tunahitaji kuamka usingizini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tunahitaji kuamka usingizini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nginda, Nov 7, 2011.

 1. nginda

  nginda JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nijiuliza kila kukicha?

  Je, Tanzania nia nchi iliyo na rasilimali nyingi kama inavyoelezewa? Kama hivyo basi, vilevile Tanznia tunajivunia utajiri wa upumbavu kwa kutoweza kuzitumia hizo rasiliamali, lakini tunajivunia utajiri wa viongozi mbumbumbu pengine zaidi kuliko wote duniani.

  hii ni nchi tajiri, lakini tangu tunapata uhuru migawo haiishi.
  1. Wakati wa awamu ya ya kwanza tulikuwa na mgawo wa sukari, unga, mchele na hata bia
  2. tumeenda awamu ya pili tukaanza mfululizo wa kushuka thamani ya shilingi
  3. awamu ya tatu walau migawo ilipungua, lakini ukaanza mfumuko wa ufisadi
  4. Awamu ya tatu, ndo kwanza najuta kuishi katika awamu hii - tumerudi kwenye mgawo wa sukari, umeme, maji na sasa ni mafuta (nishati). Kwa kipindi kifupi tumeshuhudia shilingi ya tanzania ikiporomoka kutoka 1us $ kwa Tsh 1100/- na sasa ni Tsh. 1800/-. halafu viongozi haohao kama mazuzu wanasimama kwenye majukwaa na kujivunia kukua kwa uchumi tanzana. Ni tanzania ipi? Au ni Tanzania ya mafisadi ndio inayokuwa kiuchumi. Leo ni siku ya tatu hata ukitembea utaona wazi vyombo vya moto havipo barabarani.
  Ningeshauri kuwa, kama historia na geografia zinafundiswa, basi vijana waelimishwe na uwezo wa uelewa wa viongozi wao. Sioni sababu ya kufundiswa historia ya chifu mangungu na upumbavu wao ili hali tanzania imekuwa na machifu mangungu kibao. kwa nini wasiandikiwe historia? nina mashaka kuwa kama watanzania tutaendelea hivi, basi kuna laana ambayo inatupasa tutubu kwa Mungu.
   
Loading...