Watanzania tunadanganywa sana na viongozi wetu

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari ya wakati huu

Napenda kuchukua nafasi hii kuzungumzia kitu kidogo kimuonekano lakini ni kikubwa sana kwa kukifikiria kwa kina.

Kitu chenyewe ni ukweli kutoka kwa viongozi wetu, nahisi Tanzania ndio nchi pekee ambayo viongozi wetu wamezidi kutudanganya kuliko viongozi wengine.

RAIS
*Ukifuatilia hotuba yake ya kufunga mwaka akasema nchi inaakiba ya $6253B baadaye wakakanusha wakasema ni $6253M lakini Rais huyo huyo aliwahi kusema miezi 6 nyuma akiba ni $4765B je hiyo pesa imepungua au?

WAZIRI MKUU
*Huyu nae ndio kabisaaa ameshatudanganya sana kwenye mambo yafuatayo
-Hali ya Afya ya Magufuli wakati ule
-Tarehe rasmi ya reli ya kisasa kuanza kazi
-Idadi ya ajira zilizotolewa na serikali

MAWAZIRI
*Hapa ndio kabisaa nchi ina mawaziri wa hovyo na waongo kupindukia katika wizara karibu zote waongo hapa ukianza na Mwigulu Nchemba, Gwajima, Kabudi, Makamba na wengine wametudanganya mambo mengi sana
Kama:-chanjo, Tozo za miamala, mahusiano ya kimataifa na vitu kama hivyo

WABUNGE
*Hapa wale watu wa jimbo la Kawe nawasalimu kwa jina la jamuhuri. Hapo sijajua yake majimbi mengine ambayo nyie mnajua mlidanganywa nini na wabunge wenu.

WAKUU WA TAASISI NA IDARA MBALIMBALI
*Huku nako kumeoza uongo ndio unakopikwa na kuleta taswira mbaya na mkanganyiko na sintofahamu kwa wananchi.
Hapa ndio kuna mifano ya hatari na kuhuzunisha ambayo inawashangaza wengi

Ufike wakati sasa watanzania tujitambua na tukemee haya mambo kwa kuhoji bila woga na vificho kuhoji kwa njia yoyote ile ili mradi ujumbe ufike.
Bila ya uwepo wa viongozi wakweli na wawazi maendeleo tutayasikia nchi jirani tu maana ukweli huweka mtu huru.

Maendeleo hayana chama
 
Pesa za Covid tunaambiwa zinajenga madarasa. Tozo hali kadhalika tunafahamishwa zinajenga madarasa.

Watuonee huruma hata kidogo.
Najiuliza kwanini hatuambiwi wanakusanya kiasi gani cha tozo kila mwezi na zinatumika vipi?
 
Mkishakuwa na taifa la viongozi waongo,basi hilo taifa Mungu Baba Muumba amelipa kisogo.
Uongo ni ushetani.
Baba wa uongo ni shetani.
Wanaopenda uongo ni watoto wa shetani.
 
Dah, kiongozi umechelewa sana kugundua ukweli, kwa ufupi nchii hii inaongozwa kwa propaganda kwa asilimia kubwa mno, pole kwa kuchelewa kugundua.

Na hiyo ndio sababu atuendelei kwani uongo umezidi.
 
wanachojua tu ni kuvimba na kunyanyua mabega kwenye mavietiiiiiiii yaliyonunuliwa kwa kodi zetu

hakuna anaefikiria kuwa mzalendo wao ni ubinafsi na matumbo yao tu

nchi ngumu hii
 
Huyo wazir mkuu ndio bure kabisa

Amekuwa msemaji mkuu wa Mungu 😁😁:

IMG_20220103_133404_149.jpg
 
Back
Top Bottom