nyanga kante
Member
- Jan 7, 2017
- 36
- 34
....
Ndio maana nimesema, Wapinzani wengi ni wazee wa kukurupuka. ONA kama huyu Ameandika ujinga gani hapa. Hivi hamuelewi nyie UKAWA?Hivi na wewe mpinzani? Mpinzani gani ana avatar ya ccm??
Ndukiiiii
Wakati unalalama fikiria pia tumejengwa kwa misingi ya vyama,wazo kufanana akitoa Lissu na Mwakyembe,lile la Lissu litapigwa na la Mwakyembe litakubaliwa.Unakumbuka teuzi za DED kauli za rais. Kwa hiyo wewe unalalamikia matokeo badala ya visababishiKweli sasa nimejua, Wengi tuliopo katika mtandao huu wa Jamii forum hatujielewi. Nilikuwa nashangaa hivi kweli watu wawe wanapinga tu hata Jambo Jema? Nimeamini baada ya kugundua kuwa wengi hufuata upepo tu bila kujielewa.
Leo hii Mh Rais wetu alisafiri kwenda huko Ethiopia lakini wengine wameanza kubeza safari hiyo kwa kutoa Comments zosizo na Tija kwa Tanzania na Watanzania kwa ujumla. Kweli hata Mheshimiwa Rais wetu akipitia hapa kwa jamii forum atatamani kweli mitandao Ifungwe mara moja. Yaani inasikitisha sana pale mtu anaropoka tu kila linalokuja kichwani mwake.
Wale ambao hawajielewi watasababisha uongozi wa Ukurasa huu wawe mashakani. Kama Mmiliki wa mtandao huu alikamatwa kwaajili ya Wanajamii ambao hawajielewi kabisa. Naomba tujitahidi kujirekebisha jamani. Kwenye Jema tufanye wema. Sio Jambo Akifanya Lowassa au Mbowe au Tundu Lissu na wengine kibao wa Upinzani ndio tunakubaali kuliko Jambo kubwa lifanywalo na mkubwa wa nchi hii.
Au wale Tanzagizani Wengi wao wapo huku?
Ole wenu tuone tena maneno yenu ya kejeli kwa nchi yetu hii tukufu.