MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Hivi kweli jamani mtu anatengeza ARVs fake, anasambaza kwa maelfu ya Wanzania wanaoishi na VVU wanakunywa wakidhani ni dawa za kuwaongezea maisha! Is this serious? Hivi tunaelewa kasi ya ongezeko Virusi kwa mwili wa mwathirika asiyetumia dawa? Ni Watanzania Wangapi wamepoteza maisha kwa kutumia kutumia hizo ARVs zilizothibitika kua ni fake?
Hivi hili suala lingetokea kwenye nchi kama ya China au kwa majirani pale Rwanda hawa watu wangeendelea kuranda mitaani kweli? tena wengine viongozi?
Inaumiza inaumiza inaumiza mno. Hata kama Rais atumbue majipu lakini moja lakini hayawezi kufanana na haya majipu ya ARVs fake kamwe.
Sijui hii kesi imefikia wapi mpaka sasa, Sidhani kama kuna watu wameguswa na hili na kuumia zaidi ya wale ndugu waliopoteza ndugu zao kwa matumizi ya ARVS fake.
Hivi huyu mtanzania aliyeenda akakaa na kufikiria kutengeneza ARVs fake alifikiria nini? Huyu mtu anaamini kwamba kuna Mungu kweli? Anatengeneza unga sijui ni wa mihogo au mahindi akiaminisha watu kua ARVS kweli?
Kwakweli vyombo vyetu vya dola juu ya hili kuona wahusika wamatembea mitaani haviwatendei haki Watanzania.