Vifo Mabomu ya Mbagala, Mgomo wa Madaktari, ARVs na Cloxacillin Fake - Waziri hajiuzulu, kwanini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vifo Mabomu ya Mbagala, Mgomo wa Madaktari, ARVs na Cloxacillin Fake - Waziri hajiuzulu, kwanini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Oct 26, 2012.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hivi waziri Mwinyi, unataka wangapi wafe chini ya wizara unazoziongoza ndipo uwajibike?

  Milipuko ya mbagala iliua watu, ukasema kamwe hujiuzulu

  Ulipoteuliwa kama waziri wa afya, ukasema utahakikisha migomo haipo tena kwenye wizara hiyo, lakini madaktari wakagoma, watu wakafa, na hukuona sababu ya kuwajibika.

  Mara zikaingia dawa feki za ARVs, wanaoishi na virusi vya ukimwi wakafa, ukaendelea kufurahia viyoyozi vya ofisini bila hata kushtuka, unakuja kwa waandishi wa habari kwamba umefunga kiwanda kumbe ni hadaa hata barua hujawaandikia na bado wanaendelea kutengeneza dawa za kuua watu. Kwa nini lakini?

  Na sasa zimeingia dawa feki za aina ya cloxacilline, tena kupitia MSD, watu wanakufa hili sijalisikia hata ukilisemea, maana halijakushtua. Likushtue kwa lipi, kwani wanaokufa ni binadamu, au wanakuhusu.

  Hawa wanaokufa wangekuwa dada zako, wajomba zako, wakwe zako, kweli ungeendelea kufurahia hiyo ofisi, hivi huzioni roho za watu wanaokufa chini ya wizara unazoziongoza zikizunguka ofisini kwako na zikuogofye na kuacha ofisi. Au ni kweli serikali hii ya awamu ya nne ni kweli inatoa watanzania kafaraiendelee kutawala?

  Waziri Mwinyi, wafe wangapi uwajibike?
   
 2. a

  adolay JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,586
  Likes Received: 3,064
  Trophy Points: 280
  Suala la uwajibikaji hutegemea sana nan yupo ikulu, kwanini yupo ikulu na anamtumikia nani anapokuwa pale ikulu.

  Sio lengo langu kuijadili hoja hii kwa kina, lakini kama waziri hawezi kujiuzuru basi huwajibishwa na aliyemteua, lakini nani afanye hivyo? Kikwete au......

  Tunaongozwa na serikali ya kifalme, ambao kwao siku zile za giza alipokufa mfalme alizikwa na mtu mwingine aliekuwahai kutokea jamii za walalahoi, Na kinachofanyika hivisasa ni yaleyale isipokuwa utaratibu kidogo umegeuka. Wao katika familia za ufalme feki za akina mwinyi, makamba, kikwete, mkapa, kawawa, nk - wakiugua hutibiwa nje, wanapohitaji elimu bora huenda nje, wanapohitaji kucheki afya zao huenda inje ya inchi na hata mavazi hufanya shopping zao nje ya inchi.

  Kwa mtazamo huo, jamii za walala hoi kufa kwa mabom, dawa feki, afya duni haina hasara wala maumivu yoyote kwa hawa wafalme feki.

  Hawa ndio watawala wetu wamevembewa madaraka na kufa kwa wanainchi kwa uzembe na udhaifu wa kiuntendaji sio tatizo kwao.

  Lakini wanasahau kitu kimoja, wanainchi hufikia kikomo cha uvumilivu, mfano ni kama Tunisia, Libya, Syria ivorycoast etc.
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kweli mkuu na kupeana uongozi kiushkaji, hamuwezi kuwajibishana
   
 4. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  yaani huyu hussein hamnaga kitu ni bora mwinyi mdogo mb wa EA.
   
 5. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu kapotolo, you talked very sense..ila nadhani at times mawaziri na viongozi wengine wa serikali hutuchukulia(wananchi) jinsi vile ambavyo tunajichukulia,
  Mf.Tunajiona sisi(wananchi) ni dispensable..kwa vile jinsi tunavyoweka mkazo/msisitizo katika mambo ya msingi, mfano Uhai..ambalo linagusa katika athari iliyotokana na matatizo(Janga) yaliuoikumba nchi yetu.

  Na wengi wetu, huwa tunaona hata kama makosa yatendeke kwa namna gani bado tuko radhi kumwacha kiongozi fulani aendelee, "eti,ngoja tu amalize muda wake"
  Ofcourse atamaliza muda wake lakini, at times hadi anamaliza muda wake watu wachache ambao walikuwa na chachu ya kisimamia jambo hawatakuwepo(kutikuwa hai) kwa uzembe ambao unafanyika.

  Nadhani, attitude yetu inapaswa kubadilika hasa katika mambo yanayogusa UHAI wa binadamu.
   
 6. a

  adolay JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,586
  Likes Received: 3,064
  Trophy Points: 280
  Kupeana madaraka, Mkuu umesema jambo muhim sana.

  Kikwete
  |
  Mama salma kikwete
  |
  Ridhiwani Kikwete
  |
  .....Kikwete - Hussen Mwinyi - January makamba- Adamu Malima - .....Kawawa.....Mnauye...... Mwantum mahiza...Hawa ghasia...Zakhia megji....said mwema.....vick kamata....nk

  Ndugu, mashemji na nyumba ndogo.jumlisha na muungano wa mafisadi.........hiyo ndiyo serikali ya Kikwete.

  Huwezi kuwa na utawala wa sheria na uwajikaji kwa mtazamo huo! nani atawawajibisha hawa katika mtiriko wa uongozi wa kifalme? Hapo ndipo kilipo kiburi cha akina Malima kutembea na mashine gun, Ridhiwan kuwa fisadi mkubwa na hata huyo mwinyi kuboronga kila wizara anakohamishiwa.
   
 7. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Dr mwinyi hakufanya intership! Hajawahi kutibu! Anapewa ulaji ili kulipa fadhila! ikumbukwe kuwa mzee ruksa ndiye aliyemtoa JK kutoka nachingwea kumleta hapa mjini na kumpa shavu la unaibu waziri!
   
Loading...