Wosia kwa watanzania na wapiga kura wote-maisha baada ya uchaguzi mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wosia kwa watanzania na wapiga kura wote-maisha baada ya uchaguzi mkuu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mkombozi, Oct 4, 2010.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Naomba nitoe wosia wangu na waraka huu kwa watanzania wote. Mi nimeshirikisana katika kupiga kura kwa awamu mbali mbali na sijawahi kutoa waosia wa kuwaasa watanzania wenzangu.

  Ninaomba kuwajulisha watanzania kua wakati huu mabadiliko ni muhimu sana hasa kwa safu za uongozi wa nchi hususani urais, ubunge na udiwani. Miaka mitano iliyopita 2000 hadi 2005, tumeshuhudia maisha ya kimaskini uliokithiri na mateso makubwa ya kimaisha. Katika report ya Maendeleo ya Millennium, Millennium Development Goal (MDG) iliyochapishwa kwenye gazeti la The East African toleo la tarehe 20-26 mwezi wa 9 kwenye ukurasa wa 4 hadi 6 inaonesha Tanzania imefanya vibaya sana. Kuna vigezo Vinane vya MDG

  1. Halving Poverty by 2015 (eradicate extreme poverty and hunger)
  2. Universal Primary Education
  3. Gender Parity (gender equality and empower women)
  4. Access to health and Combating HIV/Aidis, Malaria, tuberculosis
  5. Child health (reduce child mortality)
  6. Maternal Health (improve)
  7. Environment sustainability
  8. Global Partnership for development.

  Tanzania kwa ujumla imefanya vibaya sana isipokua kwenye kigezo cha uandikisha watoto shule ya msingi, hiki kipengele ndicho kimeipatia Tanzania credit bila kuzingatia ubora wa elimu. Vipengele vingine vyote imefanya vibaya sana kwa Mujibu wa the East African toleo la tarehe 20-26 September 2010.

  Kwa misingi hii, tunahitaji mabadiliko ya kweli ya mfumo wa siasa na fikra ili tuweze kulikomboa Taifa hili. Kwa mtazamo wangu safari hii watu wanapaswa kubadilia na kutoogopa mabadiliko. Asiyekubali mabadiliko basi, ni kuendelea kuukumbatia umaskini uliokithiri. Kupiga kura ni kumpa dhamana kiongozi kwa lengo la kukuletea maendeleo na kuboresha uwajibikaji wa viongozi na wananch kwa ujumla

  Rasilimali Za Tanzania

  Nchi hii ina rasilimali nyingi sana kuliko hata nchi za ulaya. Ila miaka takribanio 50 ya uhuru badi sehemu kubwa ya watu ni masikini wa kutupwa. Rasilimali hizi ni lazima ziwe na mtu thabiti wa kuzisimamia vizuri. Tusiwe na fikra za kuchagua chama, tuangalie mtu mwenye uwezo wa kubadilisha Taifa la Tanzania kua la neema. Mwenye ndia ya dhati na ukimtanzama usoni uone kweli anafaa kukuletea maendeleo na sio blabla za kila siku

  Kwa kuanzia nchi ina madini mengi kama Ulanya, Tanzanite, Makaa ya Mawe, Uranium, Gase, Almasi, Dhahabu, Chumvi, Magadi, Bati, chokaa, n.k. Chii hii ina mabonde na mito mingi isiyokauka mwaka mzima kama vile Rufiji, Pangani, Ruvuma, Kagera, Ruaha mkuu na mingine mingi. Nchi hii ina mbunga na hifadhi nyingi sana za wanyama kama vile Mikumi, Serengeti, Ngorongoro, Serengeti, Kilimanjaro, Ruaha n.k. Nchi hii ina maziwa mengi ya maji baridi kama Victoria la pili kwa ukubwa duniani, Tanganyika lenye kina kirefu zaidi duniani na lenye dagaa wazuri, Rukwa lenye mamba wengi zaidi, Nyasa, Manyara maji moto, Eyasi, na mengine madogo madogo. Chi hii ina mlima mrefu Africa, Kilimanjaro. Nchi hii ina Bahari ya hindi ukanda mzima wa pwani. Nchi hii ina ardi kubwa na yenye rutuba kwaajili ya kilimo, Nchi hii imejaliwa hali ya hewa nzuri mimea kustawi (tropical and mediterenian). Nchi hii ina rasilimali watu wengi wenye uwezo wa hali ya juu na fani mbali mbali. Nchi hii ina wawekezaji na walipa kodi wengi.

  Huduma Mbali Mbali

  Afya

  Inasikitisha sana, mpaka sasa nchi yenye rasilimali nyingi na ina zaidi ya miaka 49 ya uhuru bado wagonjwa wanalala chini wodini. Cha msingi sii vizuri sana kuahidi hospitali nyingi za Rufaa bila kuboresha kwenza mazingira ya hospitali zilizopo. Compaign ya kua na kituo cha afya kila kata ni nzuri lakini pia ni bora zaidi kuporesha huduma kwa vituo na hospitali zilizopo kwanza. Kuna maana gani kua na idadi kubwa ya hospitali zenye utendaji mbovu? Tuzingatie ubora kwanza. Ukishaona hospitali zinazokwepwa na viongozi kutibiwa basi ujue ubora wake una mashaka. Tuwe na hospitali bora kwa wahudumu, ward za waginjwa, huduma madaktari, madawa na vinginevyo. Ili kufanikisha haya tunahitaji kiongozi mwenye dhamira ya dhati, na ukimtazama usoni aoneshe hivyo. Wengine utendaji wao umeuona na unajua unaridhisha au la. Kwa hiyo kura yako ndio kuinuka kwako kimaisha au kuangamia kabisa. Chagua mwenyewe je uendelee kulala chini wardini, kukosa dawa, huduma mbovu au neema.


  Elimu

  Maendeleo yeyote huanzia kwenye elimu. Tunashukuru mungu Tanzania kua na shule za kutosha ila bado kuna changamoto kubwa sana. Sipingi kua na shule kila kata bali tuangalie ubora wake. Ni Shule nyingi bado wanafunzi wanakaa chini karne hii ya science na technology. Zipo shule hazina maabara, walimu wa kutosha, umeme, vyoo, maji n.k. Tusijisifie kwa kua na shule nyingi za kata, bali tujisifie kua na ubora wa kutosha. Elimu bora sasa imekua ni ya matajiri wenye uwezo wa kupeleka watoto wao academia. Sasa hivi kuna shirikisho la Africa Mashariki, kutakua na ushindani mkubwa kwenye soko la ajira, watakaoweza kushindana ni watoto wa matajiri

  Leo hii shule za nyingi za serikali hazina ubora wa kushindana na shule binafsi. Kwa nini shule binafsi wafanye vizuri zaidi kuliko shule za serikali? Tunahitaji kiongozi mwenye dhamira ya dhati mwenye kutoa elimu ya bure na elimu ya lazima kua kidato cha sita. Leo hii mtoto anamaliza shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 14, haajiriki popote kwani hana elimu ya kutosha na pia hajatimiza miaka 18. Tunamwacha mtoto huyu aingie mitaani kuongeza indadi ya wapiga roba au kabali usiku.

  Elimu ya juu isitolewe kwa matabaka, wote wenye sifa ya kupata mikopo wapewe mikopo kwa 100%. Tanzania ni chi mojawapo inayopinga ubaguzi lakini sielewi kwa nini kuwe na ubaguzi wa mikopo ya elimu ya juu? Nina amini matumizi ya serikali yakizingatia vipao mbele elimu bure na mikopo itapatikana.

  Mitaala ya elimu pia siiach bule, inahitaji kurekebishwa kuwe na masomo ya ufundi na gani mbali mbali kuanzia shule ya msingi. Hii itaanza kumjengea mtoto uwezo wa kujiajiri na sio kuajiriwa.

  Usafiri

  Ni kiungo Muhimu cha uchumi, ila inaniuma sana kwa nini bado miundombinu ni mibovu. Wananchi wanaotumia reli ya kati walitaabika sana kwa serikali kushindwa kuboresha reli na badala yake hudidimia kila kukicha. Usafiri huu hautaji nyuvu kuwekeza bali ni kiongozi mwenye dhamira ya dhati. Nashangaa reli ya kaskasini nayo imekufa. Dar es Salaam kuna nyinga nyingi sana za Reli kwa nini usafiri wa treni usifufuliwe ili kuondoa tatizo la foleni? Jibu unalo kwenye kura yako uajiri mtu wa kukuletwa maendeleo au kudidimiza usafiri wa reli.

  Barabara nazo ni finyu sana mijini na pia vijijini hazipitiki wakati wa vyua. Kura yako ndio jawapo la tatizo la usafiri

  Kama hutafanya mabadiliko tegemea maisha magumu zaidi kuliko kipidi chochote kile ila tusingependa pia baada ya kupiga kura yako uanze kulalamkia au endelee kulalamika wakati mfumo wa maisha umeuchagua mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yeyote na ukiwa na akili timamu. Kwa hiyo jibu la maisha yako miaka 5 iyayo unayo mwenyewe. Uchagua kuishi kama ulikotoka au neema na uwajibikaji wenye leongo la kuondoa umaskini.

  Wanaoishi Dar es Salaam na baadhi ya miji mingine tegemea kua na haya yafuatayo kama hutaamua kutumia kwa usahihi kura yako. Miaka 5 baada ya uchaguzi ni mingi mno kama hatutafanya chaguo sahihi, tushuhudie safari nyingi za nje za viongozi wetu, kama hatutafanya chaguo sahihi, tushuhudie mfumuko wa bei. Kule Dar es Slaam. Unga ulikua 350 mwaka 2005 sasa ni Shs 800 ongezeko la 129%, kwa uwiano huo tutegemee bei ya unga kufikia TShs 1,830 mwaka 2015. Mchele ulikua TShs 600 2005, sasa ni TShs 1,500 (ongezeko la 150%), tutegemee bei kufikia TShs 3,750, Sukari ilikua TShs 600 sasa ni TShs 1,800-1,600 ongezeko la 200%, tutegemee bei kufikia Tshs 5,400. Mkate TShs 250 hadi TShs 700 ongezeko la 180%, tutegemee bei kufika TShs 1,960, Maharage TShs 500 hadi Sasa TShs 1,400 ongezeko la 180%, tutegemee bei kufika TShs 3,920, Nyama ya Ngombe TShs 2,000 hadi sasa TShs 4000-5,000 ongezeko la 150%, tutegemee bei kufika TShs 12,500. Bei ya dola 1 ya Marekani ilikua TShs 1,100 sasa ni TShs 1,520 ongezeko la 39% tegemea bei kufika TShs 2,113


  Katiba

  Hebu fikiria katiba inavyompa Rais madaraka Makubwa, anateua mawaziri, manaibu waziri, kamatibu wa wizara, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurungezi wa mashirika ya uma, wakuu wa vyuo vikuu, mabalozi, majaji, jaji mkuu, mwasheria mkuu, tume ya uchaguzi, msajili wa vyama vya siasa,mkurugenzi wa TAKUKURU, Governor and Deputy Governors wa bank kuu, Amiri jeshi mkuu, mkaguzi wa serikali, Commissioner wa TRA. Haya ni madaraka makubw sana. Je TAKUKURU ikiwa inaripori kwa bunge, Je TUME huru na Msajili wa vyama vinayochaguliwa na muungano Wa vyama vya siasa ili view huru. Mimi siongezi kitu, we kura yako ndio mwambuzi hapo. Pia inampa kinga Rais ili usiweze kuhoji kama ametimiza na kufanya kazi yake ipasavyo. Na mambo mengi ya kikatiba

  Tubadilike, na saa ya ukombozi ni sasa, ahadi nyingi zisikutishe swala ni kuangalia zinatekelezeka? Je maisha bora kwa kila mtanzania yamepatikaka? Au ndio maana safari hii kauli mbiu hii haisikiki tena? Tujaribu pia kutafaka nyanya zote haki za wafanyakazi, watoto wa mitaani, miundombinu, huduma mbali mbali, usafirishaji, uvuvi, kilimo, mifugo vyote hivi vinahitaji mtu mwenye uwezo wa kuvisimamia kwa dhati na kuleta uwajibikaji kwa serikali na wananchi kwa ujumla. Lengo sio kuletwea vitu kama bajaji n.k Lengo ni kuwezeshwa kuweza kuvinunua wenyewe.

  Changua moja kati ya neema au maisha ambayo umeyazoea. Kura yako ina thamani kubwa sana, ya kukubadilisha maisha yako. Yapo mambo mengi sana ila zaidi ya yote ni kubadilika. Usichagua chama, angalia mtu wa kuweza kulikomboa kutoka katika umaskini uliokithiri.

  KAZI KWAKO, KURA YAKO NDIO UKOMBOZI WAKO

  Wenu Mlipakodi

  ILA KURA YAKO SIIHITAJI, KWA SHARTI LA KUONGEZEWA MSHAHARA
   
Loading...