Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,504
- 113,618
Wanabodi,
Tanzania ni yetu sote, kwa Watanzania wote kuwa na haki sawa, hadhi sawa, na tunawajibu wa pamoja wa kulijenga taifa letu, individually na collectively kwa kuwa wazalendo wa kweli wa taifa letu, hivyo kunapotokea ukosoaji wowote, ukosoaji huu, ufanyike kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa.
Haya ni miongoni mwa yalizosungumzwa leo kwenye kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds TV, toka kwa watangazaji, Hasan Ngoma na Ceaser, na kiukweli huyu mtangazaji Ceaser, ni mzuri sana kwa kujenga hoja, nimependa kwa jinsi alivyo construct arjument ya uzalendo, na kui drive home kwa mfono mzuri sana, kuashiria pamoja na tofauti zetu za kiitikadi, kisiasa, na kivyama, lakini linapokuja suala la maslahi ya taifa, Watanzania tuwe wamoja.
Wakatumia speeches za Lipumba na John Cheyo za jana pale Ikulu.
Declaration of Interest
Kwanza naomba kukiri, mimi ni miongoni mwa watu ambao nilikuwa siisikilizi Clouds Radio wala kuangalia Clouds TV, kwa sababu niliiona kama ni media ya vijana, hivyo kuwahesabu they are not serious, ila mara moja moja nilikuwa nasikiliza Jahazi nikiwa kwenye gari, nikawaona kama ni wapayukaji na ni watu wa kujipendekeza pendekeza sana hadi kuonekana kama kujikomba kwa CCM, hivyo nikawapotezea, ila nilipokuja kujua kuwa kumbe Magufuli anaangalia 360, ndipo na mimi nikaanza kuwaangalia, nikakuta they are fine, haswa Baby Kabae. Hivyo siku hizi naangalia Clouds.Kama Magufuli Anaangalia Clouds TV na Kuipongeza, Kunatuma ...
Naunga Mkono Hoja ya Uzalendo na Kukosoa Kwa Hoja Kwa Nia Njema ya Kujenga.
Japo hoja hii imetolewa na hawa vijana wadogo, lakini mimi, pamoja na ukongwe wangu, naunga mkono hoja hii ya tutofautiane kiitikadi, tukosoane kwa hoja, kwa lengo la kujenga na sio kubomoa, lakini linapokuja suala la maslahi ya taifa, tutangulize uzalendo kwa kuweka pembeni tofauti zetu, na kuungana kwa pamoja, tuwe wamoja kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, yaani Tanzania kwanza, mengine yote yatafuatia.
Uzalendo ni Nini, na Mzalendo ni Nani?
Uzalendo ni ile hali ya kuwa na moyo wa upendo wa dhati kwa taifa lako, hadi kuwa tayari kulifia, hivyo mzalendo ni mtu yoyote anayefanya jambo lolote la kizalendo, mfano mzuri ni kwenye hii vita ya kupigania rasmilimali mali upande wa rasilimali madini, watu kama kina Tundu Lissu, Zitto Kabwe, JJ Mnyika, ni watu waliyeonyesha uzalendo mkubwa zaidi kuliko Watanzania wengi, wakati huo Magufuli akiwa ni sehemu ya waliolifikisha taifa hili hapa, akiwa ni waziri, wakati haya madudu yote yakipitishwa ndani ya baraza la mawaziri, lakini leo kwa vile Magufuli ndio amayafumua, kwa sasa sifa na pongezi zote za uzalendo wa kweli, zinakwenda kwa rais Magufuli kwa vile amefanya mambo makubwa ya kuonekanika. Thamani halisi ya uzalendo, sio kufanya mambo ya kizalendo ya kuonekanika, bali kuna wazalendo kibao silent heroes, wanaofanya mambo makubwa kabisa yasionekana, hawataji popote, hawapongezwi, hawapewi vyeti, lakini ni wazalendo kuliko hawa wanaoonekana, na mmoja wa wazalendo hawa ni huu mtandao wa JF.
Jee Kumkosoa Rais Magufuli ni Uzalendo au ni Usaliti, hivyo Uzalendo ni Kumsifia Tuu?.
Katika kusifia uzalendo, pia imejengwa dhana ya usaliti, kuwa wale wote wanaomkosoa rais Magufuli ni wasaliti, au wale wote wanaopingana nae ni wazaliti, hivyo tafsiri ya uzalendo ni wale tuu wanaosifia rais, hata akifanya makosa, wao watasifu tuu na kupiga makofi. Ukweli ni kuwa hakuna ubaya wowote kumkosoa rais Magufuli, kama ukosoaji huo unafanyika kwa nia njema kwa lengo la kujenga kwa kumsaidia, huku ukifanywa kwa lugha ya staha yaani constructive criciticism na sio kumbomoa, kumtukana, kumdhihaki au kumdhalilisha kwa lugha ya machukizo. Kumkosoa rais Magufuli sio kukosa uzalendo, wala sio usaliti, tena unaweza kukuta, wale wanaomkosoa rais ndio wazalendo wa kweli na wanamsaidia kuliko wale wanaomsifia na kumuimbia tuu nyimbo za sifa, sjangwe na mapambio, kwa sababu rais Magufuli naye, is only human, can make mistake.
Jee Wanaokosoa Magufuli, Wanamkosoa Kwa Chuki Kwa Vile Hawampendi, Au Wanampenda Sana Ndio Maana Wanamkosoa?.
Kuna makundi makuu matatu ya Wakosoaji wa Rais Magufuli, kuna kundi la the politicians, kuna kundi la hatters, na kundi la realists, truthful na perfectionists
Maendeleo ya kweli Tanzania, yataletwa na wazalendo wa kweli wa nchi hii, kwa kutumia kanuni ya kusema ukweli daima, hata rais akikosea, akosolewe kwa staha kwa kuambiwa ukweli, na yeye kama rais wetu, auchukue ukosoaji wetu humu very positively, kama mimi nilivyo wahi kushauri humu, kuhusu madini, rais mkapa alidanganywa, akadanganyika, rais Kikwete, amedanganywa, akadanganyika, kwenye hili na makinikia rais Magufuli naye, kaisha danganywa, na kuna kila dalili, ameisha danganyika, na hapa nawaomba sana wale wote wenye mapenzi mema na taifa hili, mpigie mstari maneno yangu haya, kuwa Tukikubali kukipokea hiki kishika uchumba cha Acacia cha dola milioni 300, na tukaruhusu mchanga wa makinikia ya dhahabu kusafirishwa, bila kujua kilichomo, then this will be a done deal, forget about Trilioni 450!.Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli ...
Vipi maoni yako, uzalendo ni kusifu tuu na kukosoa ni usaliti, au uzalendo wa kweli ni kuusema ukweli daima, no matter unauma kiasi gani?
Paskali
Rejea kuhusu ukosoaji
Mwito Kwa Wana JamiiForums Kuhusu Ukosoaji wa Rais Magufuli ...
Rais Magufuli na serikali yake wakosolewe kwa hoja sio kwa viroja ...
Tusilalamike Tuu, Kulaumu na Kulaani Kila Kitu, Kwenye Mazuri ...
Rais Magufuli Akifanya Mazuri, Apongezwe: Hotuba Yake Kuzima ...
Wana JF, Jee Tuisaidie Serikali Yetu Inaposhindwa Au Tusubiri ...
2017 JF Tubadilike, Tupunguze Kuwa "Barking Dogs, Seldom Bite ...
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye ...
Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet ...
Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa ...

- The Politicians -Hawa ni wale ambao Magufuli hakuwa mtu wao, hawa wana mtu wao aliyeshindwa, hivyo hawa, kila kitu ambacho Magufuli, wao watakosoa tuu sio ili kumsaidia, but for political gain. Wengi wa kundi hili ni wapinzani, hii inapelekea kila anayemkosoa rais Magufuli, kunyooshewa kidole kuwa ni mpinzani, kazi yao ni kupinga tuu. Ndiko huku kuiga marufuku mikutano ya kisiasa kulliko ibukia.
- Haters- Hili ni kundi la watu wenye chuki tuu kumhusu Magufuli, au chuki kwa CCM, wao kazi yao ni kukosoa tuu tena kwa kutumia lugha mbaya na hata kutukana, hawa ni hate preachers, ambao wana kwenda hadi personal issues na kuingilia his right to privacy, lengo lao ni Magufuli achukiwe. Hii imepelekea kila anayemkosoa rais Magufuli, kuonekana ana chuki na Magufuli, hii inamfanya rais Magufuli kupokea ukoaji huu kwa chuki na huwajibu kwa maneno makali, na ndiko huku neon fyokofyoko lilikoibukia.
- Realists, truthful na perfectionists-Hawa ni wakosoaji ambao ni wa kweli, wanamkosoa kwa makosa ya ukweli, hivyo ukosoaji wao ni wa hoja za kweli, unaofanywa kwa nia njema ili kumsaidia, na nyingi ya ukosoaji huu hufanywa constructively yakiwemo mapendekezo ya a way forward, hawa wanamtaka rais Magufuli awe perfect, wanamkosoa sio kwa sababu wanamchukia, bali wanamkosoa kwa sababu wanampenda, kama baba anavyomrudi mwanaye, au mti wa matunda unavyopopolewa. hivyo anapofanya mazuri, watu hawa humpongeza, kwenye kundi hili, ndimo mtoa mada alimo.