Watanzania tuipende nchi yetu, tuweke kando ushabiki na itikadi zetu pembeni kwa ajili ya nchi yetu

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,745
5,446
Watanzania tuipende nchi yetu, tuweke kando ushabiki na itikadi zetu pembeni kwa ajili ya nchi yetu; huu ndio uzalendo.

Wamarekani wanao msemo -'America First ". Rais mmoja wa nchi alipata kusema: "For my country, my people and myself" yaani kwa ajili ya nchi yangu, watu wangu na mimi mwenyewe.

Hotuba ya Krismas ya Askofu Mkuu wa FGBFC, Zakaria Kokobe haikupewa uzito mkubwa na vyombo vyetu vya habari , labda imeonekana ina maneno makali dhidi ya Rais wetu mpendwa ambaye serikali yake kupitia Wizara ya Habari, imekuwa "katili mno " dhidi ya vyombo vya habari vinavyoonekana 'kuisakama serikali' na kukiuka maadili ya vyombo vya habari.

Wana CCM wa kweli wanajua kwa miongoni mwa ahadi 10 za mwanachama tangu enzi za TANU hadi sasa CCM ni ile isemayo : "nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko. "

Leo wamejaa wanachama feki wengi CCM na vyama vyote vya siasa ambao hukanusha ukweli kwa uongo na kugeuza kila wasilolipenda kuwa propaganda na kubeza hata yale yanaonekana kuwa ya muhimu kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.

Naomba niwaalike Great Thinkers tu wa JF ambao kwao itikadi na ushabiki wa vyama vyao ni kitu cha baadaye baada maslahi ya nchi.

Karibuni tujadili na kusema waziwazi bila kuuma maneno, kutikisa masikio wala kupepesa macho kuwa ktk hotuba Askofu Kakobe ina mapungufu gani?

CC: Pohamba, Lizaboni, pasco, joka kuu, Mag3, @Nguluvi, BAK, Nyani Ngabu, @Mwanakjiji, mshana, Gezaulole, Kimweri, etc.
 
Watanzania tunaipenda sana nchi yetu kuliko hawa wanasiasa hasa wa CCM wanaotumia madaraka yao vibaya sababu wao ni chama dola wana jeshi,police,magereza na idara nyingine za usalama ni tiifu kwa chama dola vyombo hivi vinatumika kukandamiza watanzania kwa kupiga,kuteka na hata kuua sasa ni nani atakayeipenda Tanzania kwa aliyepo nje ya CCM??
 
Back
Top Bottom