Watanzania tufanye nini ili tuweze kuwa taifa lenye furaha zaidi duniani?

wanzagitalewa

Senior Member
Jan 25, 2018
128
84
Wiki iliyopita, Umoja wa Mataifa ulitoa taaifa ya mwaka kuonyesha nchi zipi ambazo wananchi wake wana furaha zaidi duniani (UN Annual Happiness Report). Taarifa hii ambayo ni ya kitafiti hutazama sababu za furaha na huzuni - na nini ambacho nchi zinaweza kufanya kuongeza furaha ya wananchi wake.

Taarifa hiyo ilionyesha kuwa Finland ndiyo nchi ambayo watu wake wana furaha zaidi duniani. Lakini pia ikaonyesha kuwa Tanzania ni mojawapo ya mataifa ambayo wananchi wake hawana furaha.

Kudadvua zaidi ni kwamba Tanzania imewekwa karibu na chini kabisa katika orodha hiyo, tuko namba 153 kati ya nchi 156, ikimaanisha ni moja ya nchi ambazo watu wake wana huzuni na machungu zaidi duniani.

Tukienda mbele zaidi orodha hiyo inaamaanisha hata Haiti, nchi ambayo inasuasua kwa kupigwa na vimbunga bahari watu wake wana furaha kuliko Watanzania. Hata Yemen iko juu yetu, nchi ambayo imekuwa katika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa mwaka wa nne sasa. Tuko chini hata ya Syria, nchi ambayo sote twafahamu kuwa iko katika vita visivyoisha ikiwepo waasi ambao wamekamata sehemu kubwa ya nchi hiyo.

Tanzania iko mkiani, pamoja na Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Burundi. Tunaweza kusema hii ni orodha itokanayo na utafiti wa kibepari na ina mushkeli, lakini ingetusifia na kutuweka juu wala tusingeipiga vijembe. Hii ina maana kwamba orodha hii lazima itupe Watanzania makini tafakuri ya namna fulani. Sisi ni taifa lenye amani, kwa nini tuambiwe tuna huzuni au kwa nini tusiwe na furaha kama tunayo amani?

Tumefikaje hapa?

Taarifa ya kiwango cha furaha kwa kila nchi duniani (The Happiness Report) hutazama nyanja zote za maisha. Hupima vitu kama hasira na maumivu. Hizo ni changamoto kubwa ambazo zitahitaji muda mrefu kutatua lakini zipo baadhi ya changamoto ambazo tunaweza kuanza utatuzi wake hata kesho. Hizi ni vita dhidi ya rushwa na imani ya wananchi kwa serikali na vyombo vya dola.

Tuanze na rushwa. Inatisha kwamba hii ni mojawapo ya vitu ambavyo vinafanya wananchi wasiwe na furaha. Unakumbuka unapokasirika basi likisimamishwa na trafiki ili tu apokee chochote toka kwa dereva? Au unapoendesha gari lako, kila kitu kiko sawa kisha polisi anakusimamisha na kubambikia kosa ili umpe chochote? Lazima unakumbuka, na ni kumbukumbu chungu. Hakuna aliye salama na athari za rushwa, uwe tajiri au masikini.
Rushwa inashusha mapato ya serikali. Hii ina maanisha kwamba fedha ambayo serikali itakuwa nayo kwa ajili ya maeneo kama elimu na afya inapungua. Pili, rushwa inakimbiza wawekezaji wawe wa ndani au wa nje. Serikali haiwezi kufanya kila kitu peke yake na hutegemea wawekezaji wa ndani na nje kuleta teknolojia, mitaji, ubunifu, na ajira. Rushwa pia huondoa uaminifu. Inapunguza kuaminiana hasa kwa taasisi za serikali. Imani ya wananchi kwa serikali na taasisi zake ni kipimo kingine cha furaha kwa nchi.

Tujenge imani upya

Rushwa inaumiza. Inakera. Inakufanya ujiulize maswali ya nini maana ya serikali na kuchukia serikali na taasisi zake. Rushwa inakufanya upoteze imani na dola. Kama kila kitu kinahitaji ukinunue, hata haki yako, lazima utapoteza imani.

Utafiti wa Afrobarometer unaonyesha kuwa theluthi moja ya Watanzania hawaziamini mahakama. Kumbuka mamia ya watu walivyokimbilia kwa RC Makonda kuomba utatuzi wa kesi zao za ardhi badala ya mahakamani. Ukisikia sababu zao hasa ardhi, utaona namna ambayo matajiri wakubwa wametumia pesa kuyumbisha mfumo wa mahakama kutoa haki.

Asilimia 70 ya Watanzania wanasema kwamba wanahofia usalama wao kama watatoa taarifa kuhusu rushwa.
Kutatua hali kama hii, Wananchi wanahitaji hatua chanya toka serikalini kuondoa rushwa na kusafisha mahakama zetu. Hii ndiyo njia kubwa ya kuleta mabadiliko tunayotaka katika utoaji haki. Hii ianze na kesi kubwa kama za uhujumu uchumi ambazo zinapiga mark-time kwenye mahakama zetu kila uchao.
Hatua hizi hazitatufanya tuwe sawa na Finland ghafla lakini zitawapa Watanzania imani zaidi kwamba serikali yao inaweza kutatua matatizo yao kama vile rushwa na utoaji haki, na panapo majaliwa, baada ya miaka kadhaa mbele na sisi tukawa taifa lenye furaha zaidi duniani.

Nyaronyo Talewa
Mara, Tanzania (Safarini Dodoma)
wanzagi.talewa@gmail.com
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2018-03-22 at 18.48.00.jpeg
    WhatsApp Image 2018-03-22 at 18.48.00.jpeg
    34.9 KB · Views: 39
Nafikiri wizara ya habari utamaduni Sana'a na michezo itengewe fungu waweze kuandaa wachekeahaji wakutosha ili watuchekeshe tuwe na furaha.
Kama hivi mara pap Mzee majuto huyu hapa lazima ucheke tu.
Viwanda kwanza.
 
Kabla ya kulaumu setikali ya awamu ya tano lazima tuangalie trend ilikuAje serikali zilizopita,,,lakini CCM must go
 
Huwezi kuwa na amani.
Haki zako inaporwa unaona na wanausalama wanamtetea mporaji. Mahospitalini hongo ni km imehalalishwa bila pesa hakuna tiba. Mahakamani, hakimu anakueleza wazi tu kuwa hatima ya kesi yako iko ndani ya mfuko wako. Shuleni km hukumfanyia kitu mwalimu mwenye ushawishi ujue mwanao anaenda kufeli tu. Unaenda tanesco unataka kuunganishwa umeme unafuata taratibu zooote lakini mwishowe hawaji kuunga bila kumhonga meneja na fundi mkuu, unakubali kutoa hongo kwakuwa unashida ya umeme.unaungwa lakini luku yako hawatasajili ili urudi tena kuwapigia magoti na kutoa kachai kidogo, unatoa... Unarudi eneo la biashara unawakuta tra wanakufungia biashara, unaenda kuonana nao, watakuambia kodi kubwa ambayo hailingani na biashara yako, unaanza kuwapigia magoti, na kuwaminyia kitu mkononi mwao ili tu wakuruhusu ulipe kodi halali...... Hapo utapata amani wapi?
 
Hata furaha kidogo tuliyokuwa nayo CCM nao wanaitaka,kufikia mwaka kesho tutakuwa na furaha 0-
 
Watupe zile noah zetu walizotuahidi then tutakua na furaha isiyo na kifani.
 
Tufute vyama vyote vya upinzani.

Tuongozwe na rahisi wa milele.

Tujenge viwanda vingi vya vyerehani.
 
Tanzania inaharibiwa na wafuasi wa Chadema muda wote ni kulialia tu mitandaoni
 
Back
Top Bottom