Watanzania tuamke tuache kulala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania tuamke tuache kulala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bemg, Jun 28, 2012.

 1. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Watanzania wenye upendo wa dhati na nchi hii wanaumia mno wanapoona na kusikia matukio ya kutisha katika nchi yetu yanayofanywa na binadamu wenye roho ya kishetani.Matukio ya kuteka na kuua watu yanazidi kushamiri, wizi wawaziwazi wa mali za uuma ndo usiseme, wananchi kuteseka kwa kukosa huduma muhimu imekuwa ni kawaida.Watanzania wote wakwe kwa waume ni wakati wa kuamka sasa, maana mchana umeendelea sana na karibia itakuwa usiku.Ni wakati kwa makanisa ya Mungu aliyehai kusimama na kuomba toba kwa ajili ya taifa letu, viongozi wetu wa serikali, ardhi yetu, na tuombe atuhurumie na kuliponya taifa letu na matukio ya ajabu.Mauaji yanayofanywa na watanzania wenzetu ambao roho zao zimetawaliwa na shetani aliye baba wa wawauaji wote, wasiopenda kuambiwa ukweli, wanaojipenda wenyewe na kutohurumia mamilioni ya watanzania wanaoteseka na maisha magumu.

  Mungu asikie sala zenu na eneza ujumbe huu kwa kila mtu aweze kuamka na kuwa nakazi ya kuombea nchi yetu ili Bwana wa majeshi aweze kuiponya na kuturudishia miaka tuliyopoteza kwa kutomjua Mungu na kuwa na hofu na jina lake.Ni ombi langu watanzania wapendane wote bila kujali itikadi ya vyama, dini , kabila, kipato,nk

  Mungu ibariki Tanzania na watu :peace:
   
 2. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndio maana sisi tukaanzisha JUMUIA YA UAMSHO,,, ili kuwaamsha walio lala..... Umeona enh!??
   
 3. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ukweli unauma taifa letu linazama kwa sababu ya watu wake wengi wamekosa maarifa wanajuhudi binasfi za kujifanya hawaoni mabaya wanayoyatenda au kutendwa.Kwa moyo wangu wote naomba tanzania na watu wake waokolewe ili waweze kufahamu maarifa ya kutembea katika njia ya maendeleo ambayo tumeandaliwa na Mungu wetu.
   
 4. bemg

  bemg JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,706
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Uamsho ni jumuia nzuri kama itajikita kuhamasisha mafundisho ya allah na watu wayashike huku wakidumu katika upendo na watu wote.
   
Loading...