Naomba tuwekane sawa kuhusu mambo mawili: 1. alichosema Dr. Slaa kuhusu ushiriki wa makada wa CCM katika kikao kilchofanyika La Kairo Hotel
2. Hoja za wanaokanusha.
Alichosema Dr. Slaa:
Kwanza, (kama nitakosea nipo radhi kurekebiswa): nadhani Dr. Slaa alizungumzia kilichokuwa kwenye waraka ulioandikwa na M. W. Kabwe tarehe 18/10/2010. Huo waraka ulielekezwa kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi - majimbo ya Nyamagana na Ilemela.
Waraka ulitaja kikao cha tarehe 16/10/2010 ukitaja washiriki wa kikao kwamba walikuwa watu 30 lakini baadhi yao ni:
- Mh. J.K. kikwete
- Mh. Rostam Azizi
- Mh. Edward Lowasa
- Ndugu Christopher Gachuma
- Ridhwani Kikwete
Pili, Waraka huo ulizungumzia maagizo 7:
a) Kupunguza na kutobandika idadi kubwa ya vijana waliojiandikisha kupiga kura.
b) Kuchelewa kubandika majina ya wapiga kura ( yabandikwe 24/10/2010 badala ya 20/10/20100
c) kuhakikisha kuwepo vituo hewa (3-4)
d) Kutoa taarifa kwa vyombo vya dola (Polisi) kutovumilia vikundi vya watu baada ya kupiga kura.
e) kuchelewa kutangaza matokeo.
f) kupata wasimamizi wa vituo na wasaidizi , na makarani ambao ni makada wa Chama
cha Mapinduzi
g) kuhakikisha Green Guard inatekeleza wajibu wao wa maelekezo yatolewayo
Waraka ulihitimisha kuwa utekelezaji zoezi uwe wa siri na wa umakini wa hali ya juu sana.
Kwa hiyo, kumlaumu Dr. Slaa kuwa ni mwongo ni uzandiki wa hali ya juu kwani yeye alitaja kilichoandikwa kwenye barua ambayo inawataja kuwa walikuwa kwenye kikao huko Mwanza tarehe 16/10/2010. Hivyo, wanakanusha wakitaka kujenga hoja wangesema kuwa Kabwe hajawahi kuandika barua ya namna hiyo bali iliyopo ni ya kughushiwa. Hivyo, kutozungumzia kilichoandikwa kwenye barua na badala yake Dr. Slaa anashutumiwa huko ni kutuona sisi kuwa ni mabwege, hilo hatulikubali.
Hoja zinazokanusha:
Kwanza hadi sasa nimesikia waliokanusha taarifa za Dr. Slaa ni Ridhwani Kikwete, Rostam Azizi na Edward Lowasa.
Ridhwani anasema tarehe iliyotajwa na Dr. Slaa hakuwa kule Mwanza. sikumbuki Ridhwani alitaja tarehe ipi ambapo hakuwa Mwanza. Hali kadhalika sijui Rostam alitaja tarehe ipi ambayo yeye hakuwepo Mwanza. Lowasa yeye alijitetea kuwa tarehe 19/10/2010 alikuwa anaendelea na Kampeni hivyo hakuwa Mwanza. Pamoja na kuwa hazaelezea kampeni yake iliisha saa ngapi na kikao cha Mwanza kilianza saa ngapi na hivyo kutuondoa kwenye uwezekano wa yeye kufika Mwanza siku hiyo, lakini tatizo kubwa lipo katika tarehe anayotaja kama ndiyo tarehe ya kikao cha Mwanza na tarehe ya barua ya Kabwe. Tarehe hizo hazina uhusiano kabisa na kimsingi hakuna anachokanusha bali ni kubwabwaja maneno.
Kwa kweli naomba vitu viwili viwekwe sawa, yaani hoja ya Dr. Slaa na barua ya Kabwe. Vinginevyo mtu atajitetea kwa kumshutumu Dr. Slaa kwa kitu ambacho hakusema na kumwacha aliyesema. Hivyo ni vizuri kujua alichosema Dr. Slaa na kile alichodai Dr. Slaa kuwa kiliandikwa na Kabwe. Bahati nzuri Kabwe aliripotiwa na vyombo vya habari akikiri kuwa ile sahihi katika barua ni ya kwake ila hakuiandika.