Maandamano Mbeya, Mwanza umoja wetu umesikika

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,879
35,888
1. Mbeya Mwanza kumeonyesha - Umoja wetu utamng'oa nyoka pangoni:



2. Kwamba Slaa anasema:
_______
"Katiba iliyopo ilitengenezwa na watu wasiozidi 20 Kwa siku chache sana. Haipo sababu yoyote leo Samia na serikali yake kutuambia muda hautoshi.

Tunataka kumwambia Samia katiba ni mali ya watanzania.
Samia yuko pale kama rais ni kwa mujibu wa katiba; lazima aiheshimu na kuitii katiba ya jamhuri ya Mwungano wa Tanzania.

Samia ni mtumishi wetu; ni mwajiriwa wetu. Haijawahi kutokea duniani mwajiriwa akaandika mkataba wa ajira yake. Ni lazima watanzania tumpe sisi barua ya ajira."


Anamaliza Slaa kwa sababu ya muda, kwa kusema:

"Tuungane na Chadema kwa nguvu zote na tutaungana pamoja na asasi na wale wote wanaopigania kupunguza gharama za maisha, na wale wote wanaopambana tupate katiba mpya ......

People's ... !!!

----------

3. Maneno mwiba kabisa toka kwake Dr. Slaa kwa ule upande mwingine na chawa wao.

4. Kwa hakika tunataka katiba mpya sasa!
 
Ungeweka summary ya alichokiongea Dr Slaa,

Sababu Watz wengi uwezo wa kutizama video hawana sababu ya kupanda bundles za internate🙏

Mkuu nimeirejea na kuya paraphrase maneno yake kama ulivyopendekeza
 
Slaa ni Askofu aliyeasi, na Balozi aliyeasi..... ataaminika kwa lipi?
 
Ngumu sn maana wasomi ndiyo wajinga kuliko haa wasiosoma
Exactly mkuu hasa hawa middle class, ni wapumbavu mno, maadam wao wanasomesha watoto wao kwenye hivi vi English medium school, watoto wao wanaenda Choo twice a day ,wanajifanya wameyatoa maisha na hawaelewi yanayowakuta wananchi wa huku ngwinde,mbimbi, tagamenda au kamachumu
 
Slaa ni Askofu aliyeasi, na Balozi aliyeasi..... ataaminika kwa lipi?

"Maneno mwiba kabisa toka kwake Dr. Slaa kwa ule upande mwingine na chawa wao."

Kwani wewe ni mmoja wao?
 
Back
Top Bottom