Watanzania sasa kuiongoza TRL.................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania sasa kuiongoza TRL..................

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Dec 23, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  TRL sasa kuongozwa na Watanzania asilimia 100
  • Waziri mpya wa uchukuzi aponda menejimenti ya Rites

  na Betty Kangonga


  [​IMG] WAZIRI wa Uchukuzi, Omary Nundu, ameahidi kuishauri serikali kufanya haraka mchakato wa kulirejesha Shirika la Reli Nchini (TRL) chini uongozi wa wazalendo ili waweze kulifufua.
  Shirika hilo lilikuwa likiongozwa kwa ubia na menejimenti ya kampuni ya Rites ya India iliyokuwa na hisa ya asilimia 51 na serikali ya Tanzania iliyokuwa na hisa ya asilimia 49.
  Akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana, Nundu alisema inasikitisha kuona shirika hilo linazidi kudorora kila kukicha huku likionekana kama halipo.
  "Mmekuwa wavumilivu na wachapakazi hata kwa mazingira yaliyopo maana kwa muonekano wa wazi shirika kama halipo maaana hatuwezi kuwa na safari moja tu kwa wiki kwa shirika kama hili!" alishangaa.
  Alisema makubaliano ya kuvunjwa kwa mkataba yalikwishafanyika na serikali inaendelea kuweka mikakati ya kumalizana na wabia ambapo muda si mrefu kampuni itaendeshwa na Watanzania kwa asilimia 100.
  Waziri Nundu alisikitishwa na hatua inayofanywa na menejimenti ya Rites ya kuendelea kukusanya mapato huku serikali ikiambulia patupu.
  "Ninashangaa kama kweli jambo hili linafanywa na kuwa kimya, sisi ni wazalendo….hii ni nchi yetu tuwe wazi na kueleza yale yanayotendeka," alisema.
  Alisema ni muhimu kuangalia mikataba inayofanywa na serikali na kuichunguza kwa upana ili ikitokea mwaka wa kwanza kampuni iliyoingia ubia inazalisha kwa hasara basi kuwepo na njia nyepesi na za haraka za kuchukua.
  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU), Sylvester Rwegasira, alisema kuwa alichokifanya Waziri Nundu ni kutoa ahadi na yatathibitishwa hayo baada ya kero hizo kuondolewa.
  "Tutaendelea kupiga kelele na muelewe kuwa kila tunapoamka shirika hili linaendelea kufa hasa ukiangalia suala hili la fedha ambazo wenzetu wanazikusanya na zinaingia katika mifuko yao. Tunaomba serikali ichukue hatua za haraka sana," alisema.
  Hata hivyo, wakitoa maswali yao kwa Waziri Nundu, Elizabeth Msemo wa Idara ya Masoko alisema hali ya mabehewa inatisha jambo linaloonyesha kuwa Watanzania wako katika kipindi cha ukoloni maana abiria wamefikia hatua ya kufa ndani ya mabehewa kutokana na kukosa hewa.
  Aidha, waziri huyo alikaribishwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali likiwemo la "Hapa kama Ivory Coast, menejimenti 2 moja ya Rites na nyingine ya serikali je hii sawa?"
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]
  Ilikofika TRL ni matokeo ya ufisadi

  [​IMG]

  [​IMG] MIONGONI mwa mashirika na makampuni ya serikali yaliyokufa kwa sababu za rushwa na kukosa uzalendo kwa taifa, ni Shirika la Reli Tanzania (TRC).
  Kulegalega hadi kufa kwa kampuni hii muhimu kwa usafiri wa kwenda bara kuliongezeka baada ya serikali kupitia viongozi wake wasio makini, kuingia mkataba wa miaka 25 na Kampuni ya Rites kutoka India.
  Mkataba huo wa asilimia 49 ya wazawa na asilimia 51 ya wawekezaji wasio na uwezo ulifanyika chini ya Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC), ulisainiwa Septemba 3 mwaka 2007 na kuanza kazi Oktoba mosi mwaka huo huo.
  Mkataba huo, umeliingiza taifa katika hasara inayosababisha vifo vya watu ndani ya mabehewa, kukosekana kwa usafiri, mapato na ajira za wengi huku ukiwatukanisha watawala na nchi kwa ujumla.
  Jana, Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu, alistaajabu ya Musa alipofanya ziara kukagua shughuli za TRL pale alipoelezwa kwamba hivi sasa shirika linafanya safari moja tu kwa kutumia mabehewa machache yanayojaa abiria kupita uwezo wake na kusababisha vifo huku miundombinu ya reli hiyo iliyojengwa miaka ya 1800 ikishindwa kukarabatiwa kisasa.
  Maelezo ya wafanyakazi hayo yalibainisha kuwepo kwa kifo cha msafiri mmoja kwenye kila safari kwa msongamano. Walimweleza waziri huyo kwamba uwezo wa behewa moja ni abiria 80 lakini kutokana na uchache wake hulazimika kuchukua abiria 120.
  Kama hiyo haitoshi, serikali inasema iko kwenye hatua za mwisho za kuuvunja mkataba huo uliodumu kwa miaka mitatu sasa wakati awali mwisho wa menejimenti ya wawekezaji hao ni Oktoba 2010, lakini hadi sasa bado wapo kazini na wanaendelea kukusanya mapato yote huku serikali ikiendelea kuwataabisha wananchi wake.
  Nundu kama watangulizi wake, ametoa ahadi ya wazalendo kuchukua asilimia 100 ya hisa za TRL, tunatamani kuyaamini maneno yake japo hofu yetu na Watanzania wengine ni lini hasa wawekezaji hao wataondoka.
  Tunamkumbusha waziri huyo kwamba kilio cha wengi ni kilio cha Mungu, uharaka wa kuwaondoa wawekezaji hao usipofanyika taifa litazidi kuangamia na uchumi utadorora.
  Tunadiriki kusema kwa kinywa kipana kabisa kwamba mkataba wa miaka 25 kati ya Rite na TRC uliozalisha TRL, una dalili za rushwa ndani yake. Ni mkataba usiofaa kwa kuwa walioitwa wawekezaji wenye uwezo walishindwa kazi katika kipindi cha kisichozidi mwaka mmoja!
   
Loading...