Watanzania ni wanafiki tusiojitambua

Nwaigwe

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
1,053
913
Wakati Kikwete akiwa rais kila mtu aliongea mpaka mtoto mdogo.

Wapo waliosema 'Eti mpaka mchanga wetu wa dhahabu unatoroshwa nchini, mara ohh tunaachiwa maandaki, mara hoo mafisadi na ufisadi umezidi nchi hii" Kila mtu ataweza kukuorodhoshea mabaya kibao yaliyotokea kwenye miaka 10 ya utawala uliopita.

Chadema kupitia kwa Mnyika walimsema vibaya sana Kikwete eti tumefika hapa tulipo kwa UDHAIFU wa Kikwete.

Haya tukapata rais kwanza wakasema waliibiwa kura japo mawakala wao walikuwepo kwenye vituo na kwenye kata ambao walisaini kuyakubali. Matokeo CCM ilipata wabunge wengi zaidi ya 170 kitu ambacho hata Rais alipatikana kwa wingi huohuo hasa kwenye majimbo hayo kilichoshinda chama.

Anyway siko huko sana, Cha ajabu baada ya Magufuli kuonyesha msuli wake wa kazi wakaanza kuona wivu na kudai wameibiwa sera? seriously uibiwe sera kwani wee nani ? kwani kuna sehemu iliyoandikwa haya ni ya CHADEMA ulimwenguni na hao chadema waliyatoa wapi?

CHADEMA walitegemea Magufuli atafanya vibaya ili waendelee kusema ...tumefikishwa hapa kwa sababu ya udhaifu wa Magufuli.... ila wapi wakakuta ni mwanaume anayesimamia sheria.

Haikutosha, wameanzisha propaganda kwamba eti Magufuli ni dikteta, ana utawala wa kiimla, mabavu ..e.t.c

Jana kwenye MWANANCHI, Mbowe kasema ...eti watu wanafukuzwa ovyo bila utaratibu makazini..real? Mbowe? acha unafiki....

Kwanza watu hawafukuzwi bila utaratibu kama ulivyofukuza madiwani wako wa chama wa Arusha kipindi kile....kama ulivyomfukuza Zitto bila hata haya... hata kumwogopa Mungu kwamba ni Zitto na Slaa ndio waliowaingizia wakina Lissu, Mnyika e.tc bungeni kipindi ambacho CHADEMA haijulikani. Acha unafiki Mbowe wewe ndiwe ulifukuza fukuza bila kufuata utaratibu refer ya zito utaelewa tuu.

Msitufanye mtaji wenu wa kisiasa tuna macho tunaona kinachofanywa na Rais unataka asifanye ili kwenye uchaguzi useme CCM hakifai tuchague CHADEMA?

Mnajaribu kueneza propaganda kwenye mitandao ya jamii ila sisi wenye akili ya kuchambua hamtuambii kitu zipo sheria ndizo zinazofuatwa. Unaposema Rais dikteta ni kwa sababu kafuata sheria? Magufuli ni mtu wa Mungu anafuata haki that's all.

Roho zenu mbaya zitatufikisha pabaya hamwoni hata vibaya kutufanya mitaji yenu.

Watu wa Libya ile dhambi waliyofanya inawatafuna mpaka. Toka wamuue kwa kumdhalilisha Rais wao hawana amani miji imegeuzwa magofu... Rais aliyewaletea maji kwenye ile nchi ya jangwa na huduma zote na hata kuwatolea mahari wale wanaotaka kuoa bado mitandao ya kijamii ilikuwa gear ya mafarakano machochezi kama haya.

Wapo watu walioshikwa vibaya na Magufuli... labda ndugu zao, baba zao, wapenzi wao wako jela au wameachishwa kazi, wale wavivu, wenye mibiashara yao isiyolipa kodi wote ROHO ZINAWAUMA. Machadema nayo ndiyo WIVU kabisa unawasumbua hawakutegemea watapata wapi ya kuongea wanaanza ku blow mazuri ya Magufuli....eti tuwaamini wabadilisha gear angani wauza chama hao kwa lipi....wakafilie mbali.

Nasi watanzania tuache unafiki, wakati ambao tulikuwa na uongozi legelege tuliongea sana; sasa tumepata jembe tunaongea... hatuna shukrani haturidhiki ...tusije kuwa kama Libya.

TUACHE UNAFIKI
 
Haya tukapata raisi kwanza wakasema waliibiwa kura japo mawakala wao walikuwepo kwenye vituo na kwenye kata ambao walisaini kuyakubali. matokeo ccm ilipata wabunge wengi zaidi ya 170 kitu ambacho hata raisi alipatikana kwa wingi huohuo hasa kwenye majimbo hayo kilichoshinda chama.

Vipi CHAMA CHENU hakikuwa na mawakala Zenji? Au wote walikuwa likizo? Au walihongwa? MKUKI KWA...................
 
Hoja haina mashiko. Unafiki wa Watanzania wote unaujumuisha kwenye kikundi au makundi ya watu wachache?
 
umenena mkuu,na juzi nimemsikia msigwa eti anasema mama makinda alikuwa spika bora kuliko huyu ndungai,hivi ni kweli?walivyomdharau yule mama eti leo wanatulaghai
Wakati Kikwete akiwa rais kila mtu aliongea mpaka mtoto mdogo.

Wapo waliosema 'Eti mpaka mchanga wetu wa dhahabu unatoroshwa nchini, mara ohh tunaachiwa maandaki, mara hoo mafisadi na ufisadi umezidi nchi hii" Kila mtu ataweza kukuorodhoshea mabaya kibao yaliyotokea kwenye miaka 10 ya utawala uliopita.

Chadema kupitia kwa Mnyika walimsema vibaya sana Kikwete eti tumefika hapa tulipo kwa UDHAIFU wa Kikwete.

Haya tukapata rais kwanza wakasema waliibiwa kura japo mawakala wao walikuwepo kwenye vituo na kwenye kata ambao walisaini kuyakubali. Matokeo CCM ilipata wabunge wengi zaidi ya 170 kitu ambacho hata Rais alipatikana kwa wingi huohuo hasa kwenye majimbo hayo kilichoshinda chama.

Anyway siko huko sana, Cha ajabu baada ya Magufuli kuonyesha msuli wake wa kazi wakaanza kuona wivu na kudai wameibiwa sera? seriously uibiwe sera kwani wee nani ? kwani kuna sehemu iliyoandikwa haya ni ya CHADEMA ulimwenguni na hao chadema waliyatoa wapi?

CHADEMA walitegemea Magufuli atafanya vibaya ili waendelee kusema ...tumefikishwa hapa kwa sababu ya udhaifu wa Magufuli.... ila wapi wakakuta ni mwanaume anayesimamia sheria.

Haikutosha, wameanzisha propaganda kwamba eti Magufuli ni dikteta, ana utawala wa kiimla, mabavu ..e.t.c

Jana kwenye MWANANCHI, Mbowe kasema ...eti watu wanafukuzwa ovyo bila utaratibu makazini..real? Mbowe? acha unafiki....

Kwanza watu hawafukuzwi bila utaratibu kama ulivyofukuza madiwani wako wa chama wa Arusha kipindi kile....kama ulivyomfukuza Zitto bila hata haya... hata kumwogopa Mungu kwamba ni Zitto na Slaa ndio waliowaingizia wakina Lissu, Mnyika e.tc bungeni kipindi ambacho CHADEMA haijulikani. Acha unafiki Mbowe wewe ndiwe ulifukuza fukuza bila kufuata utaratibu refer ya zito utaelewa tuu.

Msitufanye mtaji wenu wa kisiasa tuna macho tunaona kinachofanywa na Rais unataka asifanye ili kwenye uchaguzi useme CCM hakifai tuchague CHADEMA?

Mnajaribu kueneza propaganda kwenye mitandao ya jamii ila sisi wenye akili ya kuchambua hamtuambii kitu zipo sheria ndizo zinazofuatwa. Unaposema Rais dikteta ni kwa sababu kafuata sheria? Magufuli ni mtu wa Mungu anafuata haki that's all.

Roho zenu mbaya zitatufikisha pabaya hamwoni hata vibaya kutufanya mitaji yenu.

Watu wa Libya ile dhambi waliyofanya inawatafuna mpaka. Toka wamuue kwa kumdhalilisha Rais wao hawana amani miji imegeuzwa magofu... Rais aliyewaletea maji kwenye ile nchi ya jangwa na huduma zote na hata kuwatolea mahari wale wanaotaka kuoa bado mitandao ya kijamii ilikuwa gear ya mafarakano machochezi kama haya.

Wapo watu walioshikwa vibaya na Magufuli... labda ndugu zao, baba zao, wapenzi wao wako jela au wameachishwa kazi, wale wavivu, wenye mibiashara yao isiyolipa kodi wote ROHO ZINAWAUMA. Machadema nayo ndiyo WIVU kabisa unawasumbua hawakutegemea watapata wapi ya kuongea wanaanza ku blow mazuri ya Magufuli....eti tuwaamini wabadilisha gear angani wauza chama hao kwa lipi....wakafilie mbali.

Nasi watanzania tuache unafiki, wakati ambao tulikuwa na uongozi legelege tuliongea sana; sasa tumepata jembe tunaongea... hatuna shukrani haturidhiki ...tusije kuwa kama Libya.

TUACHE UNAFIKI
 
Huwezi kuipima kasi ya magufuli kwa sasa kwani akikupita utajiona kama umesimama kumbe na wewe upo kwenye mwendo ,Magufuli ana mzigo mzito wa kuiondoa Tz hapa ilipo kusafisha njia na hata kusema kuiweka demokrasia katika mkondo wake ,tume huru zisiwe za kuwachunguza mafisadi tu bali hata ile ya uchaguzi itabidi aibomowe na kuweka inayokubaluka na vyam vyote kwani hicho ni kipimo cha kuwa anapenda kuona haki inatendeka na yapo mengi ambayo Upinzani unaweza kukamata bango achana na sera za Magufuli za kuwakurupusha wanachama wa CCM wanaijenga serikali yake ,mwisho wa muhula tutapima kwa kuangalia maendeleo ya mtu mmoja mmoja kwa mwaka napata dola ngapi.

yapo mengi na moja kuu ni hii ahadi ya elimu bure ,tayari malalamiko yamekuwa mengi na yameanza kuota ingawa kwa asiejua habari zake na malamiko yake kwa sasa hayapewi kipau mbele ,ila yapo. Sasa huu ni mwanzo pengine na ndivyo ilivyo Mh.raisi ameikuta hazina ipo tupu ,hela inayohiyajika ni kubwa ,ni lazima WaTz tuwe na subira juu ya kupima kasi ya Magufuli.
 
Kuna Wabunge wa upinzani ambao ni maboya tu. Kila atakachosema Mh Mbowe wataitikia "ndiyo". Wengi wao hawajitambui wala kutambua nafasi zao kama Wabunge. Kwao upinzani ni ubishi usio na mshiko kitaifa. Kwao kelele bungeni ndiyo haki yao.

WACHAMBUE WACHUNGUZE WAAMUE WACHUKUE HATUA SAHIHI
 
Huna point tafuta kazi ya kufanya hii ya lumumba huiwezi
 
Kuna Wabunge wa upinzani ambao ni maboya tu. Kila atakachosema Mh Mbowe wataitikia "ndiyo". Wengi wao hawajitambui wala kutambua nafasi zao kama Wabunge. Kwao upinzani ni ubishi usio na mshiko kitaifa. Kwao kelele bungeni ndiyo haki yao.

WACHAMBUE WACHUNGUZE WAAMUE WACHUKUE HATUA SAHIHI
Lakini mi ccm wananishangaza kila linalopelekwa na serikali kwao ni "NDIO" tu.
 
Watz hatujajua ni nini tunataka!! Me naona km akili zetu zipo kwenye transition period!!(kipindi cha mpito)
 
Nwaigwe umeonyesha rangi zako zote at one time. Mnafiki namba moja no wewe mwenyewe kwani kwa jinsi ulivyojieleza ulishiriki kumsema JK vibaya. Kama hukumsema ulimwambia kuwa unasemwa? Umeyapata wapi sasa ya kumlinganisha Jk na JkM? We we ndiye mnafiki na si watanzania. Isitoshe acha uchonganishi wa kitoto wa kuwachonganisha viongozi wetu. Tunawapenda wote.
 
Kumbe kuna watanzania ambao wanajielewa, nakupongeza kabisa kabisa kwa kuandika ukweli , hawa vijana wa bavicha hawajielewi.Kila kitu ni kosa kwao, hawajielewi na hawana mipango.Ila kwao siasa ndio maisha .
 
Yaliyomo moyoni,
Ni hakika tanzania sasa tumempata kiongozi,makini,muadilifu na asiyeyumbishwa na mtu yeyote zaid ya kufuata sheria na taratibu za nchi.naungana na mtoa mada watanzania ingawa sio wte lkn wamo wenye vijitabia kama hizo alizozitaja mtia mada hilo liko waz na ukiona mtu anabisha basi jua huyo ni fisadi asiyependa utawala wa sheria.anachofanya Rais magufuli ndo sisi watanzania wazalendo tunaoipenda nchi yetu tulikuwa tukiisubiri kwa miaka yte.
Angalizo:upinzani ni mzuri sana lkn unakuwa mzuri zaid pale unapokuwa na hoja zenye mashiko ya kuikosoa serikali.naam najua wamewahi kufanya hivo,lkn sasa walipofikia wameishiwa hoja.wanabaki kutafuta namna ya kuwashawishi baadhi ya watanzania wasiokuwa na uelewa na wenye vichwa vya panzi ili serikali hii ya awamu ya tano ionekane hovyo,lkn bahati nzuri wengi wetu tumeelika tuna utashi wa kutosha na maarifa tena wao "wapinzani"ndo walitufumbua macho baadhi yetu kutambua.sasa hiv wanataka kutugeuza kama samaki.wamegonga mwamba kazi lzm ifanyike na utawala wa sheria lzm ufuatwe kama anawagusa kwenye mambo yao watulie wanyolewe tu.msikubali kuyumbishwa,na hawa wanaojiita wapinzani wakati ni ccm b.hawana sera.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom