Watanzania ni walewale na CCM ni ile ile. Je, hakuna mabadiliko ya vizazi?

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Uchaguzi wa ccm umemalizika Dodoma kwa kuwaongezea muda mwenyekiti yaani Rais wa Tanzania na mwenyekiti mwenza Rais wa Zanzibar, Waliopiga kura sio wageni ni wana ccm wale wale na hata waliochaguliwa ni wale wale

Mawazo ya kizazi hiki kipya cha Tanzania ni mawazo ya karne ya ishirini, Karne iliyopitwa na wakati, karne iliyoaminisha Babu na Bibi zetu kuwa idadi kubwa ya watu ndio mafanikio na nguvu kazi ya Taifa

Wana ccm tumemaliza uchaguzi Dodoma cha kushangaza sijaona vijana wenye mawazo mapya, maono mapya na muelekeo mpya, Kumbuka uchaguzi huu umefanyika miaka zaidi ya ishirini tangu karne ya ishirini na moja tulipoianza enzi za Y2K na enzi za kuamini mwisho wa dunia ile miaka ya 1999/2000

Wazee wamekuwa mbogo na wakali Dodoma wakiwarithisha vijana mawazo yale yale na mambo yale yale, Tena ikatamkwa kwa ukali kabisa na kwa kuazimia kabisa kuwa haitegemewi kuona kijana anachukua fomu kutoa mawazo mapya au muelekeo mpya

Mawazo ya vijana kuhusu matatizo ya umeme na maji hayana tofauti na ya wazee wa zamani ambao wamesisitiza Dodoma lazima watanzania wawe na shukrani na adabu kwa maji machafu yenye udongo wanayopatiwa kwa kodi zao, Hata umeme unaozima zima wameulizwa kama kwao kuna umeme au nako unakatika katika

Maelezo ya vijana Dodoma kuhusu bei za bidhaa kupanda ni yale yale ya karne ya ishirini, Karne iliyoaminisha watanzania ukificha chakula ndani basi hakutakuwa na mfumuko wa bei ndani ya mkoa na nchi husika, Cha kushangaza vijana kama wazee wale wale hawajatamka kila mtanzania anatakiwa kuficha gunia ngapi za mchele, mahindi na maharage ndani na ni kwa muda gani waendelee kuficha mahindi, mchele na maharage na wafanye mchezo huo wa karne ya ishirini wa kuficha chakula kwa miaka mingapi

Uchaguzi huu ndani ya chama chetu cha CCM una Funzo moja kubwa sana kuwa njaa haina mkubwa wala mdogo, Njaa inaweza ukafanya lolote na ukafanywa lolote.

Njaa haina heshima wala adabu kwa wazee na vijana, Njaa imewafanya vijana kuwa watumwa wa fikra na mawazo.

Ili tuondokane na watu wale wale na mambo yale yale ni lazima kama Taifa tushughulikie tatizo la njaa ili kuweza kupiga hatua mbali, Bila kutatua tatizo la njaa tegemea hata ifikapo nusu ya karne ya ishirini na moja yaani mwaka 2050 bado vijana wa Y2K watakuwa na mawazo yale yale na watafanya chaguzi zile zile

Tambua kuna aina kuu mbili za njaa

1. Njaa inayoanzia tumboni kuelekea kichwani

2. Njaa inayoanzia kichwani kuelekea tumboni

Kati ya hizi njaa mbili kuna moja yenye unafuu kidogo ingawa zote ni njaa
 
Tambua kuna aina kuu mbili za njaa

1. Njaa inayoanzia tumboni kuelekea kichwani

2. Njaa inayoanzia kichwani kuelekea tumboni

Kati ya hizi njaa mbili kuna moja yenye unafuu kidogo ingawa zote ni njaa
 
Na sasa hivi mawazo hayo ya karne iliyopita ndio yanalindwa na vyombo vya dola kwa kuhakikisha CCM inabaki madarakani kwa shuruti. Kwasasa hofu ya CCM kutoka madarakani ni dhahiri kwani sio chama cha kizazi hiki, ndio maana wanapora uchaguzi kimachomacho.

Kwa sasa chaguzi hazina wapiga kura tena, maana wapiga kura wengi hawaichagui ccm. Hivyo wanachofanya CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola walivyohakikisha wanashikamana navyo, ni kupora uchaguzi kwa ukatali mkubwa. Machafuko pekee yake ndio yatawatoa CCM madarakani.
 
Back
Top Bottom