Watanzania, Ni vigumu Kumsahau Lowassa

Watanzania, Ni vigumu Kumsahau Lowassa

Mleta mada umesahau hata leo hao vijana unaowaona hapo u-dom ni kazi ya Lowasa
Aliwambia wakurugenzi wamashirika ya uma na toa nusu saa anayeona hawezi kutoa hela juu ya mradi huu awe amewasilisha barua ya kujiuzulu mezani kwangu wote wliofyata mpka leo tuna chuo kikubwa yani huyu bwana ni kiongozi acheni tu huyu mimi kwa nchi hii sijaona mtu ambaye anaweza akawa mbadala wake
 
NDIYO UKISHASOMA HAYA HAPA CHINI NI KWELI NI VIGUMU KUMSAHAU LOWASA

LOWASA

Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.
Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alinipigia simu na kusema yafuatayo:
“Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma’. Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!
Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema “Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali”.
Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.
Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa “Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma”. Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa “Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa”!
Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa “Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa” kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; “Kawawa sikumwambia hivyo”! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali.
Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa “Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam”. Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.
Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?.
Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema “Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?”
Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia “NDIO ALINIAMBIA”. Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.
Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa “Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge.
Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?”
Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!
Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.
Angalia tunavyofanya “total transgression of CCM regulations and ethics.” Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri.
Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!!
Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.
Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa “Natural Justice” hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli?
Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao? Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe.Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli? Tukumbuke na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM , katika katiba (ccm) inasema 15 (7) “ kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa…
Watanzania wenzangu haya anayosema Lowasa yanafanana na nukuu niliyoanza nayo? Fikiria nairudia tena “For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes basely upon the belly and not upon the feet!
There is no vile that does cover a man with shame as to be found false and pertifidious” Niharakishe kusema hapa kuwa viumbe vyote ambavyo havikupenda kusema ukweli Mungu aliviadhibu kwa kuvifanya vitembelee matumbo yao milele nyoka wakiwemo! Lowasa, Mwanyika, Hosea na wenzake naomba kama nilivyoanza, tafadhali wasome hiyo nukuu mara kadhaa na waielewe na kuizingatia.
Watanzania wanawashangaa, wanadharau na kuchukizwa na viongozi wasiopenda kusema ukweli kwa maisha magumu waliyo nayo ambayo wao wanawazomea kwa dharau kuwa ni wavivu na wachovu wa kufikiri. Wanasahau kuwa hawa watu wa kawaida ndio wanaozalisha kile kinacholipa mishahara na marupurupu yao.
Kama viongozi wakuu wa CCM, katika hili daima kumbukeni wajibu wenu kwa mujibu wa katiba ya CCM, ibara ya 15 (4) kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania. Onekaneni hivyo kwa vitendo tafadhali. Utaratibu huu wa kusema uongo unadhoofisha amani na utulivu Tanzania.
Hayo niliyasema niko tayari kuyasema bungeni akiwepo Lowasa ikibidi. Hatuwezi kukubali nchi hii kuendelea kuwa na viongozi wa aina hii. WAWE WAKWELI, WASEME UKWELI TU. WANAPOKOSEA HARAKA NA KWA UKWELI NA UNYENYEKEVU WAOMBE RADHI KWENYE VYAMA VYAO, SERIKALINI NA KWA WANANCHI. NI UPUUZI WA HALI YA JUU KUJITETEA OVYO NA KUINGIZA UKABILA ( LOWASSA NA OLE NAIKO) HATA KWA MAKOSA YALIYO DHAHIRI.
Katika mahojiano na TVT Lowassa alikiri kuwa alishindwa kuvunja mkataba wa RICHMOND. Sababu alizitaja. Sawa. Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali, kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma ( Toleo 1994), kifungu F33, makosa yake kiserikali ni haya yafuatayo; 33( xi) omission which is against public interest. 33(xiii) negligence occasioning loss to the employer ( yaani serikali na taifa kwa ujumla). 33( xiv) gross negligence in the performance of duty.
Kama mtendaji mkuu wa shughuli zote nzito za serikali bwana Lowassa hana namna ya kujitetea kwa makosa hayo yaliyodhahiri ambayo TANESCO imeendelea kudhoofishwa na RICHMOND kwa yeye kuogopa kutumia utaalam nje ya wale aliowaamini. Mbona tuna vyuo vikuu, je, aalivitumia kikamilifu? Mbona kwa maswala yasiyo na maslahi ya maana tumezoea sasa kukodi wataalam wa nje?
Kwanini hakujiridhisha katika maeneo yote hayo? Tatizo hili ni kubwa sana maana watanzania sasa wanatozwa viwango vikubwa sana kulipia umeme ikiwa ni pamoja na sehemu za uzalishaji zenye kutumia umeme achilia mbali malipo ya capacity charges? Nani anabisha kuwa kwa huu mkataba wa RICHMOND n.k Bwana Lowassa na Wenzake waliweka sahihi za kifo siyo kwa TANESCO tu bali pia cha kuvuruga maendeleo ya nchi yetu na kuendeleza umasikini?
Katika yote haya ambayo yamesemwa, Bwana Lowassa na wenzake wajue kuwa kama watanzania, we have a compelling moral case for complaining against him.
There is also a compelling case that is in Tanzania’s self interest. Recently many trade agreements already have made the poorest countries worse off. Such agreement already have condemned to death thousands of our people . Corporations of whatever name do strip Tanzania of its natural resources leaving behind a trail of environmental devastation etc. This is done through very poor legal frameworks. Nimuhimu tukawa na viongozi waaminifu, waadilifu na wasema ukweli. Kwa haya yanayotendeka, something is fundamentally wrong with our government.
Kwa kila maamuzi tunayoyafanya mara zote tuzingatie ni kwa maslahi ya nani; yale ya Taifa ni kipaumbele cha kwanza. Tuzingatie matumizi mazuri ya rasilimali zetu daima. Duniani ziko serikali nyingi tu ambazo zimevunja mikataba mibovu. Kwa ziara nyingi ambazo viongozi wetu wanafanya na baada ya wanahabari kupigia kelele RICHMOND, kwanini Lowassa huko nje hakutaka kujifunza namna ya kuvunja mikataba mibovu?
Yaani umahiri wake uliishia mkataba wa maji Dar es salaam na kiwanja cha Mnazi Mmoja? Mikakati yetu ya maendeleo imekuwa haileti tija iliyokusudiwa moja ya sababu ikiwa a flawed vision of development. Successful countries have a broader vision of what development entails and a more comprehensive strategy for bringing it about.
It is very unfortunate that in the majority of developing countries Tanzania included the nation – state has been weakened thoroughly! Haya maamuzi yanayofanywa na viongozi kama Lowassa ndiyo matokeo ya kutojua namna ya kuthibiti na kutumia kwa uangalifu fursa za kitu kinaitwa UTANDAWAZI.
Government that attempt to control capital flows find themselves unable to do so, as individuals find ways of circumventing the regulations. A county may want to raise the minimum wage, but discovers it can’t, because foreign companies operating there will decide to move to a county with lower wages.
Situmeona jinsi waziri Chiligati ( waziri wa kazi wa wakati huo) alivyohenyeshwa na wakubwa – wawekezaji kukataa kulipa kima cha chini hapa Tanzania? Wengine wamepunguza kazi ndugu zetu na sasa ni katika kundi la Machinga! Waziri mkuu wa wakati huo Lowassa alisaidiaje? KIMYA! Dhahiri kinachoonekana hapo ni sense of powerlessness. Kwa kukumbatia matajiri na wakubwa wa nje, kupitia utanzawazi, baadhi ya viongozi wetu kama inavyojidhihirisha kupitia RICHMOND n.k. find their ability to act eroded.
These days it is the order of the day for the electorate to see its government bending before foreigners wenye (mitaji). Day in day out democracy is being systematically undermined. When the electorate shouts through the media etc, no body listens! Wanataka sifa tu.
The electorate feels being thoroughly betrayed. Whether we like it or not, it is perceived, quite rightly, I think the way globalization is currently managed is not consistent with democratic principles. Little weight is given to the concerns and voices of ordinary people and the poor! Kwa kiburi cha wakubwa kutosikia, kutopenda kukosolewa Tanzania inaendelea kubaki masikini. Lowassa na wenzake wangekuwa makini na mahiri katika kusikiliza waandishi wa habari mapema RICHMOND n.k isingetufikisha tulipo sasa ambapo kila siku tunapoteza fedha nyingi.
Tusingekuwa na tume juu ya tume ambazo baadhi tunazibeza kwa kejeli hata kwa kutumia chama (CCM). CCM kweli tunasoma na kuzingatia kwa vitendo wajibu wa mwanachama wa CCM kifungu 15(3) na 15 (4) na 15(7) pamoja na ahadi za mwanachama wa CCM (3) na (4), na (8). Hivi CCM sasa ni mali na jina la mtu; kwamba hivyo mtu akikosolewa hamtaki kuona kakosa na mko tayari chama kife kwa ajili ya mtu mmoja au kundi dogo tu la watu? Nendeni Butiama mtupe majibu tafadhali. Uwezo, busara na nia vyote mnavyo. Ningekuwa Lowassa Butiama nisingeenda. Yeye kwenda huko ni kejeli kwa Baba wa Taifa.
BADO TUTAENDELEA KUWASEMA WENZAO KUHUSU MIKATABA YA HOVYO NA UKWAPUAJI WA RASILIMALI ZA NCHI HII. HOJA YA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR BWANA IDD PANDU HASSAN- “ Lowasa kutostahili kuitwa Waziri mkuu Mstaafu” ni muhimu ikazingatiwa sambamba na utata wa stahili za mafao. Haitoshi kuimba utawala wa sheria na kumbe inapofika kwa wakubwa tunakunja na kunyonga sheria zetu. Sheria ni Msumeno. Someni Pensions Ordinance cap 371 sambamba na kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la (1994) kifungu F53 (d) na (e). Tusiwe na kigugumizi katika hili.Tujifunze yaliyojiri hapo jirani Kenya hivi majuzi.
Namalizia kwa kusema “Tuheshimu na kudumisha kitu UKWELI”. Kwa viongozi, zingatieni na kwa unyenyekevu heshimuni viapo vyenumnapokabidhiwa madaraka. Baba wa Taifa daima katika mkoba wake alibeba Bibilia na Azimio La Arusha.
Nyinyi kwa kipindi hiki kigumu cha ufisadi na kukithiri kwa rushwa na mikataba mibovu; bebeni daima photo-copy za viapo vyenu pamoja na Bibilia au Koran pamoja na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mnazo dini zenu. Sikusikia yeyote akiapa kwa dini za asili kwa Rais au kwa Spika wa Bunge. Nawashukuru watanzania, Mhe. Spika na Waandishi wa habari ambao wamekemea maneno ya Lowasa na wenzake baada ya kikao cha Bunge.
Namshukuru sana Mhe. William H. Shelukindo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kwa kuwasilisha hoja ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza Richmond na shukran maalum nazitoa kwa Dr. Mwakyembe na wajumbe wote walioshughulikia suala la Richmond na kuwasilisha taarifa Bungeni kwa uadilifu mkubwa sana.
Mwisho nawashukuru Watanzania wote na nchi za nje walionipongeza na kunipa moyo kuhusu makala zangu za kukemea ukwepuaji rasilimali za nchi BoT yenye kichwa cha habari “Salaam kwa Mawaziri” Namshukuru Rais Kikwete. Namshukuru pia Mhariri gazeti la Rai namba 748 na 749. Halmashauri kuu ya CCM inayokutana Butiama naitakia mafanikio makubwa katika maazimio watakayofikia . Baada ya hapo muonekane mmedhamiria kutenda kwa kuleta maendeleo yenye kuzingatia uadilifu na uwajibikaji
Viongozi wabovu wawajibishwe tu.
Watanzania wengi leo bado wanamlilia Mwalimu J.K. Nyerere hasa kwa matatizo kama haya ya mikataba mibovu ya Madini, RICHMOND n.k. Wanasema sorry Mwalimu lived ahead of his time. Alituangazia kwa mengi, hakuna wa kututetea leo kwa matatizo yote haya.
Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Afrika
Samwel. H. Kasori
Katibu mstaafu wa J.K.Nyerere
0754 372141
 
Baada ya kuleta ule uchambuzi wa Timu za wagombea, kazi yangu ya pili ilikuwa ni kutembea mitaani kwa wananchi na kudadisi nini hasa wanachotaka na kutarajia katika uchaguzi mkuu wa 2015. Kitu kikubwa nilichojifunza ni kwamba watanzania ni wavumilivu sana na ni wachapakazi sana. La pili ni hili swala la wagombea wa CCM, wananchi bila kusita wamesema wazi kuwa ni vigumu kwa watanzania kumsahau Lowassa, kama mdadisi nilitaka kujua ni kwa nini wanasema hivyo? Majibu yao yalikuwa kama ifuatavyo........

1. Ujenzi Shule za kata
(
Wananchi wanasema): Ni Lowassa huyu huyu aliyesimamia ujenzi wa shule za sekondari za kata Tanzania nzima. Hoja kwamba hazina walimu ni sahihi, lakini lipo swali la kujiuliza lakini kipi bora kutokuwa na vyote viwili, shule na walimu au kuanza kimoja?

Hapa wapo wenye hoja sahihi kabisa kuwa serikali ingeanza na kufundisha walimu kabla ya kujenga shule, lakini walimu hawa hawa iwapo wangehitimu kwa idadi kubwa na kukosa ajira, hoja hii ingegeuzwa na kudaiwa kuwa serikali inapaswa kujenga shule kwanza kabla ya kufundisha walimu. Kwamba Shule zinapokuwepo kasi ya mahitaji ya walimu inakuwa na mashiko (real) badala ya dhahania (imaginary) ila tusisahau kuwa hakuna safari isiyokuwa na mwanzo.

2. Mradi wa maji Shinyanga

Watanzania ni wepesi sana wa kusahau mambo, Sitashangaa kukuta wakazi wa kahama na shinyanga nao wakiwa kwenye mkumbo huu wa akina Diallo. Lowassa alisifiwa kama mkombozi siku za nyuma zilizopita, leo ndiyo tunampiga mawe na vijana wadogo wadogo wanadiriki hata kumtukana hadharani. Wananchi wa Kahama na Shinyanga, Lowassa akiwa waziri wa maji alidiriki Kutofautiana na kuwa wakali mithili ya mbogo kwa WAMISRI kwa ajili ya kuvuta maji ya ziwa victoria kutoka mwanza kwenda Kahama na Shinyanga. Hili jambo sio la mzaha ilihitaji kiongozi mwenye uwezo wa kudhubutu, ilihitaji kiongozi mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu, kitu alichofanya Lowassa na leo maji yapo Shinyanga. (Alidiriki kuuwambia WAMISRI nanukuu "kama munaona mazao yenu ni bora kuliko wananchi wangu, basi hamna tofauti na wauaji wakubwa katika dunia hii na mnastahili mtengwe na dunia nzima, nilisema na narudia kusema maji lazima watanzania tuyatumie kwa namna yoyote ile" (Majira may 22, 2005).

3. MAAMUZI MAGUMU DHIDI YA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA
Leo hii ninapoandika huu uzi tarehe 7, october, kama si Lowassa, viwanja vya mnazi mmoja vingekuwa magorofa ya akina Baghdad (wahindi), kwa wale wananchi waliyokuwepo 1994 wanakumbuka hili swala vizuri sana. Ni swala lililowazi na tunajua jinsi Lowassa alivyosimamia kidete bungeni mwaka 1994 na kuamua uzio wa mabati uvunjwe uliokuwa umezungushwa viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam, hakusubiri hata kumjulisha rais ila ulikuwa uamuzi sahihi kwa wakati sahihi.....Leo mashirika ya umma, mashirika binasfi na hata wanafunzi wanafanya matamasha mbali mbali katika uwanja huo, chama tawala kinafanya matamasha katika uwanja huo ila cha ajabu viongozi hao hao wanapokuwa mnazi mmoja wanaweza diriki hata kumtukana Lowassa mtu aliyeweka rekodi ya kuurejesha uwanja huo ila ni wa kuwasamehe kwani either hawajui historia ya nchi hii au wanapuuza historia ya nchi hii.

4. JENGO LA PPF
Ni Lowassa huyu huyu alifuta umiliki wa viwanja vya tajiri mmoja anayetamba jijini Dar es Salaam ambapo leo ndipo yamejengwa majengo ya PPF, International House na majengo mengine kadhaa. Leo hii haya majengo yamekuwa msaada mkubwa kwa shirika la umma kutoa ajira, na kutunza fedha za wajane, wakulima, wanafunzi nk badala ya kumilikiwa na mhindi moja. Leo hii PPF wamepata eneo la kutolea huduma kwa jamii, najiuliza bila Lowassa kurejesha eneo hilo leo PPF wangelikuwa wapi. kama mdau anayefaidika na PPF bila shaka naomba nitoe shukrani zangu kwa Lowassa.....Daima tutakukumbuka

5. City Water Saga
Ni Lowassa huyu huyu tunayembeza, aliwafukuza nchini kampuni ya City Water mwaka 2005, waliposhindwa kutimiza masharti yaliyokuwamo kwenye mkataba. City water walikwenda mahakamani, lakini hasilani hawakushinda kesi na wakatakiwa kulipa serikali ya Tanzania sh. billioni 15. Nakumbuka mkutano wao (City water, wadau wa maji Dar es Salaam, wakurugenzi wa Dar) "Lowassa alirudia tena na kuwaambia kama munaona mumeonewa kimbieni mahakamani ila huduma yenu ni mbovu hatuwezi kuvumilia, tena sasa hivi nawapa dereva wangu awapeleke maakamani kabla ya saa tisa na nunu mkafungue kesi, Hatuwezi kukubali upuuzi upuuzi, hii ni nchi yenye wananchi wanaoitaji huduma iliyo bora"; mwisho wa kunukuu

6. USIMAMIZI IMARA
Kwa aina za viongozi tulionao kuanzia mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na hata wakurugenzi wanahitaji usimamizi mkubwa sana, na katika karne hii hakuna aliyeonyesha karma hiyo zaidi ya Lowassa, wananchi wanakumbuka jinsi alivyokuwa mkali kwa hao watendaji na hata kudiriki kusimamisha baadhi yao ilimradi maslahi ya wananchi yatekelezwe kwa maendeleo ya nchi. Wananchi waliamini na wataendelea kuamini kwamba mtu kama Lowassa kama kweli tulihitaji kuyafikia maisha yaliyo bora, alifaa na atazidi kufaa katika historia ya nchi hii. Nani asiyefahamu kuwa kuanzia mawaziri mpaka mtendaji wa kijiji, alipokuwa waziri mkuu Lowassa akitokeza mahali watu wanatafutana na hata kula kona.

7. UJENZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI
Katika siasa za chama cha mapinduzi na ya nchi kuwa rais wa nchi tu hakutoshi ila kuna swali la kujiuliza je unaweza kuwa mwenyekiti wa chama tawala (kumbuka kofia hii ni moja), nafkiri hapa kwa wale wanachama wa ccm watanielewa (which I am not), ccm kama chama ni taasisi kubwa sana na yenye changamoto nyingi sana, ni taasisi yenye kelele nyingi, majungu, fitina, njama chafu nk hivyo ni watu wachache walio na uwezo wa kuwa mwenyekiti wa chama na at the same time kuwa rais, kama hauko imara sio siri moja kati ya hizo itakupwaya. Wana ccm je ni nani leo ana uwezo na nguvu ya kuhamasisha, kuimarisha chama na jumuiya zake? kama sio Lowassa........katika hoja hii namkumbuka sana JACKSON MAKWETA kuhusu aina ya viongozi watakaotuvusha na wenye uwezo wa kuwa mwenyekiti na at the same time kuwa rais. Makweta alisema hili tokea 2008 kuwa ni Lowassa tu aliye na uwezo wa kuwa na kofia mbili na hizo taaisisi zote zikawa stable. Aliongeza na kusema tunamuitaji mtu angalau asiwe kama Adolf Hitler, lakini Lowassa anatufaa sana wakati huu, hili liliongewa pia na kiongozi wa kiroho Askofu Laizer.

Bwana Edwin Ochele Ochwera "mkazi wa Tarime anaeleza kuwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wanaishi kama Mungu mtu katika eneo lake la kazi, mjane aliyeshindwa kutoa mchango wa shillingi elfu 5000 ya ujenzi wa maabara anawekwa ndani kwa siku 14 na mkuu wa wilaya bila melezo au mwalimu anayekatwa shillingi 10000 ya ujenzi wa maabara bila ya ridhaa yake Hapa Lowassa asingekubali na hata kuvumilia huu upuuzi; Kwa hakika tunamkumbuka sana Lowassa".....

Bwana Otitmach Gati mkazi wa Shirati alisema, Ndani ya ccm lipo kundi la watendaji wenye kufanya kazi kwa mazoea, hili swala linatufanya daima kutomsahau Lowassa. Najua wachache wanamchukia Lowassa kwa utaratibu wake wa kutofumbia macho maovu, wanaona utaratibu wake wa kuweka mambo wazi/hadharani ni kikwazo kwa wahuni ndani ya chama.....

8. Richmond
Hili swala limeongewa sana sana, wengine wameongea kwa kufanya analysis, wengine wanaongea kwa mihemuko ya kihisia na hata wengine kwa mihemuko ya kimwili. Sitaki kuzungumzia hili swala tena kwani limeongewa tokea 2008, na kwa bahati nzuri tumepata fununu kuwa muda sii mrefu mhusika ambaye kamati ya Mwakyembe haikumhoji yeye binasfi ila baadaye ikamhukumu ataliongelea hili swala muda ukifika. kwangu mimi kubwa naona haikuwa sahihi kuacha kumhoji Lowassa kama waziri mkuu, haitaji ujasiri kulisema hili la kutompa fursa ya kumhoji Lowassa, kwa hulka ya ubinadamu ni rahisi kwa wajumbe wa hiyo tumekujitetea, lakini hapo ndipo umimi (egoism) unathibitika.

Biblia takatifu na Quran usema, mtendee mwenzio sawa na utakavyo utendewe wewe. na pia usema kipimo hicho ukitumiacho kumpima mwenzio, ndicho kitakachotumika kukupimia haki yako mbele ya safari; kisheria kuna dhana ya natural justice. ila all in all watanzania kwa sasa wameanza kujua ukweli na tunatumaini pindi Lowassa atakapoongea tena tutajua mengi (baada ya kuliweka wazi katika mkutano wa NEC na kusema uongozi wake wa juu ulikuwa unajua kila kitu kuhusu mchakato wa Richmond....)....

9. Lowassa atokwa machozi Chimwaga
Hili ni mahususi kwa wana CCM, hasa kwa wale wanaojaribu kuleta ugomvi na kuaminisha jamii kuwa kuna ugomvi kati ya Lowassa na JK. Naomba kuwaambia kuwa these people are still friends na wametooka mbali... nakumbuka mwaka 1995 baada ya JK kushindwa katika kura za maoni na Mkapa Bwana Lowassa alikuwa kituko pale Chimwaga alipododosha machozi wazi kabisa mbele ya wananchi, JK najua anasoma huu uzi au wapambe wake watasoma huu uzi, naomba mumkumbushe inawezekana kwa mambo mengi aliyonayo kasahau kwa namna moja au nyingine. Ni Vijana hawa wawili walikuwa mbele katika kila harakati tokea 1994/1995; historia ya JK katika mbio za urais katika miaka yote haikamiliki bila kutaja jina la Lowassa, Pascal Mabiri, Rostam Azizi, na Azizi Aljabry.

10. Chakula cha Njaa
Ni Lowassa huyu huyu aliyesimamia chakula katika kipindi cha njaa (kumbuka /20062007/2008) kilikuwa kipindi cha ukame sana sana, uchumi wa dunia kushuka hivyo kuathiri hasa nchi masikini, uzalishaji kupungua nchini, na kilimo kushuka kwa asilimia 7.9% ila kwa umahiri wa Lowassa alihakikisha pamoja na hali hiyo wananchi wake hawafi na hata kulala njaa, alisimamia usambazaji wa chakula cha njaa kila tarafa, kila kata, na zaidi ya yote kila kijiji. Vile vile ni Lowassa huyu huyu aliyeleta jitihada kubwa sana katika kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam kwa utaratibu wa njia tatu, kuna watu wanasema hizo njia zilikuwa zinauwa watu sana, ila jamani hivi mpaka swala la kutoa elimu ya usalama barabarani mpaka waziri mkuu ndiyo atufanyie, kazi ya jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ni nini hasa?. Kwamba leo misingi yote ya barabara kupanuliwa za jiji la Dar es Salaam ni kwa vission aliyoakuwa nayo na yeye kuiasisi.....

Ni swali la kujiuliza sote, je Lowassa angekuwa madarakani mpaka sasa, unafikiri tungekuwa wapi kimaendeleo?

Tunakushukuru sana MR ocampo kwa kutupa ukweli, mtanzania yeyote ambaye ni mpenda maendeleo ya nchi yake , lazima MH LOWASA awe ni dira yake, nakupenda sana Lowasa
 
ofcoz and this time he look sick,very sick nimemuona jana itv akizungumzia mambo ya ardhi, 'wananchi wapewe misaada ya kisheria' nikahuzunika sana hawezi tena kuongea kwa ukakamavu ,actually we are in bad country.
 
Baada ya kuleta ule uchambuzi wa Timu za wagombea, kazi yangu ya pili ilikuwa ni kutembea mitaani kwa wananchi na kudadisi nini hasa wanachotaka na kutarajia katika uchaguzi mkuu wa 2015. Kitu kikubwa nilichojifunza ni kwamba watanzania ni wavumilivu sana na ni wachapakazi sana. La pili ni hili swala la wagombea wa CCM, wananchi bila kusita wamesema wazi kuwa ni vigumu kwa watanzania kumsahau Lowassa, kama mdadisi nilitaka kujua ni kwa nini wanasema hivyo? Majibu yao yalikuwa kama ifuatavyo........
1. Ujenzi Shule za kata
(Wananchi wanasema): Ni Lowassa huyu huyu aliyesimamia ujenzi wa shule za sekondari za kata Tanzania nzima. Hoja kwamba hazina walimu ni sahihi, lakini lipo swali la kujiuliza lakini kipi bora kutokuwa na vyote viwili, shule na walimu au kuanza kimoja?

Hapa wapo wenye hoja sahihi kabisa kuwa serikali ingeanza na kufundisha walimu kabla ya kujenga shule, lakini walimu hawa hawa iwapo wangehitimu kwa idadi kubwa na kukosa ajira, hoja hii ingegeuzwa na kudaiwa kuwa serikali inapaswa kujenga shule kwanza kabla ya kufundisha walimu. Kwamba Shule zinapokuwepo kasi ya mahitaji ya walimu inakuwa na mashiko (real) badala ya dhahania (imaginary) ila tusisahau kuwa hakuna safari isiyokuwa na mwanzo.

2. Mradi wa maji Shinyanga

Watanzania ni wepesi sana wa kusahau mambo, Sitashangaa kukuta wakazi wa kahama na shinyanga nao wakiwa kwenye mkumbo huu wa akina Diallo. Lowassa alisifiwa kama mkombozi siku za nyuma zilizopita, leo ndiyo tunampiga mawe na vijana wadogo wadogo wanadiriki hata kumtukana hadharani. Wananchi wa Kahama na Shinyanga, Lowassa akiwa waziri wa maji alidiriki Kutofautiana na kuwa wakali mithili ya mbogo kwa WAMISRI kwa ajili ya kuvuta maji ya ziwa victoria kutoka mwanza kwenda Kahama na Shinyanga. Hili jambo sio la mzaha ilihitaji kiongozi mwenye uwezo wa kudhubutu, ilihitaji kiongozi mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu, kitu alichofanya Lowassa na leo maji yapo Shinyanga. (Alidiriki kuuwambia WAMISRI nanukuu "kama munaona mazao yenu ni bora kuliko wananchi wangu, basi hamna tofauti na wauaji wakubwa katika dunia hii na mnastahili mtengwe na dunia nzima, nilisema na narudia kusema maji lazima watanzania tuyatumie kwa namna yoyote ile" (Majira may 22, 2005).

3. MAAMUZI MAGUMU DHIDI YA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA
Leo hii ninapoandika huu uzi tarehe 7, october, kama si Lowassa, viwanja vya mnazi mmoja vingekuwa magorofa ya akina Baghdad (wahindi), kwa wale wananchi waliyokuwepo 1994 wanakumbuka hili swala vizuri sana. Ni swala lililowazi na tunajua jinsi Lowassa alivyosimamia kidete bungeni mwaka 1994 na kuamua uzio wa mabati uvunjwe uliokuwa umezungushwa viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam, hakusubiri hata kumjulisha rais ila ulikuwa uamuzi sahihi kwa wakati sahihi.....Leo mashirika ya umma, mashirika binasfi na hata wanafunzi wanafanya matamasha mbali mbali katika uwanja huo, chama tawala kinafanya matamasha katika uwanja huo ila cha ajabu viongozi hao hao wanapokuwa mnazi mmoja wanaweza diriki hata kumtukana Lowassa mtu aliyeweka rekodi ya kuurejesha uwanja huo ila ni wa kuwasamehe kwani either hawajui historia ya nchi hii au wanapuuza historia ya nchi hii.

4. JENGO LA PPF
Ni Lowassa huyu huyu alifuta umiliki wa viwanja vya tajiri mmoja anayetamba jijini Dar es Salaam ambapo leo ndipo yamejengwa majengo ya PPF, International House na majengo mengine kadhaa. Leo hii haya majengo yamekuwa msaada mkubwa kwa shirika la umma kutoa ajira, na kutunza fedha za wajane, wakulima, wanafunzi nk badala ya kumilikiwa na mhindi moja. Leo hii PPF wamepata eneo la kutolea huduma kwa jamii, najiuliza bila Lowassa kurejesha eneo hilo leo PPF wangelikuwa wapi. kama mdau anayefaidika na PPF bila shaka naomba nitoe shukrani zangu kwa Lowassa.....Daima tutakukumbuka

5. City Water Saga
Ni Lowassa huyu huyu tunayembeza, aliwafukuza nchini kampuni ya City Water mwaka 2005, waliposhindwa kutimiza masharti yaliyokuwamo kwenye mkataba. City water walikwenda mahakamani, lakini hasilani hawakushinda kesi na wakatakiwa kulipa serikali ya Tanzania sh. billioni 15. Nakumbuka mkutano wao (City water, wadau wa maji Dar es Salaam, wakurugenzi wa Dar) "Lowassa alirudia tena na kuwaambia kama munaona mumeonewa kimbieni mahakamani ila huduma yenu ni mbovu hatuwezi kuvumilia, tena sasa hivi nawapa dereva wangu awapeleke maakamani kabla ya saa tisa na nunu mkafungue kesi, Hatuwezi kukubali upuuzi upuuzi, hii ni nchi yenye wananchi wanaoitaji huduma iliyo bora"; mwisho wa kunukuu

6. USIMAMIZI IMARA
Kwa aina za viongozi tulionao kuanzia mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na hata wakurugenzi wanahitaji usimamizi mkubwa sana, na katika karne hii hakuna aliyeonyesha karma hiyo zaidi ya Lowassa, wananchi wanakumbuka jinsi alivyokuwa mkali kwa hao watendaji na hata kudiriki kusimamisha baadhi yao ilimradi maslahi ya wananchi yatekelezwe kwa maendeleo ya nchi. Wananchi waliamini na wataendelea kuamini kwamba mtu kama Lowassa kama kweli tulihitaji kuyafikia maisha yaliyo bora, alifaa na atazidi kufaa katika historia ya nchi hii. Nani asiyefahamu kuwa kuanzia mawaziri mpaka mtendaji wa kijiji, alipokuwa waziri mkuu Lowassa akitokeza mahali watu wanatafutana na hata kula kona.

7. UJENZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI
Katika siasa za chama cha mapinduzi na ya nchi kuwa rais wa nchi tu hakutoshi ila kuna swali la kujiuliza je unaweza kuwa mwenyekiti wa chama tawala (kumbuka kofia hii ni moja), nafkiri hapa kwa wale wanachama wa ccm watanielewa (which I am not), ccm kama chama ni taasisi kubwa sana na yenye changamoto nyingi sana, ni taasisi yenye kelele nyingi, majungu, fitina, njama chafu nk hivyo ni watu wachache walio na uwezo wa kuwa mwenyekiti wa chama na at the same time kuwa rais, kama hauko imara sio siri moja kati ya hizo itakupwaya. Wana ccm je ni nani leo ana uwezo na nguvu ya kuhamasisha, kuimarisha chama na jumuiya zake? kama sio Lowassa........katika hoja hii namkumbuka sana JACKSON MAKWETA kuhusu aina ya viongozi watakaotuvusha na wenye uwezo wa kuwa mwenyekiti na at the same time kuwa rais. Makweta alisema hili tokea 2008 kuwa ni Lowassa tu aliye na uwezo wa kuwa na kofia mbili na hizo taaisisi zote zikawa stable. Aliongeza na kusema tunamuitaji mtu angalau asiwe kama Adolf Hitler, lakini Lowassa anatufaa sana wakati huu, hili liliongewa pia na kiongozi wa kiroho Askofu Laizer.

Bwana Edwin Ochele Ochwera "mkazi wa Tarime anaeleza kuwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wanaishi kama Mungu mtu katika eneo lake la kazi, mjane aliyeshindwa kutoa mchango wa shillingi elfu 5000 ya ujenzi wa maabara anawekwa ndani kwa siku 14 na mkuu wa wilaya bila melezo au mwalimu anayekatwa shillingi 10000 ya ujenzi wa maabara bila ya ridhaa yake Hapa Lowassa asingekubali na hata kuvumilia huu upuuzi; Kwa hakika tunamkumbuka sana Lowassa".....

Bwana Otitmach Gati mkazi wa Shirati alisema, Ndani ya ccm lipo kundi la watendaji wenye kufanya kazi kwa mazoea, hili swala linatufanya daima kutomsahau Lowassa. Najua wachache wanamchukia Lowassa kwa utaratibu wake wa kutofumbia macho maovu, wanaona utaratibu wake wa kuweka mambo wazi/hadharani ni kikwazo kwa wahuni ndani ya chama.....

8. Richmond
Hili swala limeongewa sana sana, wengine wameongea kwa kufanya analysis, wengine wanaongea kwa mihemuko ya kihisia na hata wengine kwa mihemuko ya kimwili. Sitaki kuzungumzia hili swala tena kwani limeongewa tokea 2008, na kwa bahati nzuri tumepata fununu kuwa muda sii mrefu mhusika ambaye kamati ya Mwakyembe haikumhoji yeye binasfi ila baadaye ikamhukumu ataliongelea hili swala muda ukifika. kwangu mimi kubwa naona haikuwa sahihi kuacha kumhoji Lowassa kama waziri mkuu, haitaji ujasiri kulisema hili la kutompa fursa ya kumhoji Lowassa, kwa hulka ya ubinadamu ni rahisi kwa wajumbe wa hiyo tumekujitetea, lakini hapo ndipo umimi (egoism) unathibitika.

Biblia takatifu na Quran usema, mtendee mwenzio sawa na utakavyo utendewe wewe. na pia usema kipimo hicho ukitumiacho kumpima mwenzio, ndicho kitakachotumika kukupimia haki yako mbele ya safari; kisheria kuna dhana ya natural justice. ila all in all watanzania kwa sasa wameanza kujua ukweli na tunatumaini pindi Lowassa atakapoongea tena tutajua mengi (baada ya kuliweka wazi katika mkutano wa NEC na kusema uongozi wake wa juu ulikuwa unajua kila kitu kuhusu mchakato wa Richmond....)....

9. Lowassa atokwa machozi Chimwaga
Hili ni mahususi kwa wana CCM, hasa kwa wale wanaojaribu kuleta ugomvi na kuaminisha jamii kuwa kuna ugomvi kati ya Lowassa na JK. Naomba kuwaambia kuwa these people are still friends na wametooka mbali... nakumbuka mwaka 1995 baada ya JK kushindwa katika kura za maoni na Mkapa Bwana Lowassa alikuwa kituko pale Chimwaga alipododosha machozi wazi kabisa mbele ya wananchi, JK najua anasoma huu uzi au wapambe wake watasoma huu uzi, naomba mumkumbushe inawezekana kwa mambo mengi aliyonayo kasahau kwa namna moja au nyingine. Ni Vijana hawa wawili walikuwa mbele katika kila harakati tokea 1994/1995; historia ya JK katika mbio za urais katika miaka yote haikamiliki bila kutaja jina la Lowassa, Pascal Mabiri, Rostam Azizi, na Azizi Aljabry.

10. Chakula cha Njaa
Ni Lowassa huyu huyu aliyesimamia chakula katika kipindi cha njaa (kumbuka /20062007/200 kilikuwa kipindi cha ukame sana sana, uchumi wa dunia kushuka hivyo kuathiri hasa nchi masikini, uzalishaji kupungua nchini, na kilimo kushuka kwa asilimia 7.9% ila kwa umahiri wa Lowassa alihakikisha pamoja na hali hiyo wananchi wake hawafi na hata kulala njaa, alisimamia usambazaji wa chakula cha njaa kila tarafa, kila kata, na zaidi ya yote kila kijiji. Vile vile ni Lowassa huyu huyu aliyeleta jitihada kubwa sana katika kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam kwa utaratibu wa njia tatu, kuna watu wanasema hizo njia zilikuwa zinauwa watu sana, ila jamani hivi mpaka swala la kutoa elimu ya usalama barabarani mpaka waziri mkuu ndiyo atufanyie, kazi ya jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ni nini hasa?. Kwamba leo misingi yote ya barabara kupanuliwa za jiji la Dar es Salaam ni kwa vission aliyoakuwa nayo na yeye kuiasisi.....

Ni swali la kujiuliza sote, je Lowassa angekuwa madarakani mpaka sasa, unafikiri tungekuwa wapi kimaendeleo?
 
iwe isiwe Lowasa ni rais kwa mbinu zilezile zilizomungiza jk ndo atatumia kuingia magogoni
 
Lowassa ni mdandiaji hakuna jipya alilolifanya kwa ubunifu wake yote yaliyotekelezwa ni yale yaliyoibuliwa na Mkapa chini ya waziri wake mkuu Sumaye.Fedha zote zilizotumika ni zile ambazo ziliachwa chini ya uongozi wa Mkapa.Katika jambo moja wapo lenye faidi kwa Taifa ni pamoja na kuondoka Lowasa madarakani bila kumpunguza fisadi hata mmoja kama Lowasa tungekuwa na hali mbaya sana zaidi ya hii tuliyonayo.
 
japo lowassa ni fisadi lakin JOKA LA NDIMU anapwitapwita kusoma huu uzi
 
Lowasa alikuwa kwenye madaraka makubwa kwenye serekali hihii na tangu serekali hii iingie madarakani wananchi hawajawahi kupata nafuu yoyote,kilio kilianza mara baada ya serekali hii kuingia madarakani.Kuondoka kwa Lowasa kumesaidia sana vinginevyo wananchi wangekuwa wametumbukizwa kwenye makorongo.
 
lowassa ni mgonjwa atapofuka macho ndani ya miaka5 ijayo na strokes zake alaf awe mzigo kwa taifa kama Ariel Sharon RIP
 
Lowasa alikuwa kwenye madaraka makubwa kwenye serekali hihii na tangu serekali hii iingie madarakani wananchi hawajawahi kupata nafuu yoyote,kilio kilianza mara baada ya serekali hii kuingia madarakani.Kuondoka kwa Lowasa
kumesaidia sana vinginevyo wananchi wangekuwa wametumbukizwa kwenye makorongo.
watu wengine Bwana ulitaka Lowasa akulete maisha nyumbani kwenu
 
Lowasa ana mvuto mkubwa sana kwa watu kama Jk alivyo kuwa, kama walikwenda kwa mganga wa kienyeji watakuwa walikwenda pamoja na kwa mganga mmoja pia ni marafiki ambao hawakukutana barabarani.Lowasa akiwa Rais hakuna cha tofauti atakachokifanya zaidi ya hiki kinachofanywa na serekali ya sasa.
 
Waliomfelisha jk ni kina membe kazi dk ni majungu na kufatilia maisha ya lowasa
 
NDIYO UKISHASOMA HAYA HAPA CHINI NI KWELI NI VIGUMU KUMSAHAU LOWASA

LOWASA

Kwa mapenzi mema na nchi yetu na mwana (CCM) napenda niwape mfano hai wa Bwana Lowasa asivyo muadilifu na asivyopenda kuwajibika kichama CCM na kiserikali. Tanzania nzima mtakumbuka kuwa huyu mheshimiwa Edward Lowasa alikuwa ni mmoja wa wagombea wa nafasi ya Urais mwaka 1995 na akaenguliwa kwa hoja nzito ya kutokuwa muadilifu na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere, kwa ukweli (wala sio tuhuma) kuwa alikuwa amejilimbikizia mali nyingi kwa kipindi kifupi ndani ya CCM na Serikali.Muda mfupi alikuwa ni mtumishi wa CCM, muda mfupi kama Mkurugenzi wa kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha.
Mfano hai wenyewe uko hivi; tufuatane kwa kuusoma tafadhali:-
Mara baada ya kurudi Butiama, 1995, baada ya kuenguliwa kugombea nafasi ya urais, siku moja mapema asubuhi Bwana Lowasa alinipigia simu na kusema yafuatayo:
“Bwana Kasori, naomba uende kumwambia Baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, aende Monduli kusaidia kusafisha jina langu ili nisikose ubunge kutokana na yale aliyonisema Dodoma’. Nilishikilia mkono wa simu (TTCL) kwa zaidi ya nusu saa tukiwa tunazungumza na hatimaye mimi nilipata ujasiri wa kumwambia Bwana Lowasa kuwa siwezi kwenda kusema maneno hayo kwa Baba wa taifa na kwamba akitaka aje Butiama na nitamruhusu waongee ana kwa ana. Nikanyamaza na hatimaye yeye akawa wa kwanza kukata simu. Hiyo ikawa itifaki njema kwangu!
Kesho yake tena asubuhi nilipokea simu, safari hii akawa ni mheshimiwa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa. Kwa maneno yake alisema “Bwana Kasori,jana ulizungumza na Edward Lowasa; naomba ufikishe ombi lake kwa Baba wa taifa tafadhali”.
Kutokana na heshima ya Mheshimiwa Mzee Kawawa, nilikubali na nikaenda na kabla ya hapo nilimuomba Mzee Kawawa akae karibu na simu ili nimpe jibu muda si mrefu.
Nilimueleza Baba wa Taifa kuwa “Mheshimiwa Edward Lowasa kupitia kwa Mhe. Mzee Rashidi Mfaume Kawawa anaomba usaidie kusafisha jina lake kule jimboni kwake Monduli ili asikose ubunge kutokana na yale uliyomsema katika Kamati Kuu ya CCM Dodoma”. Jibu la Baba wa Taifa alilonipa ni kuwa “Nenda umwambie Mzee Rashidi Mfaume Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa”!
Watanzania wote, leo March19, 2008, nawaomba radhi kuwa jibu hilo kwa uzito wa maneno hayo kuwa “Kawawa asiwe mjinga kama Lowasa” kweli kwa kuzingatia heshima kati ya wazee hao wawili; “Kawawa sikumwambia hivyo”! Badala yake nilimdanganya (nawaomba radhi tena watanzania) jibu nililompa Mzee Kawawa ni kuwa juma lililokuwa linafuata tungekuwa Dar es Salaam na kwamba aje Msasani aongee na Baba wa Taifa. Mhe. Kawawa alikubali.
Nikarudi kwa Baba wa taifa kusema uongo (naomba radhi tena) kuwa “Mzee Kawawa ameomba mzungumze tatizo la Lowasa tutakapofika Dar es Salaam”. Baba wa taifa alikubali na akaagiza nimuombe Mhe. mzee Kawawa kuwa Lowasa na Guninita na wapambe wengine wa Lowasa wote wafike Msasani.
Siku ya siku ikafika. Tukawepo Msasani na Mhe.mzee Kawawa akaja. Lowasa hakuwepo! Sababu anazijua mwenyewe.(muulizeni maana nasema ukweli). Mkutano ulipoanza mzungumzaji wa kwanza nikawa mimi, kueleza lengo la mkutano. Mzungumzaji wa pili alikuwa Baba wa Taifa na swali la kwanza ni kuuliza Lowasa yuko wapi?.
Bila kupoteza wakati Mwalimu alisema “Rashidi , huyu Kasori ananiambai eti niende Monduli nikasafishe jina la Mhe. Lowasa eti asikose ubunge kwamba nilimchafulia Dodoma katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM. Kutokana na ombi lako nilimtuma akuambie usiwe mjinga kama Lowasa. Kasori alikuambia eh?”
Oneni , huko nyuma tayari nilishasema uongo kwa kutosema maneno hayo kwa Mhe. mzee Kawawa. Kweli hilo kurudiwa na Baba wa Taifa kwa Mzee Kawawa mbele yangu lilisababisha kalamu yangu kuanguka, nikatetemeka na nikatokwa na jasho jingi mbele ya hao wazee!!! Bila kutegemea na kwa mshangao mkubwa Mhe. mzee Kawawa alikubali kwa kuitikia “NDIO ALINIAMBIA”. Mwalimu akacheka sana!!!! Sababu sijui hadi leo kwa nini alicheka sana.
Kwa kuendelea, Mwalimu alimwambia Mzee Kawawa kuwa “Kasori ana umri mkubwa kuliko Lowasa. Kasori alipata taabu sana kufikisha kwangu ombi la Lowasa na aliniambia kuwa jana yake alikuwa amekataa ombi la Lowasa. Sasa nasema kuwa kwa umri wangu mimi mzee, Lowasa ni mtoto wangu tena mdogo sana. Kwa heshima mliyonayo kwangu na kwa chama cha Mapinduzi mtanishangaa sana mkisikia niko Monduli eti nipo kwenye majukwaa nasafisha jina Bwana Lowasa asikose ubunge.
Kweli Lowasa ni jasiri sana kusema maneno hayo. Hayo ningeambiwa na Kasori tu ningesita kumuamini. Lakini kwamba hata wewe Rashidi ulitumiwa kusema maneno hayo! Huyu Lowasa ni jasiri sana!!. Lakini kwa nini hajatuambia ukweli kuhusu mali hizo ambazo ni nyingi kuliko mimi ambaye nimekuwa Rais wenu kwa kipindi kirefu? Sasa Bwana Rashidi, nakuomba hivi, kamwambie mwenyekiti wa CCM Mhe. Mwinyi aitishe wajumbe wote wa Kamati Kuu, chagueni tarehe na mahali popote Tanzania, mimi nitakuja kumsafisha Bwana Lowasa na nitagharamia mkutano huo kwa hela zangu. Kamwe msitumie hela za chama wala serikali. Monduli sitokwenda,umesikia eh?”
Mkutano ukaisha hapo Msasani. Hadi uchaguzi 1995, unafanyika na kumalizika Baba wa Taifa hakwenda Monduli. Alichukia sana tabia za Lowasa na alimfahamu kama mtu muongo na mwenye kiburi. Hadi Baba wa Taifa anafariki,sikuwahi na hata niandikapo makala hii sijasikia wala kusoma popote ambapo Lowasa anakanusha alivyolombikiza mali akiwa mtumishi wa CCM na serikali kwa muda mfupi kiasi cha kumzidi Rais wa Kwanza !!!
Sasa anatuhumiwa na vyombo vya habari kununua sehemu ya Ranchi za Taifa kwa kuandika majina ya wanafamilia! Kama hilo nalo ni kweli, ningekuwa mimi nisingeota tena kugombea URAIS n.k Tanzania. Bora kuendelea na biashara kwa uwazi kuliko kupitia mgongo au wa serikali au wa chama ( CCM). Huo ndio ushauri wangu kama mwana CCM kwa Lowassa.
Angalia tunavyofanya “total transgression of CCM regulations and ethics.” Kamati kuu 1995 ilimwona Mhe. Lowassa hana uadilifu. Mhe. Mkapa baada ya kuingia madarakani baada ya muda si mrefu sijui ni kwa kikao gain cha CCM na taasisi ipi ya serikali akamwona Lowassa ni safi na akamweka katika safu yake ya baraza la mawaziri.
Huyu bwana akaendelea na huo usafi hadi akaukwaa uwaziri mkuu 2005. Yote haya yanatia shaka kama kweli ndani ya CCM na Serikali tuna benki sahihi za takwimu za mienendo kitabia ya wanachama na watumishi wetu kama si kubebana kwa majina tu! Nilinunua gazeti la mzalendo nikampa Baba wa Taifa na aliposoma kuwa Lowassa ni Waziri alimaka AHH!!
Katika hili nabaki nimeduwaa hasa tunapopeana madaraka makubwa ya kuendesha nchi kimzaha tu. Tukumbuke kuwa kwa kila kitu na kwa dini yoyote Mungu huweka wazi mambo mahali na kwa muda atakao yeye.( Time and space) ya Mwalimu J.K Nyerere juu ya Lowassa tuliyapuuza. Sasa Mungu kayaanika! Basi tuone hizi tuhuma za RICHMOND n.k, Mikataba ya Madini, EPA zitakavyoshughulikiwa.
Ni huyu Lowasa leo anasema kanyimwa “Natural Justice” hakuulizwa na kamati , kaonewa, kamati ya Mwakyembe inauonea wivu uwaziri mkuu wake na ni mahiri wa kuchukizwa mikataba mibovu na kudhalilika! Oh kweli?
Hivi Lowassa amewahi kusoma wasifu wa kila mmoja wa hao? Bila kupima uzito, busara na hekima ya maneno yake anasema ameachia ngazi kama alivyofanya Mhe.Alli Hassan Mwinyi, Peter Kisumo, Peter Siyovelwa n.k. Hivi CCM yetu hawa ndiyo viongozi tulio nao ngazi za juu? Wasio sema ukweli? Tukumbuke na kukiri kwa dhati wajibu wa wanachama wa CCM , katika katiba (ccm) inasema 15 (7) “ kuwa tayari kujikosoa na kukosolewa…
Watanzania wenzangu haya anayosema Lowasa yanafanana na nukuu niliyoanza nayo? Fikiria nairudia tena “For those winding and crooked courses, are the goings of the serpent, which goes basely upon the belly and not upon the feet!
There is no vile that does cover a man with shame as to be found false and pertifidious” Niharakishe kusema hapa kuwa viumbe vyote ambavyo havikupenda kusema ukweli Mungu aliviadhibu kwa kuvifanya vitembelee matumbo yao milele nyoka wakiwemo! Lowasa, Mwanyika, Hosea na wenzake naomba kama nilivyoanza, tafadhali wasome hiyo nukuu mara kadhaa na waielewe na kuizingatia.
Watanzania wanawashangaa, wanadharau na kuchukizwa na viongozi wasiopenda kusema ukweli kwa maisha magumu waliyo nayo ambayo wao wanawazomea kwa dharau kuwa ni wavivu na wachovu wa kufikiri. Wanasahau kuwa hawa watu wa kawaida ndio wanaozalisha kile kinacholipa mishahara na marupurupu yao.
Kama viongozi wakuu wa CCM, katika hili daima kumbukeni wajibu wenu kwa mujibu wa katiba ya CCM, ibara ya 15 (4) kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania. Onekaneni hivyo kwa vitendo tafadhali. Utaratibu huu wa kusema uongo unadhoofisha amani na utulivu Tanzania.
Hayo niliyasema niko tayari kuyasema bungeni akiwepo Lowasa ikibidi. Hatuwezi kukubali nchi hii kuendelea kuwa na viongozi wa aina hii. WAWE WAKWELI, WASEME UKWELI TU. WANAPOKOSEA HARAKA NA KWA UKWELI NA UNYENYEKEVU WAOMBE RADHI KWENYE VYAMA VYAO, SERIKALINI NA KWA WANANCHI. NI UPUUZI WA HALI YA JUU KUJITETEA OVYO NA KUINGIZA UKABILA ( LOWASSA NA OLE NAIKO) HATA KWA MAKOSA YALIYO DHAHIRI.
Katika mahojiano na TVT Lowassa alikiri kuwa alishindwa kuvunja mkataba wa RICHMOND. Sababu alizitaja. Sawa. Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa Serikali, kwa mujibu wa kanuni za kudumu za utumishi wa umma ( Toleo 1994), kifungu F33, makosa yake kiserikali ni haya yafuatayo; 33( xi) omission which is against public interest. 33(xiii) negligence occasioning loss to the employer ( yaani serikali na taifa kwa ujumla). 33( xiv) gross negligence in the performance of duty.
Kama mtendaji mkuu wa shughuli zote nzito za serikali bwana Lowassa hana namna ya kujitetea kwa makosa hayo yaliyodhahiri ambayo TANESCO imeendelea kudhoofishwa na RICHMOND kwa yeye kuogopa kutumia utaalam nje ya wale aliowaamini. Mbona tuna vyuo vikuu, je, aalivitumia kikamilifu? Mbona kwa maswala yasiyo na maslahi ya maana tumezoea sasa kukodi wataalam wa nje?
Kwanini hakujiridhisha katika maeneo yote hayo? Tatizo hili ni kubwa sana maana watanzania sasa wanatozwa viwango vikubwa sana kulipia umeme ikiwa ni pamoja na sehemu za uzalishaji zenye kutumia umeme achilia mbali malipo ya capacity charges? Nani anabisha kuwa kwa huu mkataba wa RICHMOND n.k Bwana Lowassa na Wenzake waliweka sahihi za kifo siyo kwa TANESCO tu bali pia cha kuvuruga maendeleo ya nchi yetu na kuendeleza umasikini?
Katika yote haya ambayo yamesemwa, Bwana Lowassa na wenzake wajue kuwa kama watanzania, we have a compelling moral case for complaining against him.
There is also a compelling case that is in Tanzania’s self interest. Recently many trade agreements already have made the poorest countries worse off. Such agreement already have condemned to death thousands of our people . Corporations of whatever name do strip Tanzania of its natural resources leaving behind a trail of environmental devastation etc. This is done through very poor legal frameworks. Nimuhimu tukawa na viongozi waaminifu, waadilifu na wasema ukweli. Kwa haya yanayotendeka, something is fundamentally wrong with our government.
Kwa kila maamuzi tunayoyafanya mara zote tuzingatie ni kwa maslahi ya nani; yale ya Taifa ni kipaumbele cha kwanza. Tuzingatie matumizi mazuri ya rasilimali zetu daima. Duniani ziko serikali nyingi tu ambazo zimevunja mikataba mibovu. Kwa ziara nyingi ambazo viongozi wetu wanafanya na baada ya wanahabari kupigia kelele RICHMOND, kwanini Lowassa huko nje hakutaka kujifunza namna ya kuvunja mikataba mibovu?
Yaani umahiri wake uliishia mkataba wa maji Dar es salaam na kiwanja cha Mnazi Mmoja? Mikakati yetu ya maendeleo imekuwa haileti tija iliyokusudiwa moja ya sababu ikiwa a flawed vision of development. Successful countries have a broader vision of what development entails and a more comprehensive strategy for bringing it about.
It is very unfortunate that in the majority of developing countries Tanzania included the nation – state has been weakened thoroughly! Haya maamuzi yanayofanywa na viongozi kama Lowassa ndiyo matokeo ya kutojua namna ya kuthibiti na kutumia kwa uangalifu fursa za kitu kinaitwa UTANDAWAZI.
Government that attempt to control capital flows find themselves unable to do so, as individuals find ways of circumventing the regulations. A county may want to raise the minimum wage, but discovers it can’t, because foreign companies operating there will decide to move to a county with lower wages.
Situmeona jinsi waziri Chiligati ( waziri wa kazi wa wakati huo) alivyohenyeshwa na wakubwa – wawekezaji kukataa kulipa kima cha chini hapa Tanzania? Wengine wamepunguza kazi ndugu zetu na sasa ni katika kundi la Machinga! Waziri mkuu wa wakati huo Lowassa alisaidiaje? KIMYA! Dhahiri kinachoonekana hapo ni sense of powerlessness. Kwa kukumbatia matajiri na wakubwa wa nje, kupitia utanzawazi, baadhi ya viongozi wetu kama inavyojidhihirisha kupitia RICHMOND n.k. find their ability to act eroded.
These days it is the order of the day for the electorate to see its government bending before foreigners wenye (mitaji). Day in day out democracy is being systematically undermined. When the electorate shouts through the media etc, no body listens! Wanataka sifa tu.
The electorate feels being thoroughly betrayed. Whether we like it or not, it is perceived, quite rightly, I think the way globalization is currently managed is not consistent with democratic principles. Little weight is given to the concerns and voices of ordinary people and the poor! Kwa kiburi cha wakubwa kutosikia, kutopenda kukosolewa Tanzania inaendelea kubaki masikini. Lowassa na wenzake wangekuwa makini na mahiri katika kusikiliza waandishi wa habari mapema RICHMOND n.k isingetufikisha tulipo sasa ambapo kila siku tunapoteza fedha nyingi.
Tusingekuwa na tume juu ya tume ambazo baadhi tunazibeza kwa kejeli hata kwa kutumia chama (CCM). CCM kweli tunasoma na kuzingatia kwa vitendo wajibu wa mwanachama wa CCM kifungu 15(3) na 15 (4) na 15(7) pamoja na ahadi za mwanachama wa CCM (3) na (4), na (8). Hivi CCM sasa ni mali na jina la mtu; kwamba hivyo mtu akikosolewa hamtaki kuona kakosa na mko tayari chama kife kwa ajili ya mtu mmoja au kundi dogo tu la watu? Nendeni Butiama mtupe majibu tafadhali. Uwezo, busara na nia vyote mnavyo. Ningekuwa Lowassa Butiama nisingeenda. Yeye kwenda huko ni kejeli kwa Baba wa Taifa.
BADO TUTAENDELEA KUWASEMA WENZAO KUHUSU MIKATABA YA HOVYO NA UKWAPUAJI WA RASILIMALI ZA NCHI HII. HOJA YA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR BWANA IDD PANDU HASSAN- “ Lowasa kutostahili kuitwa Waziri mkuu Mstaafu” ni muhimu ikazingatiwa sambamba na utata wa stahili za mafao. Haitoshi kuimba utawala wa sheria na kumbe inapofika kwa wakubwa tunakunja na kunyonga sheria zetu. Sheria ni Msumeno. Someni Pensions Ordinance cap 371 sambamba na kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la (1994) kifungu F53 (d) na (e). Tusiwe na kigugumizi katika hili.Tujifunze yaliyojiri hapo jirani Kenya hivi majuzi.
Namalizia kwa kusema “Tuheshimu na kudumisha kitu UKWELI”. Kwa viongozi, zingatieni na kwa unyenyekevu heshimuni viapo vyenumnapokabidhiwa madaraka. Baba wa Taifa daima katika mkoba wake alibeba Bibilia na Azimio La Arusha.
Nyinyi kwa kipindi hiki kigumu cha ufisadi na kukithiri kwa rushwa na mikataba mibovu; bebeni daima photo-copy za viapo vyenu pamoja na Bibilia au Koran pamoja na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mnazo dini zenu. Sikusikia yeyote akiapa kwa dini za asili kwa Rais au kwa Spika wa Bunge. Nawashukuru watanzania, Mhe. Spika na Waandishi wa habari ambao wamekemea maneno ya Lowasa na wenzake baada ya kikao cha Bunge.
Namshukuru sana Mhe. William H. Shelukindo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji na Biashara kwa kuwasilisha hoja ya kuundwa kwa kamati ya kuchunguza Richmond na shukran maalum nazitoa kwa Dr. Mwakyembe na wajumbe wote walioshughulikia suala la Richmond na kuwasilisha taarifa Bungeni kwa uadilifu mkubwa sana.
Mwisho nawashukuru Watanzania wote na nchi za nje walionipongeza na kunipa moyo kuhusu makala zangu za kukemea ukwepuaji rasilimali za nchi BoT yenye kichwa cha habari “Salaam kwa Mawaziri” Namshukuru Rais Kikwete. Namshukuru pia Mhariri gazeti la Rai namba 748 na 749. Halmashauri kuu ya CCM inayokutana Butiama naitakia mafanikio makubwa katika maazimio watakayofikia . Baada ya hapo muonekane mmedhamiria kutenda kwa kuleta maendeleo yenye kuzingatia uadilifu na uwajibikaji
Viongozi wabovu wawajibishwe tu.
Watanzania wengi leo bado wanamlilia Mwalimu J.K. Nyerere hasa kwa matatizo kama haya ya mikataba mibovu ya Madini, RICHMOND n.k. Wanasema sorry Mwalimu lived ahead of his time. Alituangazia kwa mengi, hakuna wa kututetea leo kwa matatizo yote haya.
Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Afrika
Samwel. H. Kasori
Katibu mstaafu wa J.K.Nyerere
0754 372141

Andiko refuuuu hakuna refference hata moja, unataka tuamini maneno yako? Sio rahisi kamanda...kuhusu hili la mwalimu na Lowassa nakuja na ukweli wote few days to come wala msiweweseke
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom