Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 4,439
- 4,153
Ujinga MKUBWA SANA tulio nao Watanzania ni kusita kutumia fursa tuliyo nayo ya mfumo wa vyama vingi kuwapa mrejesho stahiki wanasiasa na vyama vyao. Tulitakiwa kutumia mfumo huu kuwaadabisha wanasiasa watende yanayostahili kuhakikisha maendeleo, utawala bora na haki vinashamiri nchini. Kwamba kwa kutumia kura zetu tuwe na uwezo wa kubadili vyama na viongozi mara kwa mara tusiporidhika na utendaji wao. Tuwaonyeshe kwamba sisi ndio wenye kauli ya mwisho katika ajira zao.
Badala yake tumekalia kushabikia vyama na watu kama vile ni suala la soka au hata dini kabisa. Tunaabudu watu na vyama badala ya kuona ni wenzetu tu tunaowapa dhamana ya uongozi wafanye kazi na kupisha wengine tukimua. Tumeishia kujenga utamaduni wa kujikomba (sycophancy) kwa watu na vyama badala ya kuwadhibiti inavyostahili. Tunawapa binadamu "gerentii" ya hatamu za dola milele na milele halafu tunashangaa sana wakitutenda na kutuita wapumbavu!
Ukweli ni kwamba kama hatutachukua hatua kamili ya kuanza kubadili vyama na uongozi wa nchi kikamilifu basi tukae tayari kwa adha zisizomithilika. Kwangu mimi CCM ikirejea madarakani mwaka huu hakuna Mtanzania atakayekuwa na stahili ya kulalamika kuhusu uongozi mbaya na manyanyaso ya dola. Kulalamikia viongozi na familia zao kutajirika kwa mtindo wa nepotism na patronage itakuwa ni wivu tu unawasumbua. Hapo tena ni kila mtu kubeba furushi lake: everyone for himself/herself and God for all of us.