HesabuKali
JF-Expert Member
- Jan 4, 2016
- 2,880
- 5,881
Mlishawahi kutarajia mazuri zaidi ya haya ila hamkupata mlichotarajia zaidi ya maumivu. Kuna zile Noah zenu mshapewa tayari?Ni uhalisia tunaoutarajia mda mchache ujao baada ya mambo kukamilika
Hizo NEEMA mnazotarajia kupitia nchi jirani, mtambue nyinyi sio nchi pekee yenye Bandari, Kenya wanaweza pia kurahisisha mambo wakahudumia nchi za Rwanda, Uganda na Burundi, Beira inaweza kuleta ufanisi ikalisha Zambia, Malawi na Lubumbashi na Harare.
NDIO maana DP WORLD wameweka vipengele vigumu kuvunja au kushtakiwa msipofikia matarajio/ underperformance walijua fika kabisa Kenya hawajalala na wana akili timamu kuwazidi CCM na misukuke yao.
Nakata nikuhakikishie, kwa akili za CCM hamtakuwa na Bandari yenye ufanisi mkubwa kuzidi Bandari za Mombasa,Malindi na Beira, kwahiyo hilo soko mnalotarajia mnaenda kupata robo yake tu tena kwa hasara.