Watanzania na usingizi wa pono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania na usingizi wa pono

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrahim K. Chiki, Jan 31, 2012.

 1. Ibrahim K. Chiki

  Ibrahim K. Chiki Verified User

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 594
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wadau. Ukiangalia kiundani, madai ya madaktari wa tanzania ni muhimu sana, si tuu kwa madaktari bali na wananchi kwa ujumla. Ni kweli kwamba mazingira ya hospital zetu yakiboreshwa, mwananchi wa kawaida atanufaika, ni kweli kwamba mishahara na malipo ya watumish na madaktari yakiboreshwa wananchi watanufaika.

  Ila inasikitisha kuona kwamba watanzani wanakosa uzalendo wa kuwasapoti madaktari, hata kwa maaandamano. Serikali inapata wapi kiburi cha kujiamulia mambo, na je watanzania wakiamua kuionyesha serikali kwamba ni wajibu wake kuboresha huduma za jamii na siyo mifuko ya wabunge watashndwa?

  Au ni ulimbukeni na uelewa mdogo wa watanzania. Inauma sana. Ni haki ya kila mtz kupinga udhalimu huu wa serikali. Amka na tuchukue hatua.
   
 2. W

  We know next JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ahsante Mkuu, thread imetulia vyema sana. Kwa hakika tumelala usingizi wa pono. Ukiangalia kwa undani, madai ya madaktari yanataka pia mazingira ya hospitali na wagonjwa yaboreshwe. Kweli watanzania tumeshindwa kuliona hilo???
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aksante Marhaba hiki kitu wengi tumekiangalia juu juu tu na kuchukulia kuwa hili ni sakata la madaktari na serikali. Hebu tupeni kadava zenu mnazofanyia mazoezi tuingie nazo mtaani sisi. Tumechoka sasa
   
 4. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,797
  Likes Received: 6,306
  Trophy Points: 280
  Ngoja na sisi walimu tuandae Mgomo. Tumechoka kula vumbi la chaki na kutembea kilomita si chini ya tano kila mwezi kufuata mshahara
   
 5. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Watanzania ni watu wa kulalamika na kuishi kwa matumaini ya kumuomba Mungu. Mungu hata siku moja hataingilia masuala ambaya yako ndani ya uwezo wa binadamu kuyatatua. Hivi nchi zingine wananchi wanapozitimulia mbali serikali zao watu huwa wanadhani ni Mungu yule?
  Mimi nina wasiwasi mkubwa juu uwezekano wa wananchi kulizua hapa nchini, iko siku tutakumbushana hili hapa hapa.
   
Loading...