activisty
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 315
- 107
Nianze kuandika waraka huu mfupi, kwanza kwa kuweka bayana ufafanuzi halisi wa kile ninacho kusudia kufikisha kwenu wana jamii na Watanzania wote kwa ujumla ambao mtapata nafasi ya kukutana na ujumbe huu popote pale mlipo. Katika waraka huu nitakwenda kuzungumzia mambo yanayoendelea hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuitazama hali halisi ya kisiasa na kiuchumi nchini, maisha ya Mtanzania, elimu na mabadiliko hasi pamoja na dira ya uongozi mikononi mwa serikali ya awamu ya tano.
Ni dhamira ipi naijenga kwa kusema "watanzania na maisha ya mpira ndani ya uwanja"? Si dhamira nyingine bali dhamira ya dhati na kweli ya kutaka kueleza hali halisi ya maisha ya mtanzania na hatima yake. Siku zote mpira unapokuwa ndani ya uwanja unakuwa na maisha yasiyoeleweka. Mpira huenda popote pale wachezaji wa timu husika wanapotaka uende kwa juhudi zao binafsi. Mpira hauna mshabiki wanaoshabikiwa ni wachezaji na timu wanazochezea. Mpira ndio tegemeo kubwa la timu hizi pamoja na mashabiki zao, pasipo mpira hakuna kitakachoendelea.
Leo hii watanzania hatuna tofauti na maisha ya mpira ukiwa uwanjani. Wanasiasa pamoja na wanaojiita wasomi na watetezi wa wanyonge wanatutumia watakavyo. Kwa juhudi zao na ushawishi wao wanatusukuma kule wanapotaka tuende, kule wanapotaka tuelekee.Anakuja mwanasiasa anasema "hapa kazi tu" tuache siasa tufanye kazi tupate maendeleo. Lakini ayasemayo ndio siasa yenyewe na ndio kazi yake. Yani mtu yupo kazini anafanya kazi yake alafu anataka kutuaminisha kuwa hafanyi kazi hiyo inawezekanaje?
Anakuja msomi anasema, hapana tusikubali haki zetu zinaibiwa, wanatumia raslimali zetu vibaya hawa wanasiasa, tusikubali haya mambo ni ya kitaalamu na hayatekelezeki. Baada ya mwaka tunakutana na msomi huyuhuyu majimboni wakiwa na mwanasiasa huyuhuyu wakiombeana kura(kula.) Mwisho msomi anakuwa mwanasiasa na maisha yanaendelea. Lakini yupo mtu anaejiita mtetezi wa wanyonge. Huyu tutamkuta na kuwa pamoja nae pale siasa zikienda mrama na pia pale atakapokuwa ametoswa na msomi. Tofauti na hapo yeye hucheza kotekote ilimradi ale. Huyu ndio mshabiki wa mpira mwenyewe.
Yote hayo yanaendelea mhusika mkuu anae elezewa na kutendewa yote hayo ni mtanzania. Ambaye kama angaliamua hakuna wa kumzuia siyo msomi wala mwanasiasa wala watetezi wa aina hii ya hapa kwetu.Mtanzania anaishi kama mpira uwanjani. Anakokotwa huku na huku bila kujua hatima yake ni ipi. Niseme ukweli hapa kuwa tunadharauliwa sana, tunadhalilishwa sana, tunanyanyaswa sana na tunatumikishwa sana. Tumekuwa watumwa wa kifikra na kimatendo ndani ya taifa letu wenyewe.
Mwandishi maarufu wa mashairi na riwaya, Henry Charles Bukowski aliwahi kusema,
"The problem with the world is that intelligent people are full of doubts while the stupid ones are full of confidence".
Kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba tatizo mojawapo katika ulimwengu huu tunaoishi ni kwamba werevu wamejawa na hofu ya kutokujiamini lakini watu wapumbavu wamejawa na moyo wa kujiamini.
Watanzania wasomi na wanaharakati wengi wamejawa na hofu ya kutokujiamini huku wapumbavu wakipita kifua mbele kwa kujiamini mitaani. Hata mpira wenyewe ukichezewa sana mwishowe hutoboka, hupasuka na kuharibika. Ifike hatua tuache kuyumbishwa na mabwana hawa watatu, na tuamue kusimama imara na kupigania haki zetu wenyewe. Si kwa kujumuika na mabwana hawa bali kwa kuwasimamia na kuwaelekeza mabwana hawa.
Ili taifa liendelee lazima liongozwe kimikakati na kwa nidhamu ya kitaalamu. Huwezi ukaamka asubuhi tu, basi kwa kuwa ni waziri wa elimu ukaamua watanzania wote leo waanze darasa la kwanza upya. Haiwezekani. Sera mpya na taratibu mpya za kielimu lazima zifate taratibu za misingi ya elimu inayosaidia watu kuimarisha na kukuza fikra zao na si elimu inayowafunga fikra zao na kuwapotezea muda kuisoma dunia ambayo ni ya nadharia.Sisemi kuwa ni vibaya kuwa na maamuzi mapya bali maamuzi mapya lazima yatolewe kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa na si vinginevyo.
Lugha pekee ambayo kiongozi akiongea mwananchi atamuelewa ni kusema ukweli. Hauwezi ukaja ukatuambia uchumi wa nchi umepanda, makusanyo ya kodi yameongezeka n.k huku hali halisi ya maisha ya mtanzania ni mbaya mbaya siku hadi siku. Je uchumi upi umepanda? Makusanyo ya kodi yametoka wapi? Kwa wauza karanga na mihogo? Kwa wamachinga wanaokimbizana huku na kule na mgambo? Kwa mama lishe? Au kwa makampuni yaliyokuwa yakikwepa kulipa kodi kwa sababu ya sheria na mikataba mibovu ya uwekezaji au kwa kuruhusiwa(kusamehewa)?
Maisha yetu lazima sasa yabadilike, tuende mbele pale inapohitajika na inapoonekana kuwa kuna maslahi yetu sote, tuunge mkono juhudi zote za kweli na zinazoonekana kutuletea maendeleo lakini tusisite kusimama imara na kukataa kuburuzwa kama mpira uwanjani pindi inapohitajika kufanya hivo. Mwanaharakati na mpigania haki za watu weusi Malcolm X aliwahi kusema,
"If you're not careful, the newspapers will have you hating the people who are being oppressed, and loving the people who are doing the oppressing"
Yani kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba, kama hutokuwa makini magazeti yanaweza kukufanya uwachukie watu wanaokandamizwa na uwapende watu wanaofanya ukandamizaji.
Mwisho
Kwa lugha rahisi ni kwamba ili tuachane na maisha ambayo yanafanana na maisha ya mpira uwanjani, watanzania lazima tuwe makini katika kuyachambua, kuyatathimini yale tunayoyasikia ili tuweze kuyafanyia maamuzi. Unaweza ukawa unaamini kitu au mtu flani kwa sababu ya influence ya taarifa kupitia media ilihali hali halisi imefichwa.Tuwe wamoja na tujiamini si kwa kuwa ni wapumbavu bali kwa sababu tuna reasons na misingi ya kujiamini. Maisha ya mpira yabaki viwanjani.
Hasta la victoria siempre
Mwanaharakati huru
@activistyi@yahoo.com.