Huna uhakika wa kula, lakini elfu moja pekee uliyonayo unaamua kuinywea kiroba, hayo ni maamuzi magumu.
Huna hata kitanda unaamua kuoa, hayo pia ni maamuzi magumu.
Huna uwezo wa kumlisha mkeo lakini unampa ujauzito, hayo ni maamuzi magumu.
Shule haina walimu na vifaa vya kufundishia lakini unampeleka mwanao, hayo pia ni maamuzi magumu.
Daladala imejaa mpaka mlangoni lakini unaamua kupanda, hayo ni maamuzi magumu.
Unalipwa mshahara laki mbili lakini unamhonga binti laki moja hayo ni maamuzi magumu.
Kama maamuzi ni kigezo cha URAIS basi Watanzania wote wanafaa kua marais wa nchi hii!!!
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums