Watanzania na imani za ajabu ajabu

Watanzania na imani za ajabu ajabu

Eti mtoto mchanga akijamba ukimcheka unatoka kijipu jichoni
 
Ukimpiga mtoto wakiume na mwiko atakuja kuoa mbali.

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
hebu tujikumbushe imani 'potofu' za jamii mbalimbali hapa nchini.

1.kuna baadhi ya wanawake wa kitanzania wanaamini kuwa njia mojawapo ya kuepuka mimba ni kunywa maji mengi baada ya tendo la ndoa.

2.zamani tuliaminishwa kuwa wazee wengi wa pwani kama kule tanga na bagamoyo wanapata ngiri maji(mabusha) kwa kuwa kuwa ni wanywaji wa maji ya madafu.

3.tulivyokuwa watoto tuliambiwa tusipige mbinje(miluzi) usiku....mpaka leo sababu sijajua ni nini.

...........................

hebu tuwekee imani potofu mbalimbali ulizowahi kusikia kwenye jamii yako

Na hii kwamba mwanamke mjamzito asile mayai imekaaje.

Wazee walizuia kupiga miluzi usiku kwa ajili ya kumjenga kimaadili mtoto miluzi ya nini usiku?? Jaribu kuwaza kuna umuhimu gani kukunja mdomo wako na kufyatua mluzi. Lakini pia miluzi mara nyingi kwa huko vijijini husaidia kuita nyoka sasa hawa wazee walizuia miluzi maana unaweza ukawaita machatu jirani na nyumbani usiku ule mkawa mmetnengeza msiba, wazee waliona mbali sana.
 
Ukiwa na wenzako ukisimama na wao wamekaa eti unawanyonya damu.
 
Kuna hii ya chumvi, usiku haiitwi chumvi bali dawa ya mboga! Sijajua reason behind..
 
ukikuta kuku wanapigana unatakiwa uchomeke kisu chini ili waendelee kupigana
 
kunywesha maji ya walionawa wakubwa zako kabla ya kula ili kukuongezea nguvu
 
1. Kuna kumtemea mate binamu yako unaota vidude vyeusi usoni
2. ukiota moto kimgongomgongo mjomba wako atakufa...
3. Kwenye kuvuna viazi vitamu, ukikikimbilia tu kinaoza
 
Si ruhusa mtoto kula nyama ya utumbo ule wa draft ataota vibarango. 2. Mtoto awe wa mwisho kula nyama 3.kumtengenezea njia kwenye mhindi.
 
Back
Top Bottom