Watanzania na imani za ajabu ajabu

Watanzania na imani za ajabu ajabu

Uda

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2010
Posts
811
Reaction score
623
hebu tujikumbushe imani 'potofu' za jamii mbalimbali hapa nchini.

1.kuna baadhi ya wanawake wa kitanzania wanaamini kuwa njia mojawapo ya kuepuka mimba ni kunywa maji mengi baada ya tendo la ndoa.

2.zamani tuliaminishwa kuwa wazee wengi wa pwani kama kule tanga na bagamoyo wanapata ngiri maji(mabusha) kwa kuwa kuwa ni wanywaji wa maji ya madafu.

3.tulivyokuwa watoto tuliambiwa tusipige mbinje(miluzi) usiku....mpaka leo sababu sijajua ni nini.

...........................

hebu tuwekee imani potofu mbalimbali ulizowahi kusikia kwenye jamii yako
 
Albino hawafi wanapotea.kumbe walikuwa wanauwawa kama wanavyofanya sasa hivi
 
This is very serious.....na ni laazima nikienda kijiji niwaulize wale wazee wa kule.

Mama yangu alinisisitiza sana nkimaliza kupika ugali nsiache mwko ukiwa mchafu hata kwa sekunde,nami ndo nshazoea ila sijui kwa nini
 
This is very serious.....na ni laazima nikienda kijiji niwaulize wale wazee wa kule.

Mama yangu alinisisitiza sana nkimaliza kupika ugali nsiache mwko ukiwa mchafhu hata kwa sekunde,nami ndo nshazoea kama alivo nfundisha ila sijui kwa nini
 
ukiimba huku unakula utaolew mbali........[MENTION][/MENTION]
 
ukiimba huku unakula utaolew mbali........
 
Mama yangu alinisisitiza sana nkimaliza kupika ugali nsiache mwko ukiwa mchafu hata kwa sekunde,nami ndo nshazoea ila sijui kwa nini

Shanny,
Mbona unakuwa kama hujakuwa, hujamuelewa Mama anamaanisha nini?!
 
Ukikojoa mtoni kwenye maji mama yako atakuja kusombwa na maji akivuka mto, pia ukimuua chura ni sawa na kumuua bibi yako
 
1. Usitaje chumvi usiku
2. Nyoka unamwita mzee kijana
3. Ukimruka mtu unamrudia ili asiwe mfupi
4. Jogoo akiwika usiku ujue balaa
5
 
1. Niliwahi kuambiwa nisile chakula huku nikiwa nimesimama nitaoa mbali
2. Niliwahi kuambiwa nisishone nguo wakati nimeivaa nitakufa mapema
3. Niliwahi kusikia pia eti ukifagia uwanja usiku unawafukuza wageni.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom