Watanzania mnataka nini? Mnamtaka nani?

Watanzania mnataka nini? Mnamtaka nani?

Nimeshindwa kuwaelewa Watanzania msimamo wao uko vipi?.... Kwani Mama ana shida tena au ni wanyonge pekee ndio wanaotoa sauti za Vilio hivi huku Wale Walio Juu Wakinyamaza pasi na shaka...

Vilio vile nilivyokuwa nikivisika wakati wa Hayati Magufuli.."Hali Ngumu..Vyuma Vimekaza...Uchumi Unashuka..Utawala w Kibeba"..Nilidhani itakuwa mwisho wake..lakini kinachonishangaza hata baada ya Mama Yetu Kipenzi kushika hatamu siamini kama Machozi yaleyale yaliyokuwa yakimwagika kuwa Hayati Hafai ndio yamefutika kwa Huzuni kumkumbuka au ni Kumnafikia Aliye Kaburini...

Mrisho Mpoto aliwahi "Waliopo hatuwataki wanaotaka Tuwape hatuwaamini"..sasa naona hili linaonekana Dhahiri Hata Huyu wa Sasa Hamumtaki tena au ni Unafiki...Labda Machozi haya ni Ya Muda Tu kutimiza Ile Kauli kwamba "Marehemu hana Baya"

Mliyembeza Kafa Tayari aliyepokea kijiti mmeanza kulia hata Kabla Hajafika mwisho wa Safari...
Vilio vya nini Tena na Mnataka Nini
hufahamiki heading yako na ulichoandika tafrani tupu
 
Nimeshindwa kuwaelewa Watanzania msimamo wenu uko vipi? Je ni kweli tunajua ni kitu gani tunahitaji au ni yupi tunamtaka.....Yawezekana hata tungeongozwa na Malaika bado lawama haziwezi kukoma...


Vilio vile nilivyokuwa nikivisika wakati wa Hayati Magufuli.."Hali Ngumu..Vyuma Vimekaza...Uchumi Unashuka..Utawala w Kibeba". Nilidhani itakuwa mwisho wake..lakini kinachonishangaza hata baada ya Mama Yetu Kipenzi kushika hatamu siamini kama Machozi yaleyale yaliyokuwa yakimwagika kuwa Hayati Hafai ndio yamefutika kwa Huzuni kumkumbuka au ni Kumnafikia Aliye Kaburini...

Mrisho Mpoto aliwahi kusema "Waliopo hatuwataki wanaotaka Tuwape hatuwaamini"..sasa naona hili linaonekana Dhahiri Hata Huyu wa Sasa Hamumtaki tena au ni Unafiki...Labda Machozi haya ni Ya Muda Tu kutimiza Ile Kauli kwamba "Marehemu hana Baya"

Mliyembeza Kafa Tayari aliyepokea kijiti mmeanza kulia hata Kabla Hajafika mwisho wa Safari...
Je Ni Kwamba Tanzania tumekosa Neema Ya Mungu kutupa yule tunayemhitaji Sisi au ni kwa Vile Tuna Unafiki mkubwa kwa Kumbeza KILA anayeshika hatamu ilimradi tu akate tamaa..

Kabla ya Kulalama kwa KILA kukicha Tungejitafakari Je Sisi Tunataka nini!na Je Tunamtaka nani?Ambaye nafsi zetu zinaweza Kuridhika
Hakuna rais anayeingia ikulu na kuondoka pasipo lawama na hii ni tabia ya afrika yote kama sio dunia nzima.

Akiondoka ikulu ndio anayekuwepo anapimwa kwa kumlinganisha na mtangulizi wake na siku zote huonekana hajafikia vigezo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom