Kenya 2022 Watanzania mmepata wapi Uhalali wa Kuusifia Uchaguzi Mkuu wa Kenya wakati Naibu Mwenyekiti wa IEBC na Makamishina Wanne wameyakataa?

Kenya 2022 General Election

Cognizant

JF-Expert Member
Aug 13, 2022
491
1,056
'Kama Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC pamoja na Makamishina Wanne wa Tume hatukubaliani na Matokeo ya Uchaguzi kwani hatujashirikishwa katika hatua Muhimu ya Uhakiki wa Nyaraka na tumemshangaa mno Mwenyekiti Wafula Chebukati Kumtangaza William Ruto kuwa ndiye Mshindi' amesema Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC nchini Kenya.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia na U Magazene ya Uhai FM.
 
Uchaguzi wa Kenya ulikuwa huru na wazi, na yoyote yule anayeona haki haikutendeka anao uamuzi kwenda mahakamani kuhoji ili kupata haki yake.

Vitu vyote hivyo viko kwenye katiba yao na vimefanyika vyema kwenye uchaguzi wao.

Tanzania hatuna uchaguzi unaozingatia hivyo vitu vitatu (Huru, Wazi na Haki).
 
Ktk siasa MUNGU huwa mbali sana na wanasiasa - Uhuru, haki na uwazi viko ktk kipimo cha siasa si biblia wa kuruani.
 
'Kama Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC pamoja na Makamishina Wanne wa Tume hatukubaliani...
Ukumbuke kuwa uzuri wa tume ile unabaki palepale tatizo ni moja tu kuwaingiza wanasiasa ndani ya tume huku wakiwa wamebeba watu wao.

Uwazi wa uchaguzi Kenya hauna mashaka kabisa ni mfano wa kuigwa hasa kwa wapenda Amani na Haki.
 
'Kama Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC pamoja na Makamishina Wanne wa Tume hatukubaliani...
Ukiwa wewe si mpenzi wa HAKI na AMANI Basi huu uchaguzi wa kenya utakufaa nini.

Watu wajinga na Wapumbavu huwa wanategemea mambo mabaya yawakute ndio wajue umuhimu wa kutenda haki na kuheshimu maamuzi ya watu.

Tanzania tujifunze tungali tuna akili ili tusichanganyikiwe tukashindwa kujua nn cha kufanya huko mbeleni.
 
'Kama Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC pamoja na Makamishina Wanne wa Tume...
1. The whole idea and rationale of having an independent electoral commission is to have a commission which is free from govt intervention but also a 100% impartial committee which shall stand for no one but the true results of the elections results lakini hapa what can we see?

1. Three returning officers go missing nothing is done

2. Returning officers disappear with ballot boxes still no answer from IEBC no strict measures taken.

3. The public portal which we all wanted to believe is 100% protected, kumbe it’s not and reported that may be was hacked or attempted to hack.

4. Unsecured computer reported to be infiltrated in the portal system but then rechecked and was removed and confiscated by the IEBC for further investigation and examination 😃

5. Last one which is an obvious irregularity, out of 7 commissioners, 4 of them have defected from IEBC, they have stated that they will speak on the their reasons later

Mahakama again will come into picture to either determine the tallying process or a re-election on presidency.
Let’s wait and see
 
Dunia nzima hakuna kutangazwa mshindi baada ya mshindi kujulikana ,anachofanya Odinga ni kujitekenya na kucheka mwenyewe.

Odinga alichofanya ni Kama alichofanya Hayati Seif alipoona kashindwa akaamua kujitangaza mshindi na huo ndio ukweli mchungu Odinga alidhindwa akaamua kushinikiza uongo uwe ukweli.

Sometimes uwa tunajitoa ufahamu kufikiri yasiyowezekana yanaweza kutokea kimiujiza, Ruto ni Rais aliyeandaliwa na mbingu kuiongoza Kenya na mbingu ikiamua hakuna wa kutengua.

Haya ndio makosa yaliyofanywa na Odinga na yamemgharimu pakubwa Sana.

Kwanza, kumpendekeza mpagani kuwa mgombea mwenza. Hapo ni Kama alijaribu uweza Mkuu wa Mungu. Sote tunajua Rais anapofariki makamu anakuwa Rais kwa matakwa ya katiba ya kenya hivyo ingetokea kwa mapenzi ya Mungu Odinga angetwaliwa basi ikulu ingeongozwa na mpagani. Mungu saidia CCM tusiwaze kuteua asiyeamini Mungu kuwa mgombea.

Pili, Sera za Ruto zilijikita katika maisha ya wakenya wa chini Sana kwa mfano Kama ile ya kuahidi kusimamia rasilimali za nchi kwa faida ya wakenya wote. Kama ilivyokuwa kwa Hayati Magufuli 2015 ahadi zake zilijikita katika kuijenga Tanzania. Watu wanaguswa na kiongozi aliye tayari kupambana kwa niaba yao.

Tatu, Nguvu za Ruto kisiasa. Ili Kenyatta ashinde alihitaji mtu mwenye nguvu Sana kwa siasa za Kenya na huyo hakuwa mwingine bali ni Ruto pia Kenyatta na Odinga wanalijua Hilo. Kwa hiyo Ruto anaweza kubezwa lakini ndani yake kuna nguvu Sana na nguvu hii inatokana na Imani na hofu ya Mungu.

Nne, Umri wa Odinga ulikuwa changamoto. Tukiachilia mbali nchi zilizoendelea kuchagua mtu mwenye umri wowote kwa nafasi ya Umri, kwa nchi zetu zinazoendelea kigezo Cha umri kinazingatiwa Sana na hii ni kwa Sababu umri mkubwa kwa Afrika una changamoto nyingi.

Tano, Ruto alikuwa ni Naibu Rais. Nakumbuka Mwalimu alikuwa anapenda Sana waziri Mkuu na mwanadiplomasia nguli Salim awe Rais baada yake lakini Getruda Mongela akaja na hoja iliyobadili upepo wa Salim kabisa na kumbeba mzee Mwinyi ambaye alikuwa makamu wa Rais kipindi hiko, alisema " Dunia itatushanga tukimchagua waziri Mkuu na kumwacha makamu wa Rais". Kwa kanuni hiyo hiyo wakenya ndio wameitumia kwamba wasingeweza kumwacha makamu wakamchagua waziri mkuu
 
Dunia nzima hakuna kutangazwa mshindi baada ya mshindi kujulikana ,anachofanya Odinga ni kujitekenya na kucheka mwenyewe...
Hapo kwenye mpagani umebugi step mkuu!

Tulipata kiongozi akaonekana mcha Mungu wa kweli maana kila siku Kanisani mstari wa mbele na kamera zinamfuata huko.

Hata kapu la sadaka alibeba lakini kipindi chake ndio watu waliuwawa wengi kimaajabu, kupotea na wengine kupigwa risasi hadharani mchana na akazuia uchunguzi.

Ni bora ya mtu mwema Mpagani kuliko "muumini" atendaye kama shetani
 
Kuna nchi yeyeto imepongeza ushindi wa uraisi kama Hakuna jua ngoma bado mbichi. Pana vita Kati ya nguvu ya giza na nuru, lakini nuru atageuka mshindi
 
Back
Top Bottom