WaTanzania hawazitaki Tume za Uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WaTanzania hawazitaki Tume za Uchaguzi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwiba, Oct 1, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  “Sisi tumeambiwa maandamano haya ni hadi ofisi za msajili wa vyama, nyinyi polisi kwa nini mnatulazimisha kwenda kidongo chekundu? Alihoji mwandamanaji mmoja wakati anajibishana na afisa wa polisi.

  “Sisi huko kidongo chekundu hatuendi,” alisikika mwandamanaji mwingine na baada ya kuona hivyo polisi iliongeza ulinzi.

  “Mnatuonea sisi kwa nini mnatuzuia tusiende ofisi ya msajili, pale kidongo chekundu ndiko kuna ofisi yake…sisi tumeandamana kwa haki hivyo tunataka haki yetu,” alisema mwandamanaji mwingine huku akipaza sauti kuelekea kwenye gari la polisi.

  “Nawashangaa hawa wenzangu yaani pale walikuwa wanasubiri Profesa Lipumba atuamuru twende mbele, haiwezekani yule ni kiongozi hawezi kusema na tena keshachoka na mambo haya
  sisi ndio wenye nguvu tunapaswa kupambana,” alisema mwandamanaji mwingine.

  “Unajua tumefanya makosa sana kusimama pale, sisi tungekomaa tu hata kama wangepiga mabomu ya machozi hatuna cha kupoteza ni
  heri kufa wakati unadai haki,” alisema.

  [​IMG]

  Nawashangaa hawa wenzangu yaani pale walikuwa wanasubiri Profesa Lipumba atuamuru twende mbele, haiwezekani yule ni kiongozi hawezi kusema na tena keshachoka na mambo haya.
   
Loading...