Watanzania hatuna msimamo

Watanzania hatuna msimamo

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,834
Reaction score
15,626
Tatizo kubwa sana sasa kwenye nchi yetu sio wanasiasa bali ni Watanzania wote kwa ujumla kama nchi. Watanzania tumekuwa nchi kama mpya vile wengi wetu ni wavivu wa kufikiri, washabiki wa mambo yasiyo na tija kwa nchi na hatari na hatujui tunataka nini.

Kwenye nchi nyingi kuna misimamo ya wananchi mfano DRC wanataka uchaguzi huru, China wananchi hawajali siasa wao ni uchumi imara, US demokrasia ya watu na haki. Je sisi tunasiamama kwa lipi ambalo tunawaonyesha wanasiasa au mtu yeyote kwamba hapa tuna umoja. Je tunasimama kwa katiba ya nchi? Wakati tunaona katiba ina kiukwa waziwazi na hatusemi chochote, Je tunasimama kwenye demokrasia? Mbona tunaona demokrasia inakiukwa waziwazi bila kufanya lolote, Je tunasimama kwa uchumi? Mbona wafanyabiashara wana nyanyaswa bila kusema lolote mfano kodi, maduka kufugwa na kulipishwa laki saba kabla hata ya kipato ukifungua duka. Je tunajali Utanzania na uraia? Mbona kuna wenzetu kisiasa tu wanaambiwa sio raia na tumenyamaza wengi. Je ni usalama? Mbona wabunge wanapigwa risasi, wafanyabiashara wanatekwa bila kusimama pamoja.

Tatizo letu tunategemea wanasiasa watuletee mabadiliko wakati wenyewe ndiyo wameleta hayo matatizo. Sasa Watanzania kwa serikali tumekuwa kama houseboy mvivu ambaye anapelekwa tu lakini naye hawazi kufanya maamuzi. Tumekuwa na uzuba wa hali ya juu. Tusikokuwa waangalifu itachukuwa miaka mengi kurudisha nchi yetu pazuri. Hatuwezi kulalamikia wanasiasa ambao wanafuata wananchi na wananchi hawaeleweki misimamo yao
 
Watanzania hatujielewi, enzi za JK demokrasia ilikuwa juu mno watu wakakejeli wakisema nchi inahitaji mbabe.

Sala zikajibiwa na Mungu, kaja mbabe ambaye ana hamu kuona nchi inapiga hatua, tumerudi kule kule kwenye akili za kutaka demokrasia pana.

Wabongo ni watu wasioridhika, siku zote kuna mtu mahali fulani ambaye ndio chanzo cha shida walizonazo, kwamba wao ndio tatizo la kwanza la msingi kabla ya hizo shida, hilo ni wazo ambalo halipo vichwani mwao.
 
Matatizo yetu ni makubwa zaidi.kuanzia akilini,rohoni hadi mwilini.Tuko kama wale wadudu kama minyoo ukimgusa mbele anarudi nyuma ukimgusa nyuma anaenda mbele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo kubwa sana sasa kwenye nchi yetu sio wanasiasa bali ni Watanzania wote kwa ujumla kama nchi. Watanzania tumekuwa nchi kama mpya vile wengi wetu ni wavivu wa kufikiri, washabiki wa mambo yasiyo na tija kwa nchi na hatari na hatujui tunataka nini.

Kwenye nchi nyingi kuna misimamo ya wananchi mfano DRC wanataka uchaguzi huru, China wananchi hawajali siasa wao ni uchumi imara, US demokrasia ya watu na haki. Je sisi tunasiamama kwa lipi ambalo tunawaonyesha wanasiasa au mtu yeyote kwamba hapa tuna umoja. Je tunasimama kwa katiba ya nchi? Wakati tunaona katiba ina kiukwa waziwazi na hatusemi chochote, Je tunasimama kwenye demokrasia? Mbona tunaona demokrasia inakiukwa waziwazi bila kufanya lolote, Je tunasimama kwa uchumi? Mbona wafanyabiashara wana nyanyaswa bila kusema lolote mfano kodi, maduka kufugwa na kulipishwa laki saba kabla hata ya kipato ukifungua duka. Je tunajali Utanzania na uraia? Mbona kuna wenzetu kisiasa tu wanaambiwa sio raia na tumenyamaza wengi. Je ni usalama? Mbona wabunge wanapigwa risasi, wafanyabiashara wanatekwa bila kusimama pamoja.

Tatizo letu tunategemea wanasiasa watuletee mabadiliko wakati wenyewe ndiyo wameleta hayo matatizo. Sasa Watanzania kwa serikali tumekuwa kama houseboy mvivu ambaye anapelekwa tu lakini naye hawazi kufanya maamuzi. Tumekuwa na uzuba wa hali ya juu. Tusikokuwa waangalifu itachukuwa miaka mengi kurudisha nchi yetu pazuri. Hatuwezi kulalamikia wanasiasa ambao wanafuata wananchi na wananchi hawaeleweki misimamo yao


Nilisema hili 2019 sasa naona tuna amka. Salamu kwa Sirro, Polepole, Kinana, President Samia. Mpaka Raisi kasema jana IGP Sirro alikuwa hajui Dunia imebadilika!.
 
Back
Top Bottom