Watanzania bara hawana udini

Sijawahi kumwona au kumsikia Mkristu anayemchukia mtu wa dini nyingine(naowajua); ila nimewasikia wengi wa upande mwingine na ghadhabu kabisa na kuapiza chuki iliyopo. "The Fire in the eyes" inatisha sana
Upo Jf gani ?

Jf Wakristo ndio wanaongoza kwa nyuzi za chuki na kusimanga Uislamu na Kuna mpaka ID special kwa kazi hiyo.

Kipindi cha nyuma ukija Uzi wa Sheikh kulawiti dakika chache wanajaa Wakristo wakifurahia ,kutukana mpaka kuvuka mipaka kusema ndio mafundisho yao nk. Lakini Uzi ukija kuhusu Padri kufanya kitendo hikohiko Uzi unapoa na wanasema hayo sio mafundisho ya ukiristo.

Mimi binafsi nilikuwa naamini Wakristo ni watu poa hawana chuki kivile ni kawaida na wachache sana , ila Imani hiyo ilinitoka baada ya Kuna Jf humu ndio nimeshuhudia live yaliyomo vifuani mwao unakuta jukwaa la Habari na Hoja Mchanganyiko lote zimajaa nyuzi kuhusu Uislamu na kuusema kwa chuki.
 
Kilichopo ni kuomba wazalendo kupata ujasiri, maana wahuni ni wachache na nguvu yao ni katiba.

Shida ni ustaarabu, na mjinga ukijifanya mstaarabu atakufanyia abuse.

Tayari washaonyesha hiyo abuse of power kutokana na katiba (kama mimi na wewe tunaona) na wao wameona.

Ni swala la tolerance na loyalty ya mustakabali wa kiapo cha walio wengi kuilinda Tanzania.

Wizi auzuiliki serikalini, lakini kuna abuse za madaraka za wazi; kuna uvumilivu na kukosekana kwa vyombo vya ulinzi.

Una sababu gani ya kununua G Wagin wakati kwa nafasi yako serikali inakupa luxury land cruiser na escort.

Akili za kipuuzi tu na tamaa za mali kwa walinzi wa taifa.

Waibe tu no one cares, lakini kuacha taifa litumbukie kwenye udini kisa mali. Hiyo ni adhabu ya kitanzi (ni usalitI uliotukuka)
 
Ingependeza media zingeacha kurusha maudhui ya mtu au kikundi chochote kinachozungumzia udini. Ni bahati mbaya sana waliotuletea dini wao kwa wao wanagombana tena wa dini moja. Sisi amani ilijengwa katika misingi ya kitaifa na sio katika misingi ya dini.
 

Ili kujenga taifa upya, uzalendo, uadilifu, uaminifu, haki, ukweli, katiba mpya inayotetea wananchi ni lazima tuliondoe hili genge la wahuni la Samia, Kikwete, Rostam.
 

Hakuna media Tanzania zote zimefungwa. Ukiwa mbishi unatekwa.

Wahariri katika mkutano wao na Mwigulu Mchemba walimwambia ukweli.
 
Kwa sababu kuna genius mmoja ambae kaanzisha forum ambae katukasanya watu wenye interest tofauti.

He is also supposedly all knowing hata kama hana media knowledge, kuelewa madhara ya narrative, ideology and target audience.

Watu wamelalamika sana kuhusu contents za udini; hasa ukienda jukwaa la international. Kuelewa ukubwa wa tatizo inataka na abc ya huduma unayotoa.

Hata wanaelewa basi JF contribution yao kwenye kuchochea udini; probably hakuna hata moderator mmoja ambae kasoma maswala ya media.

Kuwaeleza hawa watu this is wrong for the society ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
 
Hao ni wachache sana, njoo huku mtaani utaona watu wengi hata hawana muda na hizo dini
 
Hao ni wachache sana, njoo huku mtaani utaona watu wengi hata hawana muda na hizo dini

Sidhani kama kuna familia ya Tanganyika haina muingiliano wa kuoana, undugu. Huwezi kutaka kumuua mjomba, Baba yako, mke wako.

Haya ni mambo tunaletewa na Abdul, Samia, Kikwete kutugawanya ili watutawale. Divide and rule.
 
Sijasoma jukwaa lolote lingine zaidi ya siasa, ila hii ya ku-discuss hapa, ni hisia za kufikirika tu, watu wanadhani, siyo ya moyo. Ila ukiona Mufti au Padri au Sheik anatoa mishipa na macho yanawaka moto hapo ndiyo udini. Kama alivyosema Quimby hapo juu, kwa Tanzania ya sasa sioni huo udini kwa waTanzania. Halafu kiukweli kwa nini uumie moyo, dini siyo kama race au wazazi au asili, dini zililetwa na ni imani, ukifikiria sana ukweli ndani ya dini zote ni swa tu, labda ondoa dini uisjifunge na dini, amini Mungu tu si sawa tu? Tunakuwa watumwa kwa uoga ambao hatuujuwi. Fear of unknown, ukiuliza sana unaambiwa unakufuru, na unaovyoona mauti, unatishika.
 
Hawataweza
 
Unapokuwa moderate na mambo ya dini huwezi kuweka akili yako sana kwa viongozi wa dini wanasema nini, unakuwa na akili huru,, akili huru haina ubaguzi wa kidini
 
Kabisa nimekulia magomeni kagera asilimia 99 ni Muslims lakini sijawahi baguliwa na ukristo wangu
 
Kabisa nimekulia magomeni kagera asilimia 99 ni Muslims lakini sijawahi baguliwa na ukristo wangu
Mitaa hiyo hiyo hata tofauti ya John na Juma hakuna.

Kifupi ni kwamba sehemu nyingi Tanzania udini hakuna.

Hii social division inalelewa na wanasiasa wa hovyo na media (including JF).

Vinginevyo wengi wetu humu tuna marafiki wa dini tofauti nasi na tunaheshimu taratibu zao; ambazo haziasiri ukaribu wetu wa kila siku.

Na wengi tuna ma-best ambao ni dini tofauti na sisi; na tume kuwa tukiheshimiana kwa miaka.
 
Hao hao ndio wanaongoza hapa Jf kwa nyuzi mbaya na maneno machafu ya kidini pamoja na dhihaka.

Tunachekeana tu moyoni chuki zimetawlaa
Wewe bado ni muislamu πŸ™„πŸ™„! ...matatizo ya kufuata dini kitumwa ndiyo haya ...yaani unafuata Dini kwa sababu baba na mama yako ni hiyo dini !! Je mtu wa hivyo anayo haki ya kuwa elekeza au kuwa kosoa watu kuwa dini zao siyo sahihi ikiwa yeye mwenyewe msingi wa kuamini dini yake kuwa ni ya kweli ni kutokana na kuzaliwa na wazazi wenye hiyo dini ? Swali ninalo taka kukuuliza mfano wewe adriz je ukitambua kuwa kweli kabisa Yesu ndiye Mungu utafanyeje mbele ya wazazi, na familia na waislamu wenzio...?

na kuuliza ili swali ili MTAMBUE KIFUNGO CHA UPUMBAVU AMBACHO WAKRISTO NA WAISLAMU MMEJIFUNGA TOFAUTI NA MIMI AMBAYE NAUTAZAMA UKWELI KWA KUTUMIA AKILI KABLA YA KUSEMA DINI SAHIHI NI IPI...SIONGOZWI NA DINI ZA KURITHI.
 
Your browser is not able to display this video.


☝️Dhabi ya ubaguzi ukishaanza aina mipaka

Sote wamoja; wanasiasa wasitugawe kwa tamaa zao kupitia udini, ukabila wala rangi.

Viva Tanzania πŸ‘‹
 
Kuna namna fulani mimi naamini kiongozi mkuu wa chombo chochote cha usalama hatakiwi kuwa ametoka kwenye background ya maskini..

...ni rahisi sana mtu aliyekulia maisha ya kimaskini kupumbazika na pesa nyingi ambazo hakuwahi kuzishika huko nyuma na kiasi cha kuvunja kiapo chake bila kujali athari zake.

..Suleiman Mombo,Jacobo Mkundu na Camillius Wambura kwa jinsi Samia na mtoto wake walivyowageuza mazezeta kwa rushwa za mabilion wanazowapa, nina amini kabisa hawa watatu wameishi kwenye maisha ya kimaskini sana katika makuzi yao.

Ndio maana wamekubali sio tu kuliweka usalama wa taifa rehani, bali hata kutweza utu wao kwa kumnyenyekea na kumtii Abdul ambao kimsingi nina uhakika wanaweza kumzaa...

...hakika pesa mwanaharamu, yaani mababa mazima yamekubali kubeba lawama zote za watanzania 67m+ hili tu bank accounts zao zisome mabilioni hili kuilinda hii first familiy haramu iendelee kubagaza taifa la watanganyika.

Ila kwa hii katiba kweli baba wa Taifa alituweza.
 
Yaani kweli kabisa sisi watanganyika hatuna vita za udini, Wazee wetu walitulea hivyo.Shule za kikristo tumesoma na waisilamu pamoja, Hospitali za waislamu wakristo tumetibiwa bila ubaguzi na tunashirikiana katika shughuli zote za maendeleo ya jamii yetu.Vikundi vya vikoba mama zetu wanashirikiana dini zote kwa umoja na upendo.
Tunaishi kwa kuheshimiana sana kwenye maswala ya Imani na kuna wakati hata katika sherehe zetu za kiimani tumesheherekea pamoja na kula pilau Pamoja. Na pia waislamu na wakristo hufunga ndoa pamoja.Hivyo zipo familia nyingi zenye waislamu na wakristo wanaoishi nyumba moja,na imekuwa hivi kwa miongo mingi.
Sasa kuna watu wenye chuki na wivu na Tanganyika, wivu wao ni juu ya umoja tulionayo na uhuru wetu wa kiimani. Watanganyika tunaheshimiana na tunapozungumzia maswala ya kijamii tunazungumza kwa hoja sio kwa udini au ukabila.
Watanganyika hatuna ardhi nyingine yakukimbilia ,Mungu alitupa Tanganyika, waislamu na wakristo Tanganyika ni yetu sote.Viongozi wetu wa dini zungumzeni kwa hoja za msingi, teteeni haki ya taifa letu.Yeyote atakayeleta ugomvi wa kidini tumkemee kwa nguvu zote.Hiyo mbegu ya udini tunaikataa haitapandikizwa kwenye ardhi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…