Wana JF hii ni hatari kwa matarajio na ndoto za kutokomeza vitendo vya kinyama na ubadhilifu hapa nchini. Kuna mambo mengi sana ya unyanyasaji,ufisadi,ubadhilifu na usultan hapa nchini. Hii inajirudia kwa watanzania kila linapotokea jambo moja tunalipigia kelele kwa muda mfupi na kulitupilia mbali hata kama halijarekebishwa.
Ilipotokea ubadhilifu na mikataba ya ulaghai ktk shirika la umeme na kampuni ya Richmond,ikaja, epa,dowansi na mingine mingi tulipiga kelele na kuacha bila hata kutatua tatizo,ikaja mawaziri kula rushwa mf wizara ya utalii,wizara ya nishati na madini,wizara ya fedha na wizara nyingine tumenyamaza huku watuhumiwa wakiishia kuachia ngazi bila kufilisiwa. Haya vikaja vitendo vya kinyama dhidi ya binadam kwa watu kuuawa,mf mauaji ya igunga,ruvuma,singida,arusha,dr Ulimboka, Ally zona, na Mwangosi.
Tumekuwa maarufu kwa kupiga kelele jamvini bila kuchukua hatua stahiki ili kuinusuru Tanzania kwa vitendo hivi haramu. Wito kwa watanzania wote ni kwamba tuwe tunaongea na kufuatilia na kuhimizana ili kutokomeza vitendo hivi hapa nchini. Hata watawala ona sasa Baba anakuwa mwenyekiti wa chama, Mama mjumbe wa Nec na mtoto ni Mjumbe wa Nec je,hivi kweli hii ni demokrasia? Maana hapo yatafanywa maamuzi ya kifamilia katika masuala nyeti ya kitaifa.
Naomba tuungane kuupinga utawala huu wa kisultani. Kukaa kwetu kimya kutawapa kiburi watawala kwani watajua kuwa huwa tunaongea kwa muda mfupi na kutoweka, naomba tusiwe watu wa kupigia kelele matukio na kuayasahau bila majawabu.