Watanzania Afrika Kusini

Mchagaa

Member
Jul 31, 2007
20
5
Wenzangu wana JF,

Nina binamu yangu mwanafunzi chuo cha UNISA anayekaa Johannesburg sasa ni miaka minne. Jambo la kushangaza anadai eti hajapata kuwaona Watanzania jijini Johannesburg. Wale anaowakuta ni watanzania mjini wanaouza viazi, vitungu, nyanya na kadhalika. Swala lake ni hili: Hamna wanaofanya kazi maofisini au hamna hata vyama vya watanzania jijini? Alipokuwa london, Watanzania kibao. Anasema eti inaonekana watanzania hawapendi sana kuja Afrika Kusini. Anadai akienda maofisi mengi tu yani coperate world, Wakenya kibao. Kasema Wakenya ni wachache London, lakini ukienda America, kila State eti hukosi Wakenya. Inakuwaje? Na kama wapo huko SA, ni mahali gani wanajificha ili naye ajitumbukize humo.

Siku njema.:):confused:
 
Nina binamu yangu mwanafunzi chuo cha UNISA anayekaa Johannesburg sasa ni miaka minne. Jambo la kushangaza anadai eti hajapata kuwaona Watanzania jijini Johannesburg. Wale anaowakuta ni watanzania mjini wanaouza viazi, vitungu, nyanya na kadhalika. Swala lake ni hili: Hamna wanaofanya kazi maofisini au hamna hata vyama vya watanzania jijini?

Mkuu Mchagaa, huyo binamu yako anataka tu watanzania wanaofanya kazi ofisini?, ina maana hao wafanyabiashara sio waTZ ama kwakuwa wanafanya biashara ya viazi, vitunguu, nyanya, alitaka wale wanaofanya biashara za magari, TV nk. Hao wafanya biashara ndio ndugu zake akiwa huko, na nadhani haohao ndio wangeweza kumuonesha waTZ wengine wa maofisini. Kama kweli kutakuwa hakuna chama hapo J'burg cha waTZ, alitakiwa ashirikiane na hao wafanya biashara kukianzisha, UMOJA NI NGUVU.
 
Mwenzangu,
Usimwelewe vibaya. Nafikiri katika field yake, ilibidi atafute wenzake ambao wapo ofisini ili wasaidiane kimasomo pia. Wale wanaouza barabarani, tayari anawafahamu tena sana maana supply yake ya mboga, anaipate maeneo hayo hayo. Ila hawana idea kuhusu vyama au wananchi wengine mjini. Usije ukakosa kumwelewa vizuri.

Siku njema mwenzangu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom