Watanzania 12 waliovuma 2012...!

Watanzania 12 waliovuma 2012...!

Olaigwanani lang

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
547
Reaction score
183
Ifuatayo ni orodha ya watanzania 100 waliovuma zaidi mwaka 2012, kulingana na utafiti maalum uliofanywa na NIPASHE kwa kuangalia majina ya Watanzania yaliyoripotiwa zaidi na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi, kitaifa na kimataifa. Utafiti huu wa mwezi mmoja ulirejea taarifa kupitia mtandao na tovuti maarufu kama Google, Yahoo, Facebook na Twitter.

1. Jakaya Kikwete: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kama alivyo baba mwenye nyumba, jina lake lilitajwa kila mambo mazito yalipotokea nchini.

Baadhi ya makubwa yaliyojiri ikiwemo kulaumiwa kutokana na kukithiri kwa ugumu wa maisha ya watanzania na matukio ya migomo ya madaktari, utekwaji wa Dk. Ulimboka, mauaji ya mwandishi wa habari wa Channel 10, David Mwangosi, ghasia za kisiasa na kidini, uteuzi wa majaji, mgogporo wa Ziwa Nyasa na kadhalika.

Alisifiwa katika uundwaji wa Tume ya Katiba, uteuzi wa Baraza jipya la mawaziri alioufanya baada ya kujiuzulu mawaziri wanane mwanzoni mwa mwaka, uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara, uvumilivu wa kisiasa, mabadiliko katika safu ya juu ya CCM, na kadhalika.

2. Steven Kanumba: Msanii maarufu wa filamu nchini Tanzania alifariki usiku wa kuamkia Aprili 7, 2012 akiwa na msanii mwenzake Elizabeth Michael ‘Lulu’. Msiba wake uligharimu takribni sh.milioni 52. Ulikuwa moja ya misiba mikubwa zaidi katika historia ya Tanzania, ukikaribia ule wa Mwalimu Julius Myerere mwaka 1999, hayati Edward Sokoine mwaka 1984, hayati Abeid Amani Karume mwaka 1972 na hayati Rashid Kawawa mwaka 2010.

3. Dk. Steveni Ulimboka: Aliteswa vibaya katika msitu wa Pande alikopelekwa baada ya kutekwa kutoka katika eneo la Leaders Club, Kinondoni Dar es Salaam. Hata hivyo, kwa kudra za mwenyezi Mungu aliokolewa na Juma Mgaza, Msamaria mwema aliyefanya tendo la kijasiri la kumchukua na kumpeleka hospitali

4. Elizabeth Michael ‘Lulu’: Jina lake lilivuma sana tangu siku Steven Kanumba alipopoteza maisha na baadaye, Aprili 11, Lulu akasomewa mashtaka ya kuhusika na kifo hicho. Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 5 iliyopita, jina la Lulu ndilo likawa la msanii wa kwanza wa kike kulipita lile la Wema Sepetu kwa kuandikwa ama kuzungumzwa mara nyingi zaidi nchini.

5. Daudi Mwangosi: Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel 10 ambaye Septemba 2012 aliuawa kwa bomu/risasi na polisi huko Iringa wakati wa mkutanowa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tukio hili lilisababisha simanzi, malalamiko, maandamano, kupungua kwa imani ya raia kwa polisi na hatimaye kuundwa kwa Tume mbili tofauti za uchunguzi wa jambo hilo.

6. Edward Lowassa: Waziri Mkuu zamani wa Tanzania aliyelazimika kujiuzulu wadhifa wake kwa kashfa ya Richmond na Mbunge wa Monduli alivunja ukimya Machi 15, 2012 aliporejea kutoka matibabu nchini Ujerumani na kusema kuwa yuko fiti kisiasa. Baadaye akashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Halmashauri Kuu ya CCM na jina lake likazidi kung’ara kama mmoja wa wale wanaotishia kwa kasi uteuzi wa mgombea Urais kupitia CCM na imefikia wakati sasa gumzo mtaani ni swali kwamba kama kuna ‘mbabe’ ndani ya CCM anayeweza kupambana naye kwa namna kasi yake inavyozidi kutisha.

7. Sheikh Ponda Issa Ponda: Mwenyekiti wa Shura ya Maimamu alivuma kila mara madai, maandamano, ghasia na tafrani za waumini wa Kiislam zilipotajwa, pamoja na kesi ya jinai dhidi yake ambayo inaendelea ilipotajwa mahakamani. Aliongoza pia jaribio lililokwama la kuhamasisha Waislam wasishiriki zoezi la Sena lililofanyika kote nchini Agosti 26.

8. Sheikh Farid Hadi Ahmed (Kiongozi wa Kundi la Uamsho Zanzibar): Tuhuma za utekwaji wake nyara zilisababisha machafuko na kuuawa kwa watu Zanzibar katikati ya mwezi Oktoba. Baadaye alionekana, kukamatwa na kushtakiwa kwa kesi za kuhatarisha amani ya nchi.

9. Wema Sepetu: Kwa miaka mitano hivi sasa jina la Wema Sepetu limeendelea kuwa na mvuto miongoni mwa wafuatiliaji wa masuala ya filamu na skendo za wasanii. Kama kawaida, jina lake liliendelea kupamba na ‘kuuza’ katika magazeti mbalimbali.

10. Godbless Lema: Mbunge machachari wa CHADEMA aliyerejesha Ubunge wake wa jimbo la Arusha Mjini Desemba 2012 baada ya Mahakama ya Rufaa kutokubaliana na hukum ya Aprili 5, 2012 ya Jaji Rwakabalira aliyempokonya Lema ubunge huo.

11. Zitto Kabwe: Alivuma kama miaka yote tangu alipoanza siasa na hasa shinikizo aliloliongoza kupinga matumizi mabaya ya fedha za umma na hivyo kuanza mchakato bungeni wa kukusanya saini 70 za wabunge sawa na asililimia 2, Aprili 19, ya idadi inayohitajika kukidhi kifungu cha 133(1) cha Kanuni za Bunge kinachohusika na uletwaji hoja rasmi ya kumwajibisha Waziri Mkuu kwa kutokuwa na imani naye. Jambo hili lilichangia kujiuzulu Mawaziri wanane. Alizidi kutajwa pia Urais wa 2012..

12. Tundu Lissu: Mwanasheria na mwanasiasa huyu machachari aliyetamba sana 2012. Nyota yake iling’ara zaidi alipoongoza timu ya mawakili iliyofanikisha kulishawishi jopo la Majaji watatu wa Mahakama kuu kutengua hukumu ya jaji Gabriel Rwakabalila iliyokuwa imempokonya Ubunge mbunge Godbless Lema wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA. Lissu mwenyewe Aprili 26, 2012 alifanikiwa kulitetea jimbo lake baada ya kushinda kesi ya pingamizi dhidi yake iliyotupiliwa mbali na jaji Moss Mzena wa Mahakama Kuu. Lissu tena alisikika kwa nguvu Julai 13, 2012 kwa kumshambulia Rais Kikwete kwa tuhuma za kuteua Majaji wa Mahakama Kuu wasiokidhi viwango vya kitaaluma na utendaji kazi. Halafu akataja hadharani bungeni majina ya wabunge aliowatuhumu kuhusika na rushwa ndani ya Kamati ya Nishati na Madini.

Ripoti ya Jenerali Ngwilizi haikuona kashfa yeyote kati yao kuhusika.
SOURCE:Nipashe
 
Acheni vituko bila kuniwekea dk slaa skubalii huu utafiti
 
Nape Nauye na Anna Makinda vipi?
 
Kafunikwa na lulu na wema sepetu.

Acheni vituko bila kuniwekea dk slaa skubalii huu utafiti

Ifuatayo ni orodha ya watanzania 100 waliovuma zaidi mwaka 2012, kulingana na utafiti maalum uliofanywa na NIPASHE kwa kuangalia majina ya Watanzania yaliyoripotiwa zaidi na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi, kitaifa na kimataifa. Utafiti huu wa mwezi mmoja ulirejea taarifa kupitia mtandao na tovuti maarufu kama Google, Yahoo, Facebook na Twitter.

1. Jakaya Kikwete: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kama alivyo baba mwenye nyumba, jina lake lilitajwa kila mambo mazito yalipotokea nchini.

Baadhi ya makubwa yaliyojiri ikiwemo kulaumiwa kutokana na kukithiri kwa ugumu wa maisha ya watanzania na matukio ya migomo ya madaktari, utekwaji wa Dk. Ulimboka, mauaji ya mwandishi wa habari wa Channel 10, David Mwangosi, ghasia za kisiasa na kidini, uteuzi wa majaji, mgogporo wa Ziwa Nyasa na kadhalika.

Alisifiwa katika uundwaji wa Tume ya Katiba, uteuzi wa Baraza jipya la mawaziri alioufanya baada ya kujiuzulu mawaziri wanane mwanzoni mwa mwaka, uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara, uvumilivu wa kisiasa, mabadiliko katika safu ya juu ya CCM, na kadhalika.

2. Steven Kanumba: Msanii maarufu wa filamu nchini Tanzania alifariki usiku wa kuamkia Aprili 7, 2012 akiwa na msanii mwenzake Elizabeth Michael ‘Lulu'. Msiba wake uligharimu takribni sh.milioni 52. Ulikuwa moja ya misiba mikubwa zaidi katika historia ya Tanzania, ukikaribia ule wa Mwalimu Julius Myerere mwaka 1999, hayati Edward Sokoine mwaka 1984, hayati Abeid Amani Karume mwaka 1972 na hayati Rashid Kawawa mwaka 2010.

3. Dk. Steveni Ulimboka: Aliteswa vibaya katika msitu wa Pande alikopelekwa baada ya kutekwa kutoka katika eneo la Leaders Club, Kinondoni Dar es Salaam. Hata hivyo, kwa kudra za mwenyezi Mungu aliokolewa na Juma Mgaza, Msamaria mwema aliyefanya tendo la kijasiri la kumchukua na kumpeleka hospitali

4. Elizabeth Michael ‘Lulu': Jina lake lilivuma sana tangu siku Steven Kanumba alipopoteza maisha na baadaye, Aprili 11, Lulu akasomewa mashtaka ya kuhusika na kifo hicho. Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 5 iliyopita, jina la Lulu ndilo likawa la msanii wa kwanza wa kike kulipita lile la Wema Sepetu kwa kuandikwa ama kuzungumzwa mara nyingi zaidi nchini.

5. Daudi Mwangosi: Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel 10 ambaye Septemba 2012 aliuawa kwa bomu/risasi na polisi huko Iringa wakati wa mkutanowa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tukio hili lilisababisha simanzi, malalamiko, maandamano, kupungua kwa imani ya raia kwa polisi na hatimaye kuundwa kwa Tume mbili tofauti za uchunguzi wa jambo hilo.

6. Edward Lowassa: Waziri Mkuu zamani wa Tanzania aliyelazimika kujiuzulu wadhifa wake kwa kashfa ya Richmond na Mbunge wa Monduli alivunja ukimya Machi 15, 2012 aliporejea kutoka matibabu nchini Ujerumani na kusema kuwa yuko fiti kisiasa. Baadaye akashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Halmashauri Kuu ya CCM na jina lake likazidi kung'ara kama mmoja wa wale wanaotishia kwa kasi uteuzi wa mgombea Urais kupitia CCM na imefikia wakati sasa gumzo mtaani ni swali kwamba kama kuna ‘mbabe' ndani ya CCM anayeweza kupambana naye kwa namna kasi yake inavyozidi kutisha.

7. Sheikh Ponda Issa Ponda: Mwenyekiti wa Shura ya Maimamu alivuma kila mara madai, maandamano, ghasia na tafrani za waumini wa Kiislam zilipotajwa, pamoja na kesi ya jinai dhidi yake ambayo inaendelea ilipotajwa mahakamani. Aliongoza pia jaribio lililokwama la kuhamasisha Waislam wasishiriki zoezi la Sena lililofanyika kote nchini Agosti 26.

8. Sheikh Farid Hadi Ahmed (Kiongozi wa Kundi la Uamsho Zanzibar): Tuhuma za utekwaji wake nyara zilisababisha machafuko na kuuawa kwa watu Zanzibar katikati ya mwezi Oktoba. Baadaye alionekana, kukamatwa na kushtakiwa kwa kesi za kuhatarisha amani ya nchi.

9. Wema Sepetu: Kwa miaka mitano hivi sasa jina la Wema Sepetu limeendelea kuwa na mvuto miongoni mwa wafuatiliaji wa masuala ya filamu na skendo za wasanii. Kama kawaida, jina lake liliendelea kupamba na ‘kuuza' katika magazeti mbalimbali.

10. Godbless Lema: Mbunge machachari wa CHADEMA aliyerejesha Ubunge wake wa jimbo la Arusha Mjini Desemba 2012 baada ya Mahakama ya Rufaa kutokubaliana na hukum ya Aprili 5, 2012 ya Jaji Rwakabalira aliyempokonya Lema ubunge huo.

11. Zitto Kabwe: Alivuma kama miaka yote tangu alipoanza siasa na hasa shinikizo aliloliongoza kupinga matumizi mabaya ya fedha za umma na hivyo kuanza mchakato bungeni wa kukusanya saini 70 za wabunge sawa na asililimia 2, Aprili 19, ya idadi inayohitajika kukidhi kifungu cha 133(1) cha Kanuni za Bunge kinachohusika na uletwaji hoja rasmi ya kumwajibisha Waziri Mkuu kwa kutokuwa na imani naye. Jambo hili lilichangia kujiuzulu Mawaziri wanane. Alizidi kutajwa pia Urais wa 2012..

12. Tundu Lissu: Mwanasheria na mwanasiasa huyu machachari aliyetamba sana 2012. Nyota yake iling'ara zaidi alipoongoza timu ya mawakili iliyofanikisha kulishawishi jopo la Majaji watatu wa Mahakama kuu kutengua hukumu ya jaji Gabriel Rwakabalila iliyokuwa imempokonya Ubunge mbunge Godbless Lema wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA. Lissu mwenyewe Aprili 26, 2012 alifanikiwa kulitetea jimbo lake baada ya kushinda kesi ya pingamizi dhidi yake iliyotupiliwa mbali na jaji Moss Mzena wa Mahakama Kuu. Lissu tena alisikika kwa nguvu Julai 13, 2012 kwa kumshambulia Rais Kikwete kwa tuhuma za kuteua Majaji wa Mahakama Kuu wasiokidhi viwango vya kitaaluma na utendaji kazi. Halafu akataja hadharani bungeni majina ya wabunge aliowatuhumu kuhusika na rushwa ndani ya Kamati ya Nishati na Madini.

Ripoti ya Jenerali Ngwilizi haikuona kashfa yeyote kati yao kuhusika.
SOURCE:Nipashe

Dr Slaa anawaumiza sana vichwa hawa VIMETA, japo ya wezekana ni kweli kutokana na shughuli zake za sasa kuwa za kimkakati zaidi, hii inaweza kuwa ya kweli sema mapenzi yetu kwa Dr Slaa
 
Bila Mnyika sikubali kabisa,kaongoza kutoa michango bungeni,na alimchana live mkuu wa kaya kwa udhaifu.
 
1. Jakaya Kikwete: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kama alivyo baba mwenye nyumba, jina lake lilitajwa kila mambo mazito yalipotokea nchini.

Baadhi ya makubwa yaliyojiri ikiwemo kulaumiwa kutokana na kukithiri kwa ugumu wa maisha ya watanzania na matukio ya migomo ya madaktari, utekwaji wa Dk. Ulimboka, mauaji ya mwandishi wa habari wa Channel 10, David Mwangosi, ghasia za kisiasa na kidini, uteuzi wa majaji, mgogporo wa Ziwa Nyasa na kadhalika.

Alisifiwa katika uundwaji wa Tume ya Katiba, uteuzi wa Baraza jipya la mawaziri alioufanya baada ya kujiuzulu mawaziri wanane mwanzoni mwa mwaka, uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara, uvumilivu wa kisiasa, mabadiliko katika safu ya juu ya CCM, na kadhalika.

Tume ya katiba haikuundwa kwa hiyari yake bali ni shinikizo kiongozi mwenye vision anafanya kazi kwa kuweza kuona
mahitaji ya jamii yake na si kwa shinikizo.

uteuzi wa baraza la mawaziri ilibidi iwe hivyo tume imeundwa wahusika wote wameonekana hawafai kwahiyo unamsifu
kwa kuwaondoa watu ambao wameshaonekana hawafai???

miundo mbinu hatuangalii idadi ya barabara tunaangalia ubora wa kile kinachotumia mkopo wa mabilioni ya dola kama
vile shule hatuangalii idadi ya shule zinazojengwa tunaangalia ubora wa kile kinachotoka ndani ya shule hizo ambazo
watanzania wote tumejonea kuwa ni aibu tupu kwa taifa.

uvumilifu wa kisiasa hakuna kwani ndiye kiongozi pekee Tanzania kwa kuwa na idadi kubwa ya watu kuhuliwa kwa
sababu za kisiasa bila kuchukuliwa hatua yeyote. suala la kufanyika mikutano ni suala la kikatiba na siyo fadhila yake.

Uongozi mpya ndani ya CCM. kama unawaona wakina mangula na kinana ni viongozi wapya Good luck njoo nitakuuzia
gari langu la mwaka 1985 jipya kabisa.
 
Lulu na Sepetu wamemzidi Mhe Halima Mdee,pamoja na mambo mengine hoja yake ya masuala ya ardhi ilitikisa sio TZ tu hata nchi jirani.Kwa mtizamo wangu katika wanawake wote yeye alitia fora
 
huu sio utafiti bali ni wewe umeona hivyo lakini kwa tafiti ambazo tunajua siwezi kukubaliana na wewe hata kidogo
 
Ifuatayo ni orodha ya watanzania 100 waliovuma zaidi mwaka 2012, kulingana na utafiti maalum uliofanywa na NIPASHE kwa kuangalia majina ya Watanzania yaliyoripotiwa zaidi na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi, kitaifa na kimataifa. Utafiti huu wa mwezi mmoja ulirejea taarifa kupitia mtandao na tovuti maarufu kama Google, Yahoo, Facebook na Twitter.

Mbona sio 100 ni 12? Halafu siamini kama hakuna Nape,dk Slaa,Mnyika au Diamond.pia sidhani kama hao mashehe wawili wamekuwa maarufu kiasi hicho cha kuwa top ten.
 
Huu ni ule utafiti wa kijinga wa akina Dr Bana bila Dr Slaa, Mbowe na Mnyika na Lissu akawa wa nne huu ni upumbavu tuu
 
Bila Dr Slaa na Mbowe hii taarifa haijakamilika.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hii ipo kisiasa zaidi,MAMVI amebebwa,huwezi kumuacha dr Slaa hapa.huu ni uchochezi
 
Back
Top Bottom