Watanzani tuna uelewa zaidi wa kiingereza?

fikirini

Senior Member
May 24, 2011
114
22
Binafsi huwa naumia sana na kujiuliza maswali mengi, ukichunguza karibu maeneo yaliyomengi hasa ya kibiashara utakuta huduma husika imetambulishwa kwa kiingereza mbaya zaidi kiingereza chenyewe cha kukosea....mf: hair cutting saloon badala ya hair cutting salon., kamgahawa tu unakuta kanaitwa hotel, inn..kweli wanajua maantiki ya maneno haya ya kiingereza? watu wengi wamekuwa wanakwama kutambua huduma fulani inapatikana wapi kutokana na lugha iliyotumika, juzi jamaa kaenda kuulizia paracetamol kwenye duka la autoparts!
Taabu yote hii ya nini, wakati tuna lugha yetu ya kiswahili maridhawa kabisa
Nawasilisha kwa masikitiko
 
Kweli kabisa mkuu. kama ulivyosema wanaandika:

Saloon badala ya salon
Stationary badala ya Stationery
Vitu vya hovyo hovyo vinapewa lebo za "hotel, inn, enterprise, company ltd, supermarket, etc"
hahaha!

Wateja wao ni waswahili toka kwa Tandale kwa Mtogole lakini utakuta wanaandika kwa hicho "kiingereza" chenye makengeza. Ulimbukeni tu.
 
unajua ndugu yangu watu wanashindwa kutambua maeneo muhimu ya kutumia maneno haya mfano unakuta mtu kaandika chicken chips. baada ya kuandika( take away food) au unakuta mtu kaandika cafe hivi hawa watu nadhani wanatakiwa kwenda shule ili wakajifunze wasipotoshe lugha za watu.
 
Inatia aibu sana,pale tandale kwa mtogole,nliona "show shaini" badala shoe shine,kila daladala likipita unasoma,aibu hii mpaka lini?
 
kwa kuharibu kiingereza hatujambo...utasikia watangazaji wa redio..ajali imetokea barabara ya mandela road.
 
tatizo ni kutaka kila mtu anataka aonekane kuwa anaweza lugha ya kiingereza matokeo yake ni aibu. utasikia tangazo kwenya runinga "changamkia nafasi hii spesheli"
 
Jamani wana jf kiingereza ni moja ya lugha inayozaa sana lugha nyingi nyingize zinazofanana kulingana na jamii husika na mazingira yaliyopo, sidhani kuwa ni makosa wala la kushangaza,, ndio maana utakuta pana nigerian english/ kenyan english/Indian english unapotokea sehemu tofauti yaweza tokea kuelewana kabisa kwenye baadhi ya matamushi na maandishi na ni matokeo ya matumizi dhaifu/mabovu ya kiingereza bila kuelewa,,, pana baadhi ya wataalam wanadai kwamba TZ inatumia na kuongea kiingeraza vizuri zaidi kuliko hata kenya,uganda JE UTAAMINI ? Unaweza kuhakikisha hapa ...http://en.wikipedia.org/wiki/List_of_countries_by_English-speaking_population
 
Achana na lugha ya watu, mpaka waheshimiwa wanaingia mkenge kwenye mambo ya mikataba we acha tu!!
 
unajua ndugu yangu watu wanashindwa kutambua maeneo muhimu ya kutumia maneno haya mfano unakuta mtu kaandika chicken chips. Baada ya kuandika( take away food) au unakuta mtu kaandika cafe hivi hawa watu nadhani wanatakiwa kwenda shule ili wakajifunze wasipotoshe lugha za watu.
kiswahili cha chips ni viazi vya kukeketa.
 
Watanzani kila sehemu aibu. Tumeamua kudumaza lugha yetu ya taifa (Kiswahili) bila sababu ya msingi!
 
Hivi bora kuacha kabisa kingereza ao bora kuandika kwa kiingereza (ili tuweze kua competitive) alafu tutoe maelezo kwa kiswahili?
ex: Beauty Salon (tunatoa huduma za kutengeneza nywele, kucha, ngozi na kadhalika)?
 
Binafsi huwa naumia sana na kujiuliza maswali mengi, ukichunguza karibu maeneo yaliyomengi hasa ya kibiashara utakuta huduma husika imetambulishwa kwa kiingereza mbaya zaidi kiingereza chenyewe cha kukosea....mf: hair cutting saloon badala ya hair cutting salon., kamgahawa tu unakuta kanaitwa hotel, inn..kweli wanajua maantiki ya maneno haya ya kiingereza? watu wengi wamekuwa wanakwama kutambua huduma fulani inapatikana wapi kutokana na lugha iliyotumika, juzi jamaa kaenda kuulizia paracetamol kwenye duka la autoparts!
Taabu yote hii ya nini, wakati tuna lugha yetu ya kiswahili maridhawa kabisa
Nawasilisha kwa masikitiko

"Watanzani tuna uelewa zaidi wa kiingereza?" Hawa Watanzani ni watu wa wapi hawa?

Mkuu, unahukumu wakati na wewe hata kuandika "Watanzania" ni tabu. Tutafika kweli? Soma kichwa cha mada.

Maana, kule wanasema "were you at?" Huko hiyo sentensi ni kosa.
 
Hivi bora kuacha kabisa kingereza ao bora kuandika kwa kiingereza (ili tuweze kua competitive) alafu tutoe maelezo kwa kiswahili?
ex: Beauty Salon (tunatoa huduma za kutengeneza nywele, kucha, ngozi na kadhalika)?

Tafuta makosa ya lugha hapo kwenye quote.
 
Moja ya vigezo vya kuitwa ulimwengu wa tatu ni pamoja na uliyoyataja. Wewe mwenyewe wajua sheria za misosi? Wajua uma unakamatiwa mkono gani? Wajua kuku..nguruwe..na samaki ni nyama nyeupe? Na wajua kama inalika ikiambatana na white wine..divai nyeupe? Wajua iwapo nyama nyekundu i.e ng'ombe..mbuzi..etc inaondoka na redwine? Wajua kama misosi ina dishes nne? Soup....ya ngegere..beans et...wa pili starter...hii ni salad mazee...kachumbali kiaina....tatu main dish..yaani mlo kamili i.e chicken chips...nne....desert hii ni ice cream ama cake na kahawa chungu....iitwayo ESSPRESSO..ama CAPPUCINO mapovu ya maziwa moto na kahawa ndani yake. Je wajua suits zina majina? Wedding..dinner suit nk. Unazo? Unazitambuaje? Consults wauza pamba proffessionals sio maduka ya sharobaros sinza...hamna kitu hapo ni wajanja wajanja tu kutoka mbuguni na wakinga Iringa
 
unajua ndugu yangu watu wanashindwa kutambua maeneo muhimu ya kutumia maneno haya mfano unakuta mtu kaandika chicken chips. baada ya kuandika( take away food) au unakuta mtu kaandika cafe hivi hawa watu nadhani wanatakiwa kwenda shule ili wakajifunze wasipotoshe lugha za watu.
<br />
<br />
embu eleza vizuri juu ya hiyo chicken chips na take away food kwani kwa ulivyoandika haileti maana ya unavyotetea hoja
 
uelewa wenyewe wa lugha yetu unafifia kwa kuathiriwa na lugha ya pili/tatu ya kiingereza. hiyo ya kusema "saloon" badala ya "salon' ni kutokana na kuwa incompetent kwenye lugha ya kiingereza.lakini tusilaumu pale mtu anapochanganya lugha tunaita "codemixing" au 'codeswitching'. hiyo inatokea automatically mtu akiwa na lugha zaidi ya moja.cha msingi ni kuelewa maana ya maneno na namna au mahali yanapotakiwa yatumike!
 
Back
Top Bottom